TCRA wanatumezesha sumu/ juu ya kutrace simu iliyo potea

TCRA wanatumezesha sumu/ juu ya kutrace simu iliyo potea

silver25

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2010
Posts
743
Reaction score
44
Wajameni Taarifa ya Uhakika
Msije mkapoteza simu mukadhani kuna kiinstitution kinaweza fanya Tracing Simu ikapatikana, Kwa Tanzania ni Propaganda tu na si kweli. hakuna TCRA wala Mtandao wa simu ambao unaweza kukupa support katika kufanikisha hili, limenitokea mimi na sasa nimepata majibu sahihi kabisa.

Kwa kifupi Jana nimepoteza simu yangu Nokia Lumia 520, niliinunua 1th December 2013, Saa nne asubuhi pale Mlimani city. Nimeitumia hata mwezi haujaisha Bahati mbaya Wezi na fani zao wakakwapua, nikawahi maramoja jana saa nne usiku kupiga kwenye mtandao ninao tumia Simu yangu ili kuliport juu ya kuibiwa na kuulizia Taratibu za kuitrace, jibu nililo pata (HUDUMA HIYO SISI HATUTOI LABDA UONGEE NA COMPANY ILIYO TENGENEZA SIMU WAFANYE HIYO)

Sikuchoka nikapiga simu moja kwa moja kwa NOKIA Dealer wa hapa Tanzania. nao wakaniambia hawana huduma ya kutrace. Nikasema ngoja nipige TCRA nipate haka kautaratibu Maana walisha tangaza sana kwenye Vyombo vya habari kuwa ukiwa na Cerial number ya simu ilio kuwa attached kwenye Receipt ama nyuma yaambako Batery ya simu inakaa basi mambo yamekaa sawa

Baada ya kupiga nikapewa jibu kuwa (Sidhani kama huduma hiyo inaweza kufunction Hapa Tanzania, sasa nikauliza inamaana kwenye TVs huwa munaongea uhongo "wanasema nilete ushahidi wa video ili waangalie kama wataweza nisaidia kutrace")

Nikaquit TCRA nikaamua kutembelea mwenyewe kwenye ofice za mtandao mmoja wa Simu hapa Tanzania unaoaminika kuwa na wateja wengi kuliko yote, na kupata consultations service, wao ndo wakanipa mbicho kavu kuwa Hao wanao ongea kwenye Vyombo vya habari si Wataalamu wa mambo ya Mitandao na Mawasiliano they are just Politicians) maanayake ni kitu ambacho kwa Tanzania Technolojia hii hatuna na huwezi pata kitu chochote kama umepotelewa na simu yako.

So TCRA kwanini munatumezesha sumu?
 
Hiyo ni 1. Number moja (tcra) ....nashukuru tumepata mfano halisi....
Namba mbili ni 2.(sumatra).......3.(ewura).........hivi ni visehemu vya kuuzia maneno na watu kujipatia riziki ambayo si halali........yaani wanavuna bila kupanda.........
 
makubwa, ya teknolojia inagubikwa sa propaganda za siasa. Tanzania bana!
 
safi sana mkuu kwa kufunguka na kutoboa, kweli WE DARE TO TALK OPENLY!
 
hahahahahahahaahaha hivi wewe unaamini watendaji walioteuliwa na mfumo wa ccm!!! haya muulize @j.makamba yumo humu nadhani
 
Mkuu, Ungekuwa unatumia OS ya Android ungeweza ku trace simu yako kwani kuna Applicationa kama " Where is my android" ungeweza kui trace ! Pole sanaa Mkuu!
 
Kwa hapa Tanzania
.
POLICE, TCRA, NSP wote ni vilaza tu yaani ukipotelewa na simu usijetegemea hawa jamaa watakupa msaada,
.
Unamwambia TCRA mimi nimepotelewa na LUMIA yeye hata kuishka tu hajawai, sina maana kwamba hawez kununua ila haja develop ktk teknolojia, siasa zimewaweka pale...
.
Juzi juz tu namsikiliza jamaa wa TCRA anawadanganya wananchi wa PWANI et hakuna anaeweza kusikiliza simu, za watu wananchi wasiwe na wasiwasi, nikasema huyu jamaa cjui anaish dunia gan huyu..
.
yaani saiz ni wewe mwenyewe tu ku fight ANDROID wanakula raha tu.. Kama wakiibiwa simu zao. Mtu una m track mwenyewe mwizi wako .. POLICE wenyewe ndo majanga tu..
 
Hakuna kaka Hawa jamaa hawako serious kabisa, Hivi Tanzania hakunaga sheria ya kuwa shitaki wat waliotoa Tamko la uongo kwenye vyombe vya habari na kuudanganya uma?
 
MKuu silver25 naona ulipotezwa toka mwanzo, ungekuwa well informed kwa hakika ilikuwa rahisi kuipata hiyo simu bila hata kwenda TCRA wala VODACOM, msaada ambao ungehitaji labda ni askari mmoja tu ambaye baada ya kazi ungempoza na buku ten ya usumbufu (na hiyo buku ten ingetoka kwa huyohuyo unayemkuta na simu)! Kuna apps zinazokusaidia kutrack siu yako wewe wenyewe, hata mtu akibadili line app inakupa taarifa na unaona mpaka location, inabaki kazi kwako kutumia akilii yako kichwani kupeleleza na kumpata!!
 
