TCRA: Yatoa neno kwa Vyombo vya Habari vinavyowatumia watangazaji wasio na Taaluma ya Habari

๐Ÿ˜๐Ÿ˜๐Ÿ˜
Kwani Kina Lokole na Baba Levo ndio Walioomba hiyo kazi ama UTAWALA uliamua?!!!

Isije ikawa vetting ya kupata faida zaidi imefanyika zaidi kuwa recruit halafu wewe unakalia HISIA..๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Sasa wasafi wasubiri kufutiwa leseni.
 
Nawaza Hapa.....

Hivi mtu anataka kuwe na MWANATAALUMA wa habari,kwenye kipindi Kama MASHAMSHAM Cha WASAFI FM?!!!

Huyo mwanataaluma atadeliver vyema ubora kwa wateja wao kama hao kina Dida,Babu Iddy na Ankali Mambi?!!!

Nikiwa Kama Msomi nilikuwa Sina mzuka kabisa wa kusikiliza vipindi Aina hiyo,ila ninavyozidi kukua kifikra huwa nikiwa OFF DUTY huwa ninawasikiliza vyema tu ili kuwafahamu maisha ya wenzetu wa uswazi lakini pia kutoa STRESS ZA MIHANGAIKO๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Nawaza Hapa.....

Hivi mtu anataka kuwe na MWANATAALUMA wa habari,kwenye kipindi Kama MASHAMSHAM Cha WASAFI FM?!!!

Huyo mwanataaluma atadeliver vyema ubora kwa wateja wao kama hao kina Dida,Babu Iddy na Ankali Mambi?!!!

Nikiwa Kama Msomi nilikuwa Sina mzuka kabisa wa kusikiliza vipindi Aina hiyo,ila ninavyozidi kukua kifikra huwa nikiwa OFF DUTY huwa ninawasikiliza vyema tu ili kuwafahamu maisha ya wenzetu wa uswazi lakini pia kutoa STRESS ZA MIHANGAIKO๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Basi walau wawe update na sheria na wajue nini inatakiwa iende hewani na ipi haitakiwi.
 
Aache fujo alete makaratasi
Ha ha ha Kwako Makaratasi Yana Umuhimu Sana kuliko INTELLECT eee?!!!
Mbona Kuna WASOMI kibao wanapata Makaratasi kwa mbeleko za kubebwa,kupendelewa,mahusiano TATA...halafu kichwani ni taburarasa Tofauti na GPA zenye mng'aro...๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Haya Mkuu Wangu.
 
Sina Mafungamano na Masudi Ally Kipanya na nikiwa Kama kijana Msomi siijui elimu yake ila toka ninakua mpaka Sasa nimekuwa nikimfuatilia KP na kumaizi kuwa ni mtu Mwenye akili,patriotic and visionary zaidi ya Sisi wengi tulio na Doctorates na Masters....

Nisamehe kwa kusema labda unamsigina haiba yake kwa Ad Hominem.
Huyu jamaa Ni jembe!
 
Kutabaki mtu kweli kwenye vyombo vyetu vya habari Tanzania?

Mtu mwenye uzoefu miaka 5 wa kufanya kazi chini ya mtu mwenye taaluma au chombo cha habari tajika pia wangeruhusiwa lakini siyo chini ya Cyprian Musiba wa Tanzanite TV.

Hii TCRA wakikazia kina Dida, Fumbuka n.k kweli watabaki mjengoni?

Au wafanye kipindi cha mpito wasiokuwa na vyeti wasome Kozi maalum ya wiki moja kuwawezesha wasio na vyeti isimamiwe na Media Council of Tanzania (MCT) au The School of Journalism and Mass Communication UDSM , SAUT n.k

Baada ya muda wa mpito tuseme miaka 5 toka sasa sheria hiyo ya TCRA itumike bila kupepesa macho.
Ilitolewa Miaka mitano kuanzia 2016 mpaka 2021 sasa Kama mtu anataka kuwa mtangazaji na hajasomea awaachie waliosomea.
Hata uijue Sheria vipi huwezi kusimama mahakamani Kama advocate mpaka uidhinishwe kuwa advocate.
Lakini naona taaluma zingine Kama uandishi wa habari kila mtu mradi anajua kuongea anakuamwandishi wa Habari.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA) YATOA ONYO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUAJIRI WATANGAZAJI WASIO NA TAALUMA.

Mamlaka ya Mawasiliano nchini imetoa onyo kwa vyombo vya habari hususani redio na televisheni kwa kile inachodai kuwa vyombo hivyo vimekua na tabia ya kuajiri watangazaji wasio na taaluma hiyo.

Katika tarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Septemba 14 imewataka wamiliki wa vyombo hivyo kuzingatia matakwa ya sheria na masharti ya leseni ya utangazaji kwa kuhakikisha kuwa wanaotangaza katika vyombo vyao wana vigezo vya kitaaluma kama waandishi wa habari.

Mamlaka hiyo imefafanua kuwa kwa mujibu wa sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 kifungu cha 19(1) kinaeleza kuwa kufanya kazi kama mwandishi wa habari pasipo kuthibitishwa kwa mujibu wa sheria ni kuvunja sheria na kwa mujibu wa kanuni ya 17(2) ya vyombo vya habari ya mwaka 2017 ili mtu athibitishwe kuwa mwandishi pamoja na mambo mengine anatakiwa kuwa na shahada au stashahada ya uandishi wa habari au inayohusiana na masuala ya vyombo vya habari kutoka chuo kinachotambulika kinachotoa elimu ya masuala hayo au shahada au stashahada ya masuala ya Vyombo vya Habari.

Kuwa na watangazaji wasio na elimu juu ya masuala ya habari na utangazaji kunapelekea kutendeka kwa makosa mengi ya kutozingatia miiko ya uandishi na utangazaji wa habari, hivyo kuwa kinyume na matakwa ya kifungu cha 7(2)(a)(iii) cha sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 kinachotaka vyombo vya habari kuzingatia misingi na miiko ya uandishi wa vyombo vya habari.

Aidha, Mamlaka imevikumbusha na kuvionya vyombo vya habari kuwa hatua zaidi zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kutoza faini, au kufuta leseni ya chombo chochote kitakachokiuka masharti ya leseni, kanuni na Sheria.

Ikumbukwe kuwa mamlaka hiyo ilitoa taarifa kuwa mpaka kufikia mwaka 2021 Vyombo vyote vya Habari vinatakiwa kuwa na waandishi na watangazaji waliokidhi vigezo vya kitaaluma.

Hivi kunatofauti kati ya "journalist" na "Presenter"..?
 
Ni jambo zuri kama serikali imefikia mahari na kuona umuhimu na kudhamini swala la profesionalism katika kazi basi ni sawa ,

Lakini na jaribu tu kufikiria kama kweli serikali ina maanisha hicho inachokisema ,mbona bado tunaendelea kuona madudud yale yale yakiwa yanataka kutokea upande mwingine ? .

Ukweli lazima usemweme , kama serikali imeona kufanya kazi ya utangazaji pasipo kuwa na taaluma ya utangazaji ni kosa kisheria , je kuajili wa watu ambao hawana taaluma ya ualimu wakawe waalimu tena bira ya wafunzo yoyote yatakayo wafanya waendane na fani ya ualimu , kisheri hii imekaaje ?..

Ushauri wangu kama tumeamua kuheshimu swala professionalism basi hili swala lisiishie huko tu kwenye utangazaji sheria hii ipite kote kwenye taasisi zote binafsi na taasisi za umma , na kama hilo haliwezekani basi tuache tu mambo yaende kama yalivyokuwa yanaenda lakini siyo huku kigezo hichi kinazingatiwa lakini kule kigezo hicho hicho hakizingatiwe huku ni kuharibiana kazi .
 
Hakuna tatizo hapo na vyombo vya habari vilishajipanga.
Mfano:
1. Clouds katika powerbreakfast mtangazaji ni Barbara ambaye naamini ni mwana taaluma. Halafu hawa wengine wanahudhuria kama waalikwa au wachangiaji. Ndio maana utaona yeye ndiyo hucontrol matukio ndani ya kipindi.
2. Wasafi vivyo hivyo wana Salma Dakota, Maulid, Sekioni ambao ni wana taaluma na wanacontrol vipindi husika. Wengine wanakuwa wachangiaji tu.
Yule Dr Isaack Mzee wa Njia Panda vipi? KASOMEA UANDUSHI AU UDOKTA?
 
Safi sana aisee nimekuwa nikiongea hili mara nyingi mno, watu hawataki kusoma mwishowe wanavamia kazi za watu, hili tatizo limekuwa kubwa nchini, tunaambiwa ajira hazipo lkn kiuhalisia zipo lkn wanaajiriwa watu wasio na ujuzi, ifike wakati tuache kuchekeana unakuta mtu kasoma ualimu lkn yupo benki kisa kuna ndugu yake benki husika.

Kuna kazi nyingi wanakaa watu wasio na sifa, mfano hata ubunge eti kigezo ni kujua kusoma na kuandika what a joke!!! Wakati tungeweza kuambiana ukweli kwamba inampasa mbunge awe na atleast degree, diwani atleast diploma vivyo hivyo wenyeviti wa serikali za mitaa.

Tunalalamika ajira hakuna wakati zipo, tunaharibu thamani ya elimu kwa kuendekeza siasa mwishowe hao hao wasio na elimu wanaanza kutukana elimu yetu je unadhani watoto watakuwa na hamu ya kusoma?

Tuache siasa tuweke uhalisia kwa kuzingatia professionalism, ifike kipindi kila idara kuwe na watu wenye taaluma ya kazi husika, ubabaishaji hautatufikisha popote.
 
Back
Top Bottom