Tcu: Taarifa kwa umma

nyambari

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
355
169
Hebu angalia ni jinsi gani watu wasivyokuwa serious yaani TCU si ndo wanaregulate vyuo vikuu vyote Tanzania inakuwaje wakati wa kufanya selection wanafanya nusunusu wao si wana idadi kamili ya wanafunzi wanaohitajika kwa kila chuo na hawa wanaochaguliwa zamu hii mkopo watapewa au ndo mambo yale ya budget exhaustion

[FONT=Cambria,Bold][FONT=Cambria,Bold] Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania
TAARIFA KWA UMMA
[/FONT]
[/FONT]
[FONT=Cambria,Bold][FONT=Cambria,Bold][/FONT][/FONT] Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania inautaarifu umma kuwa
utaratibu wa kuomba udahili kwa vyuo vya elimu ya juu
ambavyo bado vina nafasi unaandaliwa na kwa mantiki hiyo
wale wote ambao hawana udahili kwa sasa na wangependa
kuomba kujiunga na vyuo hivyo katika mwaka wa masomo
2011/12 wasubiri mpaka utaratibu huo utakapotangazwa na
Tume kuanzia tarehe 26 Septemba 2011.
Matangazo ambayo yametolewa na Chuo Kikuu cha Dar es
salaam kuitisha udahili zaidi kwa sababu ya chuo hicho kuwa
na nafasi katika programu mbalimbali ni ishara kwamba bado
kuna nafasi katika programu za chuo hicho na hivyo
wanafunzi wasubiri utaratibu wa kuomba udahili katika vyuo
utakapotangazwa na Tume kuanzia tarehe 26 Septemba 2011
ili kuepuka usumbufu wanaoweza kuupata hapo baadaye.
Kwa taarifa hii vyuo vikuu vyote nchini vinataarifiwa
kusubiri utaratibu utakapotangazwa kabla ya kutoa
matangazo yao. Pia vyuo vyote vya elimu ya juu ambavyo
bado vina nafasi kwa ajili ya wanafunzi kwa mwaka wa
masomo wa 2011/12 vinataarifiwa kutuma taarifa hizo kwa
Tume ili programu husika ziweze kuongezwa kwenye mfumo
kabla ya tarehe 26 Septemba 2011.

[FONT=CenturyGothic,Bold][FONT=CenturyGothic,Bold] Katibu Mtendaji
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA

Heri ya miaka 50 ya Uhuru
[/FONT]
[/FONT]
[FONT=CenturyGothic,Bold][FONT=CenturyGothic,Bold][/FONT][/FONT]
 

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Wizi mtupu,. Ninavyojua kila chuo kinatoa idadi ya wanafunzi wanatakiwa kwa kila kozi. Hii imekaaje tena?
 

babayah67

JF-Expert Member
Mar 28, 2008
493
78
Hilo Tangazo la TCU limetoka jana last week. Hadi hii leo tarehe 27/09 TCU hawajatoa utaratibu wowote wa nini kifanyike kwa wale vijana wote ambao hawajapata udahili. Tangazo hili sidhani kama linawasaidia wanafunzi wanaotaka kuwahi kujiunga na vyuo kabla muhula mpya haujaanza mapema wiki ijayo. Hivii kwa kauli hii TCU wanawaambia nini wanafunzi wote waliojaza fomu kama private candidate kwa chuo kikuu cha Dar es Salaam ambao wamejaza hasa baada ya chuo kutangaza uwepo wa nafasi??? Je UDSM sasa wanatakiwa wasiendelee na udahili kwa wanafunzi hao hadi TCU itakapotoa utaratibu???

"THIS COUNTRY BWANA!!!!!!!!"
 

Eunda

Member
May 2, 2008
60
11
TCU hawana jipya. Walidai watatoa utaratibu tarehe 26th Sept na leo ni tarehe 28th Sept hakuna kiilichafanyika na ukizingatia vyuo kama UDSM orientation week kwa first year inaanza tarehe 01st Oct, na masomo yanaanza rasmi tarehe 10th Oct.
 

Bukijo

JF-Expert Member
Jul 28, 2010
208
71
Wadau hawa TCU mwaka huu naona wanajichanganya,make kuna kipindi walitangaza empty slots.
Siamini kama kweli Second selection ilijaza slots zote zile,na bado wale waliochaguliwa second selection uhakika wa kusoma haupo kwa kua HESLB haijesema lolote juu yao.
Sasa vyuo vingi vina lalamika kua havipata wanafunzi wa kutosha,baada ya kutangaza nafasi hizo TCU wanaingilia tena sijui niwaeleweje!

Mbaya zaidi kwa kua TCU sijui niseme wanaugonvi na NACTE wamaefanikiwa kuzuia Equivalent na Mature age applicants wasipate udahili vyuoni hasa vile vyuo ambavyo haviko chini ya NACTE.
Mfano: UDOM mwaka huu hawajachukua kabisa Equivalent na Mature Age ambao waliomba chuo wakitarajia Mkopo Toka HESLB waliopata tu ni wale ambao waliomba under Private sponsorship na wale toka TCU!
Jana nimefanikiwa kufika UDOM nikauliza juu ya swala hili kua Kwa nini mwaka huu hawajadahili Equivalent na Mature age?
Nikajibiwa kua udahili umeshakamilika majina yaliyopo kwenye website ndo hayohayo hawana mpango wa kudahili wengine labda kama TCU wataongeza wao.

Mbaya zaidi ukicheck majina ya watu waliodahiliwa UDOM ambao hawakupita A-level ni kama 53 tu.
Swali je ni kweli hao 53 ndo wenye sifa sitahiki kwa jumla ya idad ya wote walioomba kupitia Mature age na Equivalents?
Ukiangalia Empty slots: TCU Website , UDOM ni 1159.Je,second selection ni kweli wamechaguliwa 1159 kwenda UDOM?.
Ndugu zangu udahili wa mwaka huu ni vituko tu,mwenzenu nasubiria kipindi cha uchaguzi ndo ni apply make at least kuna fair,ubavu wa kudai haki sina nauli ya kwenda mjini sina na ofisi zipo mijini.Nalazimika kua mwalimu wa Pysics na Math na Diploma yangu ya Computer Engineering make no way out!
 

Didia

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
719
258
Sarakasi hizi zinaonesha tume hii haina uwezo wa kufanya kazi. Vyuo vinaipatia tume courses zinazotolewa na na mahitaji ya kila kozi (iddadi ya wanafunzi na cut-off points). Kama UDSM imebaki na nafasi si iwaache wadahili wenyewe. TCU walipewa takribani miezi mitano ya kufanya udahili lakini haijakidhi matakwa ya baadhi ya vyuo kwa nini ingang'anie?
 

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,720
1,435
hawa jamaa kama walikuwa hawajajipanga kwa nini wali centralize mambo ya udahili!? hawa jamaa wanatia hasira sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom