TCU wameua ndoto yangu

TCU wameua ndoto yangu

kwel kabisa, mimi nilipata 1:9 CBG,kutokana na kutokuwa na pesa za kwenda private maana advanc yenyew nilimaliza kwa mbinde though michango kwa ujumla haizid lak 4 kwa mwaka, nikaamua kuomba vyuo vya serikal kwa program za afya! kutokana na admission capacity kuwa ndogo sana kwa udom, muhas, ajuco nikaamua kuweka education kama last priority ili nikikosa afya bac nipate hata eductn kwa chuo ninachokipenda! na mambo ya kawa ivy nimechaguliwa ed na sijajutia maamuz yang maana ilikuwa hamna namna. N.B ufaulu wa 2.11 ni kawaida sana kwa mwaka huu! tena unasema huna pesa za kutosha kwenda privat kama vile bugando,st joseph, khairuk! nilitegemea hata 2nd selectn ungeweka educatn! mi nakushaur nenda tu education ndo bongo edc
umenena mkuu coz wengi tulioenda education hatukupenda bali hali ya uchumi wa nyumbani ndio iliotupeleka uko education coz ya mkopo tu
 
Inauma sana kaka mwenyewe ni mmoja ambae malengo yangu yamekwama ila mi mimeacha nijaribu bahati mwakan
 
Usikae bure mwaka mzima kama vipi omba tempo ufundishe tena kwa masomo yako uhitaji ni mkubwa sana
 
Nakumbuka nilipokuwa mtoto watu wazima wakiniuliza,"ukiwa mkubwa unataka kuwa nani?" niliwajibu "nataka kuwa daktari kwani napenda nije kuwasaidia wagonjwa"

Wazazi wangu ni maskini lakini hawakutilia shaka na uamuzi wangu.Walijitahidi kwa hali na mali ili nifikie ndoto yangu.Walilipa karo zangu za shule na hata pesa kwa ajili ya tuition.

Nilipofika A level nilijitahidi sana kwenye masomo yangu ya mchepuo wa PCB.Wazazi wangu hawakuwa nyuma kunipa msaada wa kimawazo na pesa pale ilipohitajika kunilipia tuition na kununua mavitabu makubwa kama BS,Chand,Nelkon na mavitabu mengineyo ingawa hali yao kiuchumi haikuwa nzuri.

Picha lilianza pale NECTA walipobadilisha gia kwa kupandisha grades tukiwa kwenye hatua za mwisho za kumaliza kidato cha sita.Lakini hilo halikunishtua sana nilijitahidi sana bila kukata tamaa ingawa sikusoma shule bora sana.

Matokeo yalipotoka sio haba nilipata Div 2.11 yaani DDC, nikajipa moyo kwamba nitachaguliwa medical school.Part two ya picha ilikuja pale TCU ilipovifungia baadhi ya vyuo ambavyo vinatoa course za afya na kupunguza admission capacity kwenye vyuo vilivyobaki.

Nimepigwa danadana katika selections kutoka 1st round hadi 3rd round.Roho imeniuma pale nilipoona hata hii 3rd round haina vyuo za afya.

Nimebaki kushika tama, medical school ni jambo la kusikika tu kwangu.

Ndoto yangu tayari imeyeyuka.
Ndugu ndoto zako bado hazijafa, bado Sana, usikate tamaa , Jipange upya. Mimi binafsi nakushauri airisha Mwaka na apply tena mwakani wakati ukijua namna gani ya kuapply ili system isikuteme tena, coz una matokeo mazuri ila nadhani ulikosa elimu ya kuapply kitu ambacho wanafunzi wengi kinawatatiza. Hizo ni changamoto tu, All da best
 
Laiti ungeomba hata ualimu, pole mwanangu,
tutasoma hadi tarakimu za kirumi.
 
Div 2,pcb wanakuacha?kweli hawajakutendea haki.cku hizi toka magu aingie mambo hayaeleweki eleweki yani.cjui wanatumia vigezo gani kudahili
Usikimbilie kwa Magu, hii system ya tcu na kutema watu imeanza 3years back huko, jifunze udahili unafanyikaje then ndo ujudge, nilishatemwa but nilifuatilia na kujua wapi nilikosea
 
Wahi apply diploma clinical medicine your dream will come true
 
je kama mwakani watoto kipasua zaidi atafanyaje?
sasa hivi ukitaka uhakika wa kwenda MD lazima uwe na div1.
cha kufanya kwa sasa aende akasome diploma tu, TCU wakifungua maombi aombe tena akifanikiwa kupata hiyo MD anaachana na hiyo diploma. kuliko kupoteza mwaka mzima mtaani
Hukunielewa
Tatizo yy anataka udaktari tu
Digrii kuapply course zingine sidhani km atakosa
Uamuzi ni wake kwani ht diploma washaanza kubana hii serikali ya sasa utakuta nafasi vyuo vya serikali zimejaa na pia akipata hadi afikishe GPA 3.0,ndo ataenda digrii
 
jana niliona pale nacte mtu ana 2 kaambiwa hastaili kusoma ata diploma kapangiwa asome nursing na yeye ni kidume kwaiyo ataki..... akauliza sababu nini wakamjibu sisi atuangalii ulichopata kidato cha sita tunaaangalia kidato cha nne.... alipata B physics...B biology.......C mathe na D chemistry..... wakamwambia bola kidogo iyo D angepata kwenye physics coz hawaangalii sana.... kwakuwa amepata kwenye chemistry hastaili kusoma afya diploma...... aisee amelia yule kaka
Umeongea point kuna watu hawathink twice
 
ana div 2 asome diploma?
Kuna mtoto wa ndg yangu alipata Div 1 lakini akaenda Diploma ya Marine Engineering ili kutimiza ndoto yake ya kuwa Engineer wa Meli. Mwakani anaingia First Degree. Usishangae.
 
alikosa washauri
Hujui usemalo, Div 1 ilikuwa ya nini? Not Science! Diploma ametumia cheti chake cha Form 4 ambacho kina Science subjects na combination nzuri. Hiyo Div 1 ya A level hangeweza kuingia nayo Diploma Marine labda angeenda Law.
 
Hujui usemalo, Div 1 ilikuwa ya nini? Not Science! Diploma ametumia cheti chake cha Form 4 ambacho kina Science subjects na combination nzuri. Hiyo Div 1 ya A level hangeweza kuingia nayo Diploma Marine labda angeenda Law.
Sasa case yake na mleta mada ni tofauti
Ungefafanua mapema
 
hautakiwi kulalamika mdogo wangu,ushauri wangu fanya haraka uombe dip in clinical medicine kupitia nacte ni miaka 3 tu,ukimaliza unaweza ukaendelea na MD,ingawa ni njia ndefu itakulazimu uvumilie tu cz wenzako wengi waliotemwa wameamua kukimbilia huko.
Usikae makuanza kulalamika haitokusaidia chukua hatua
Hii ni njia sahihi zaidi
 
Hujui usemalo, Div 1 ilikuwa ya nini? Not Science! Diploma ametumia cheti chake cha Form 4 ambacho kina Science subjects na combination nzuri. Hiyo Div 1 ya A level hangeweza kuingia nayo Diploma Marine labda angeenda Law.
kama mkuu alivyosema hapo juu, hio ni wastage of time coz kama dream zake zilikua hizo kulikua hakuna haja ya kusoma A level angeenda tu moja kwa moja Diploma.

wastage of time plus resources. ndo mana nasema alikosa washauri.
 
Back
Top Bottom