N
isaidie kwa hili bwana: Kijana wangu amepata physics B, chemistry B+ biology B+. akijaza UDM medicine inakataa kuwa point ni 5 zinazohitajika (system inasema yeye ana 4 wakati sio kweli). Vyuo vyote vingine vimekubali. anataka kujaza Muhimbili, CUHAS na Udom. Please help
Hayo matatizo yapo tangu 2012 nimeanza kuyaona. Japokuwa huwa kunakuwa na mistake kwenye website ya TCU-CAS ila ukiona vingne vinakubali na kimoja kinagoma usiendelee kubishana nao sana, tafta kingne. Lakin pia kuna wakati ambapo unakuta walioomba kile chuo wapo wengi sana na washajaa, ile setting system ikawa haikuwekwa kwaajili ya kuchange status kwahyo ikaleta status nyingine.
hizo deadlines ndivyo zilivyo,ila kwa ushauri ni kwamba hata hao wanaoapply kupitia TCU walitakiwa kuwa wamemaliza mambo yao tar 2/8 zaidi ya hapo unajiweka katika wakati mgumu. wabongo wengi husubiri mpaka siku ziishe ndio waanze kuapply sasa wameambiwa wamepele fomu ofisi za tcu wenyewe lakini ukweli ni kwamba kupeleka fomu mwenyewe ni kujikosesha nafasi mwenyewe, siku hizi mambo ni kwenye computer hakuna mtu huko wa kudeal na hardcopies
TCU mwisho haikuwa tar 2 ilikuwa ni tar 15/08/2015
Nacte na TCU ni taasisi mbili tofauti zilizo na mamlaka ya kudahili wanafunzi independently,Nacte inajihusisha na equivalent na TCU ni direct ,mbona hukuuliza kwanini Nacte walianza kupokea maombi kabla ya TCU kuanza?
Ni taasisi mbili tofauti lakini zinahusika na elimu ya juu. Nasema hivi kwa kuwa nimemaliza diploma mwaka huu na matokeo ndio yametoka. Kwa maana nyingine nimechelewa. Inabidi sasa kila taasisi iwe na guidebook yake
Nadhani njia rahisi ni kuwasiliana na huduma kwa wateja wa mtandao husika..Labda wanaweza kusaidia