Jamani tuache maneno na kejeli, Team Lowassa wameshindwa, tena wameshindwa vibaya. Walijipanga vizuri sana kuliko kambi yoyote ile ya wagombea CCM, Lakini kila mtu ameona nini kilichotokea, haikuwa siasa iliyowafanya washindwe, bali Zengwe Zitto, Goli la Mkono.
Mipango yote ya Team Lowassa inategemea sana mwelekeo wa Lowassa mwenyewe, kama mwenyewe yuko kimya, msitegemee kuna mtu yoyote wa Kambi yake atakuja na issue yoyote ya maana.
Mahali popote Team ikishindwa hali inakuwa kama Msiba, mambo yote yanavurugika kabisa. Jambo kama hili lilimpata pia Kikwete 1995.
Busara pekee ni kukaa kimya na kumalizia issue kimya kimya.
Litakuwa ni jambo la ajabu kabisa kama Team Lowassa hawakuwa na Plan B, hata mimi nitashangaa sana. Sometimes kukubali kushindwa nako kunaweza kuwa ni Plan.
Kushindwa kubaya sana. Poleni Team Fisadi Lowassa, hiyo ndio CCM na CCM ina wenyewe!!