TCRA: Wenye akaunti ‘feki’ kukiona

TCRA: Wenye akaunti ‘feki’ kukiona

Kwa hiyo hiki ndio kipaumbele cha hiyo mamlaka ya mawasiliano?

Sijui huko ofisini huwa wanafanya nini, baadala ya kuwaza mipango ya kuendeleza teknolojia wao wanawaza kutoa matamko kwamba watakiona, watakoma, utafikiri wamepewa mamlaka ya kuwakomesha wananchi tu.
 
Mmeshindwa tu kuyasimamia Makampuni ya simu kwenye usajili wa line tu, ije kwenye mitandao? Facebook wenyewe wameshindwa hayo Ndio maana kuna account fake, sasa tuambieni Sheria ya JF inaruhusu watu kutumia majina fake, nyinyi mmasema ni kosa kisheria, ina maana mnampango Jf ikate roho?
Siku mkianza kukamata fake account basi ndio itakuwa mwisho wangu kutumia mitandao
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji13]
 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo, anaandika Charles William.

James Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kilaba ameyasema hayo leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT).

“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” amesema Kilaba.

Kampeni hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao, itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama, “Darasa mtandao”.

“Miongoni mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni kutoweka wazi taarifa zao binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza neon la siri (password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na mengineyo mengi,” amesisitiza Kilaba.
Waende zao huko ndoooorobo tangu waliposhindwa kuzima simu zangu feki 3 siwez kuwaamini
1471452869898.jpg
 
Hakuna vigezo vyovyote vya kuweza kutambua hili ni jina feki au halisi.
Na huwezi kuzuia majina feki kweny mtandao.
Mfano.
Mm naitwa Masanja Thomas, je nikijisajili kwa jina la Josiah Allen utanikamata? Au utatambua kuwa sio jina langu halisi?
Hapo wamechemka, id feki zitakuwepo tu.
 
Sasa bila kujisajili kwa majina ya uongo ujasiri wa kuandika neno DIKTETA UCHWARA tungeutoa wapi?
 
Kwa iyo um JF tusubili hatua kali za kisheria
 
Mwl Nyerere alishawahi kusema 'Kiogozi mzuri ni yule ambae anae deal na mambo muhimu, Na mambo ya kijinga unaacha nayo'

Sasa naona viogozi wetu wanapambana na mambo ya kijinga yale yenye muhimu kwa wananchi wanayaacha!
 
Duuh,ule ujumbe wa...... "You're visiting this page as a visitor" ndio utakaotamba wakati huo.
 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano hapa Nchini (TCRA) imewaonya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanaojisajili katika mitandao hiyo kwa kutumia majina na taarifa za uongo, anaandika Charles William.

James Kilaba Kaimu Mkurugenzi wa TCRA amesema, vitendo vya watu kujisajili katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina na taarifa zisizo sahihi, ni kosa kisheria na kwamba wanaofanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kilaba ameyasema hayo leo, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao ambayo inasimamiwa na Kitengo cha dharura cha kuitikia matukio ya usalama kwenye mitandao hapa nchini (TZ-CERT).

“Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” amesema Kilaba.

Kampeni hiyo ya kuongeza ufahamu kuhusu matumizi sahihi na salama ya mitandao, itafanyika kupitia matangazo ya redio, televisheni, magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ambapo katika mitandao ya kijamii itajulikana kama, “Darasa mtandao”.

“Miongoni mwa mambo ambayo tutawafundisha wananchi ni kutoweka wazi taarifa zao binafsi zote katika mitandao, kubadili na kutunza neon la siri (password), kutojibu ujumbe unaosema umeshinda bahati nasibu na mengineyo mengi,” amesisitiza Kilaba.
.
Charles, ungechimba kidogo na kutuletea vifungu husika katika ile sheria husika. Pia ungemwuliza kidogo huyo jamaa kuhusu vitu kama vile pen names, etc. Otherwise, story yako haijakamilika. Ikamilishe plz...
 
TCRA wanazungumzia suala linalohusu eneo lao (Tanzania)

Wanazungumzia suala la awareness na mitandao, usalama wa watumiaji na athari za uhalifu wa mitandaoni.

Ila sidhani kama wanaweza kuanza kumtafuta mtu kama Lizaboni pale Songea and Co ambao tupo kila kona ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom