TCRA: Yatoa neno kwa Vyombo vya Habari vinavyowatumia watangazaji wasio na Taaluma ya Habari

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,562
2,000
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA) YATOA ONYO KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUAJIRI WATANGAZAJI WASIO NA TAALUMA.

Mamlaka ya Mawasiliano nchini imetoa onyo kwa vyombo vya habari hususani redio na televisheni kwa kile inachodai kuwa vyombo hivyo vimekua na tabia ya kuajiri watangazaji wasio na taaluma hiyo.

Katika tarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Septemba 14 imewataka wamiliki wa vyombo hivyo kuzingatia matakwa ya sheria na masharti ya leseni ya utangazaji kwa kuhakikisha kuwa wanaotangaza katika vyombo vyao wana vigezo vya kitaaluma kama waandishi wa habari.

Mamlaka hiyo imefafanua kuwa kwa mujibu wa sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 kifungu cha 19(1) kinaeleza kuwa kufanya kazi kama mwandishi wa habari pasipo kuthibitishwa kwa mujibu wa sheria ni kuvunja sheria na kwa mujibu wa kanuni ya 17(2) ya vyombo vya habari ya mwaka 2017 ili mtu athibitishwe kuwa mwandishi pamoja na mambo mengine anatakiwa kuwa na shahada au stashahada ya uandishi wa habari au inayohusiana na masuala ya vyombo vya habari kutoka chuo kinachotambulika kinachotoa elimu ya masuala hayo au shahada au stashahada ya masuala ya Vyombo vya Habari.

Kuwa na watangazaji wasio na elimu juu ya masuala ya habari na utangazaji kunapelekea kutendeka kwa makosa mengi ya kutozingatia miiko ya uandishi na utangazaji wa habari, hivyo kuwa kinyume na matakwa ya kifungu cha 7(2)(a)(iii) cha sheria ya vyombo vya habari ya mwaka 2016 kinachotaka vyombo vya habari kuzingatia misingi na miiko ya uandishi wa vyombo vya habari.

Aidha, Mamlaka imevikumbusha na kuvionya vyombo vya habari kuwa hatua zaidi zitachukuliwa, ikiwa ni pamoja na kutoza faini, au kufuta leseni ya chombo chochote kitakachokiuka masharti ya leseni, kanuni na Sheria.

Ikumbukwe kuwa mamlaka hiyo ilitoa taarifa kuwa mpaka kufikia mwaka 2021 Vyombo vyote vya Habari vinatakiwa kuwa na waandishi na watangazaji waliokidhi vigezo vya kitaaluma.

efqwcdqef.jpg
 

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
6,886
2,000
Msumari ulishapigwa na kuzibwa pale juu usionekane, hawa TCRA ni kama wanaandaa mazingira ya kuutafuta msumari ili wauondoe.

Aliyekuwa mbunge wa Kyela H. Mwakyembe alisimamia hili kwa nguvu zote na kila media inafaham.

Hapa kila mwanahabari anaelewa elimu yake, vinginevyo ajichunge kwa ustawi wa chombo alichopo.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
10,774
2,000
Kutabaki mtu kweli kwenye vyombo vyetu vya habari Tanzania?

Mtu mwenye uzoefu miaka 5 wa kufanya kazi chini ya mtu mwenye taaluma au chombo cha habari tajika pia wangeruhusiwa lakini siyo chini ya Cyprian Musiba wa Tanzanite TV.

Hii TCRA wakikazia kina Dida, Fumbuka n.k kweli watabaki mjengoni?

Au wafanye kipindi cha mpito wasiokuwa na vyeti wasome Kozi maalum ya wiki moja kuwawezesha wasio na vyeti isimamiwe na Media Council of Tanzania (MCT) au The School of Journalism and Mass Communication UDSM , SAUT n.k

Baada ya muda wa mpito tuseme miaka 5 toka sasa sheria hiyo ya TCRA itumike bila kupepesa macho.
 

Percy

JF-Expert Member
Jul 21, 2014
5,939
2,000
Kutabaki mtu kweli kwenye vyombo vyetu vya habari Tanzania?

Mtu mwenye uzoefu miaka 5 wa kufanya kazi chini ya mtu mwenye taaluma au chombo cha habari tajika pia wangeruhusiwa lakini siyo chini ya Cyprian Musiba wa Tanzanite TV.

Hii TCRA wakikazia kina Dida, Fumbuka n.k kweli watabaki mjengoni?

Dida kasomea uandishi wa habari pale dsj.
 

Possibles

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
1,531
2,000
Hakuna tatizo hapo na vyombo vya habari vilishajipanga.
Mfano:
1. Clouds katika powerbreakfast mtangazaji ni Barbara ambaye naamini ni mwana taaluma. Halafu hawa wengine wanahudhuria kama waalikwa au wachangiaji. Ndio maana utaona yeye ndiyo hucontrol matukio ndani ya kipindi.
2. Wasafi vivyo hivyo wana Salma Dakota, Maulid, Sekioni ambao ni wana taaluma na wanacontrol vipindi husika. Wengine wanakuwa wachangiaji tu.
 

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
6,362
2,000
Hakuna tatizo hapo na vyombo vya habari vilishajipanga.
Mfano:
1. Clouds katika powerbreakfast mtangazaji ni Barbara ambaye naamini ni mwana taaluma. Halafu hawa wengine wanahudhuria kama waalikwa au wachangiaji. Ndio maana utaona yeye ndiyo hucontrol matukio ndani ya kipindi.
2. Wasafi vivyo hivyo wana Salma Dakota, Maulid, Sekioni ambao ni wana taaluma na wanacontrol vipindi husika. Wengine wanakuwa wachangiaji tu.
Kipanya darasa la saba B
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
3,177
2,000
Ni Jambo Zuri Lenye Afya...

Ila.....


Mtazamo Wangu Utabaki PALEPALE...

#Taifa Linahitaji Kuthamini Elimu Na Kuweka Mkazo Wa Ubora Kuanzia Shule Ya Msingi.

Je Watu Wetu Wa Mitaani Wanasikiliza Redio Zenye Waandishi Waliobobea Kwa Kuwa Na Vyeti Bora?!!!

Jibu ni:

Ukifuatilia huko Mitaani,utamaizi kuwa RADIO CLOUDS FM,WASAFI FM n.k zinasikilizwa mno na makundi yote(yasiyo na Elimu+yenye elimu,hususani VIJANA).

Je Makampuni Ya BIASHARA Hayapeleki Matangazo Yao katika hizo Redio Zisizo na Wanataaluma Wengi Wa Habari?!!!

Jibu ni:

Serikali Inaingiza Kodi Kubwa Kupitia FAIDA Wanazopata Makampuni yanayopeleka Matangazo Yao kupitia hizo redio na televisheni,mfano WASAFI TV,RADIO NA CLOUDS.

Hebu Fikiria..Kampuni inapelekaje matangazo yake ya BIDHAA zao kupitia Redio na Televisheni zisizoangaliwa na kusikilizwa kwa wingi na Walaji Wa Habari?!!!!

Hakika Tuna Dhima kubwa ya kuwajua vyema Watanzania walioko huko Mitaani....

Ni Lazima Tuongeze UBORA kwa elimu ya watoto kuanzia Shule za msingi,ili tuwe na TAIFA LILILO BORA ZAIDI VINGINEVYO ni kutwanga maji kwenye kinu.....


Jumbe Brown
Kijana Muuza Al Kasus.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom