JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Kwa mujibu wa ripoti ya takwimu ya sekta ya Mawasiliano ya robo mwaka inayoishia Septemba 2025 inaonesha idadi ya utumiaji wa intaneti inatokana na laini/waya ambazo zimetumia huduma ya Intaneti angalau mara moja katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, bila kujali teknolojia iliyotumika (FTTX, 2G - GPRS na EDGE, 3G, 4G, au 5G).
Ripoti hiyo imefafanua kuwa huduma ya intaneti kwa njia ya simu ya mkononi inapendelewa zaidi (99%) ikilinganishwa na huduma ya intaneti isiyohashimishika.
Kuongezeka kwa utumiaji wa intaneti unatokana na ubora wa huduma na miundombinu inayowezesha upatikanaji wa mawasiliano kwa wananchi.
Tembelea tovuti ya TCRA (www.tcra.go.tz) kwenye kipengel cha Machapisho, kisha bofya Takwimu, au bofya kiunganishi https://bit.ly/48CADOW ili kusoma ripoti nzima ya Sekta ya Mawasiliano (Julai – Septemba 2025).