Team Lowassa walikuwa disorganised!

Team Lowassa walikuwa disorganised!

alikuwa anakomaaa tu sababu ya pesa lakini hakuwa sawa kwa kazi ya urais
 
Hii hoja ya kwamba kukatwa kwa Membe imewapooza mashabiki wa Lowasa ni hoja hafifu sana, Malengo yalikuwa EL agombee uraisi kupitia CCM hivyo kimkakati Membe hakuwa threat kabisa, kifupi ni umafia tu umetendeka kukata jina lake tokea kamati ya usalama na Maadili....
Kwa umri wa Lowasa hana cha kupoteza endapo atajitoa ndani ya CCM na kwenda kupitishwa na chama kingine kuwa mgombea uraisi kutimiza ndoto yake hiyo.... Ukweli ni kuwa kokote atakapoenda kwa upepo ulivyo sasa EL atakuwa ni zaidi ya threat kwa CCM.
kwa historia ya ukanda wetu huu wa Africa mashariki vyama tawala vilivyowapa Uhuru nchi nyingi vilianguka pale tu ambapo mtu aliyekubalika ndani kukatwa na kuamua kwenda kujiunga na vyama pinzani e.g Kenya & Zambia
Hivyo kwa kufuata historia hiyo EL bado ana fursa kubwa sana ya kufanya maajabu kwa kipindi hiki kifupi kilichobaki kuelekea uchaguzi mkuu akiwa njee ya CCM.

Regards
Cosmas
Mchambuzi Huru.



naamini akitaka avurugikiwe aende huko nje. ni salama kwake kubaki ndani. watu wasafi na wenye wapiga kura wengi ndio huwa na ujasiri wa kutoka nje ya chama na kufuatwa na watu.

kwa yeye akifanya hivo atakuwa amejilostisha zaidi. kila mtu anamcheka na kumshangaa.

nguvu ya mwanasiasa ni watu - wapiga kura. lakini yeye hana rekodi nzuri na wapiga kura - watu wa kawaida. ukitaka kujua kuhusu hili angalia alivyoshindwa kuwabeba akina batilda na sumari.

hao wapiga debe wenyewe wakipiga kura kwa siri wanaweza hata mtosa. na walipatikana kwa kupewa mapene na kuahidiwa nafasi pamoja na kutegemea nafasi - ubinafsi. ahadi za sampuli hii huwez kuzitoa kwa wapiga kura wote na wala huwezi gawa hela kwa wapiga kura wote
 
Lowasa hajatumia pesa zake toka mfukoni pesa nyingi alichangiwa na marafiki isitoshe Lowasa ni tajiri ana Mali nyingi hawezi kuchoka ataishi maisha ya kushiba bila njaa Kama Raila Odinga , wafuasi wa Lowasa wengi sasa wamehamia kwa magufuli kwani Adui wa Lowasa alikuwa Membe na sasa Membe kakatwa wameamua kumuunga mkono magufuli hawaendi kokote.

vp ule msemo wa huwezi zuia mafuriko kwa mikono umeishia wapi?
 
Kama mwaka mmoja lowasa alishaulia kuwa Na plan b akawa mbongo kweli yaliyotokea sasa no historian hawakuwa Na mkakati mbadala
 
Timu Membe si watulivu bali walikuwa wachache sana na wengi walikuwa waganga wa kienyeji na vijana wa kushinda kwenye mitandao kupika uongo, uzushi na kila mbinu za kumchafua Lowasa , Membe yeye aliwatumia Nape, jack Gotham na Timu za kimafia ambazo sasa zimejikausha tayari na hawana kazi wameludi mitaani .
Kwani timu ya Membe ndiyo ilikuwa imemtuma ama kumshauri team Lowassa kufanya mbwembwe zilizozidi kimpimo hadi kuwafanya wananchi kuanza kujisikia kichefuchefu? Mimi ninafikiri mzee wa maamuzi magumu na timu yake kwa kiasi kikubwa walijichafua wenyewe. Walijitia upofu na ukiziwi wakalewa ukwasi ambao hapana shaka ulisababisha mafuriko ambayo hata hivyo yameweza kuzuiwa kwa vidole viwili tu! Tunamshukuru Muumba kwa hilo. Ninakubaliana na mJF mmoja ambaye amesema zuio hilo limetupunguzia mafisadi kadhaa.
 
Ina maana kama lowasa alikuwa chaguo la wengi,mbona haongelewi popote?
Subiri uone tofauti ya CDM na ZZK na CCM na Lowasa...mimi nitamuongelea km ccm walivyomuongelea ZZK,Lowasa anaongelewa na wana CCM na wasio CCM kwa malengo tofauti kwa sasa NChi nzima.
 
Ni wazi hii ndio team pekee iliyokuwa na rasilimali fedha na watu lakini ilikosa uongozi au weledi.Tazama siku ya uzinduzi wa safari ya matumaini ilikuwa ni vurugu tupu.Hilo linaonekana mpaka sasa kwa kuwa baada ya kukatwa team hii imepagawa na kuchanganyiwa kabisa.1-Kuna kundi limechana kadi za ccm.2-Kuna kundi limetangulia ACT3-Kuna kundi limebaki kimya ndani ya ccm4-Kuna kundi limemsapoti magufuli5-Kuna kundi linatishia kwenda CDM6-Kuna kundi halijulikani linafanya nini Bashe yuko kimyaa!Kingunge yuko kimyaa!Nchimbi,Simba na Kimbisa hatukusikia kama waliwasilisha ile rufaa yao au la.Yale mabasi ya Team lowassa hayajulikani yalipo yaani ni full chaos.Hii ni ishara tosha ya kutokujipanga kwa Team hii.kwa upande wa Team membe bado ni watulivu
usichojua ni kwamba hiyo disorgazation dio shida kubwa kwa ccm..akiwa ndani ya ccm.Msizo usiofungwa au kuweka ktk mpangilio ktk ndege huangusha ndege
 
ha ha ha ha, mungu anaangalia mwisho na sio mwanzo. Kwisheny, Lowasa hakuwa na ma strategist bali aliwa confuse washikaji na watekaji. Hiyo safi sana International school ya Wakina Lau, kinje Joseph kusaga karudi toka Dubai akijua ushindi ni wao, ephramim kibonde, Bashe, Kingunge, nchimbi sofia simba ndio vichwa cha Mamvi, pole sana hata, ile nyomi ya mafisadi Arusha ndio aliona imemtoa, pale pale wakali tulichua kachemsha, kweli sayansi haina siasa, kila tulichoon kimetokea hakuhitaji expatriate kujua kama hamnazo, kweli akili ni nywele

Ufisadi ccm upo kila kona hakuna msafi wala Mtakatifu asiye na Dhambi ccm. Lowasa hajakwisha kwani Lowasa ni Tajiri isitoshe alikuwa kajiandaa Kwa Ajili ya kampeni ana pesa za kampeni na hazikutumika zilitengwa kutumika October na hatashiriki Uchaguzi pesa inabaki , kwenye kutafuta kuna kukosa na kupata alijiandaa kwa hilo ndiyo maana yupo ccm hana mpango wa kuhama kwenda popote.
 
Lowasa alizungukwa na money mongers na si wafuasi

Tambua kuwa Lowasa hata angekuwa na Timu kutoka Mbinguni asingepenya kwani Jk na watu wake walikuwa wanataka kumpenyeza Membe , lakini dk za mwisho wakabaini kuwa watachemsha vibaya endapo wangefanya hayo maamuzi ndipo wakahamia Kwa magufuli dakika za majeruhi , lakini hii haimpi Lowasa shida kwani ana vitega uchumi vingi hawezi kulala njaa maisha yataendea Kama kawa.
 
Hawa team ya Lowasa watakiwa wameenda kujitumbikiza baharini kuogopa aibu

Aibu ipi ? Kwenye kutafuta na kupata na kukosa , Lowasa alijua njama za kumwengua mapema hivyo alijiandaa Kwa lolote lile.
 
Lowasa yupo imara Kama Raila Odinga alijua mapema kuwa kuna kukosa ama kupata hawezi kuishi maisha ya shida alishajipanga vizuri siku nyingi Timu yake sasa wapo wamehamia Kwa magufuli maisha yaendelee.
 
''ilibidi mwana wa adamu asulubiwe ili unabii utimie'' ogopa sana watu wamekiuka taratibu za uteuzi wa kamati kuu ili wamuondoe mapema, kwanini wazee wa chama walikutana kwa dharura?, ilikuaje kamati ya maadili ifanye kazi ya kamati kuu kumkata mmasai? kwa iyo unaona jinsi unabii uliotabiriwa umetimia ndio maana hata wewe umepata cha kuandika apa jf, ukawa watapata kiki ya kampaini pia hata kama lowasa akisema wafuasi waingie mtaani itakuwa mambo ya nkurunzinza. kiujumla nazidi kuendelea kumuheshimu lowasa kwa uzalendo, uvumilivu na busara yake kunyamaza kimya waswahili wanasema ''mtu mzima akivuliwa nguo huchutama''
 
Na hii disorganisation imeingia rasmi ndani ya Chadema.
 
Back
Top Bottom