nyambari
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 355
- 171
Hebu angalia ni jinsi gani watu wasivyokuwa serious yaani TCU si ndo wanaregulate vyuo vikuu vyote Tanzania inakuwaje wakati wa kufanya selection wanafanya nusunusu wao si wana idadi kamili ya wanafunzi wanaohitajika kwa kila chuo na hawa wanaochaguliwa zamu hii mkopo watapewa au ndo mambo yale ya budget exhaustion
[FONT=Cambria,Bold][FONT=Cambria,Bold] Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
TAARIFA KWA UMMA
[/FONT][/FONT][FONT=Cambria,Bold][FONT=Cambria,Bold][/FONT][/FONT] Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania inautaarifu umma kuwa
utaratibu wa kuomba udahili kwa vyuo vya elimu ya juu
ambavyo bado vina nafasi unaandaliwa na kwa mantiki hiyo
wale wote ambao hawana udahili kwa sasa na wangependa
kuomba kujiunga na vyuo hivyo katika mwaka wa masomo
2011/12 wasubiri mpaka utaratibu huo utakapotangazwa na
Tume kuanzia tarehe 26 Septemba 2011.
Matangazo ambayo yametolewa na Chuo Kikuu cha Dar es
salaam kuitisha udahili zaidi kwa sababu ya chuo hicho kuwa
na nafasi katika programu mbalimbali ni ishara kwamba bado
kuna nafasi katika programu za chuo hicho na hivyo
wanafunzi wasubiri utaratibu wa kuomba udahili katika vyuo
utakapotangazwa na Tume kuanzia tarehe 26 Septemba 2011
ili kuepuka usumbufu wanaoweza kuupata hapo baadaye.
Kwa taarifa hii vyuo vikuu vyote nchini vinataarifiwa
kusubiri utaratibu utakapotangazwa kabla ya kutoa
matangazo yao. Pia vyuo vyote vya elimu ya juu ambavyo
bado vina nafasi kwa ajili ya wanafunzi kwa mwaka wa
masomo wa 2011/12 vinataarifiwa kutuma taarifa hizo kwa
Tume ili programu husika ziweze kuongezwa kwenye mfumo
kabla ya tarehe 26 Septemba 2011.
[FONT=CenturyGothic,Bold][FONT=CenturyGothic,Bold] Katibu Mtendaji
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA
Heri ya miaka 50 ya Uhuru
[/FONT][/FONT][FONT=CenturyGothic,Bold][FONT=CenturyGothic,Bold][/FONT][/FONT]