Last edited by a moderator:
January Makamba badala ya kuuwaza sana Urais ambao hawezi kuupata labda by Mwaka 2030 ni afadhali angetumia muda wake mwingi kuwasaidia hao jamaa zake wa TCRA kwenda na wakati
Kwani ingemgharimu bei gani kuhakikisha TCRA wanakuwa na Applications hata 6 za ku track simu tofauti tofauti na kuhakikisha makampuni ya simu yanalipa Tsh 10 kila simu inayopigwa kwa kutumia / kupitia kwa makampuni haya ya simu na Serikali ikapata mapato na bajeti isiwe tegemezi??
Sijui anawaza nini humu kichwani mwake?
 
MKuu silver25 naona ulipotezwa toka mwanzo, ungekuwa well informed kwa hakika ilikuwa rahisi kuipata hiyo simu bila hata kwenda TCRA wala VODACOM, msaada ambao ungehitaji labda ni askari mmoja tu ambaye baada ya kazi ungempoza na buku ten ya usumbufu (na hiyo buku ten ingetoka kwa huyohuyo unayemkuta na simu)! Kuna apps zinazokusaidia kutrack siu yako wewe wenyewe, hata mtu akibadili line app inakupa taarifa na unaona mpaka location, inabaki kazi kwako kutumia akilii yako kichwani kupeleleza na kumpata!!

Kaka hiyo app inaitwaje niinstall kwa hii niliyonayo sasa hivi maana nimenunua tena lumia 520, si unajua mambo ya offer
 
Nilishasema na nitarudia hapa tena, kama TCRA hawataacha siasa na kusimamia weledi Watumiaji wa huduma yao yaani Watanzania tutakwenda mbali sana. Tatizo siasa nyingi.

SUMATRA ndio usiseme, waulize watu wanaotumia daladala nje ya mji watakuhadithia.
 
Last edited by a moderator:
Hakuna kaka Hawa jamaa hawako serious kabisa, Hivi Tanzania hakunaga sheria ya kuwa shitaki wat waliotoa Tamko la uongo kwenye vyombe vya habari na kuudanganya uma?
si mtaalam wa sheria lakini bila shaka hii kitu ipo shida hawa wote ni majuha hivyo hata ukashitaki ni kupoteza muda,tz si unaijua vizuri mkuu full majanga
 
Nime-mforadia hii link Mr Innocent Mungy, msemaji wa TCRA, bila shaka atatolea ufafanuzi, jamaa anajitahidi, tusubiri kidogo
 
Okay i get you na nimeiona hiyo sehemu nimesha install
 
.......huyu jamaa ana watoto wawili, kila mke wake anapokaribia kujifungua huwa anampeleka U.S.A, watoto wote wawili wamezaliwa huko! Kwa sheria za U.S.A anaezaliwa ndani ya nchi yao ni raia wao! Sasa sijajua ana nia gani na nchii hii!
 
Wajameni Taarifa ya Uhakika
Msije mkapoteza simu mukadhani kuna kiinstitution kinaweza fanya Tracing Simu ikapatikana, Kwa Tanzania ni Propaganda tu na si kweli. hakuna TCRA wala Mtandao wa simu ambao unaweza kukupa support katika kufanikisha hili, limenitokea mimi na sasa nimepata majibu sahihi kabisa.

Kwa kifupi Jana nimepoteza simu yangu Nokia Lumia 520, niliinunua 1th December 2013, Saa nne asubuhi pale Mlimani city. Nimeitumia hata mwezi haujaisha Bahati mbaya Wezi na fani zao wakakwapua, nikawahi maramoja jana saa nne usiku kupiga kwenye mtandao ninao tumia Simu yangu ili kuliport juu ya kuibiwa na kuulizia Taratibu za kuitrace, jibu nililo pata (HUDUMA HIYO SISI HATUTOI LABDA UONGEE NA COMPANY ILIYO TENGENEZA SIMU WAFANYE HIYO)

Sikuchoka nikapiga simu moja kwa moja kwa NOKIA Dealer wa hapa Tanzania. nao wakaniambia hawana huduma ya kutrace. Nikasema ngoja nipige TCRA nipate haka kautaratibu Maana walisha tangaza sana kwenye Vyombo vya habari kuwa ukiwa na Cerial number ya simu ilio kuwa attached kwenye Receipt ama nyuma yaambako Batery ya simu inakaa basi mambo yamekaa sawa

Baada ya kupiga nikapewa jibu kuwa (Sidhani kama huduma hiyo inaweza kufunction Hapa Tanzania, sasa nikauliza inamaana kwenye TVs huwa munaongea uhongo "wanasema nilete ushahidi wa video ili waangalie kama wataweza nisaidia kutrace")

Nikaquit TCRA nikaamua kutembelea mwenyewe kwenye ofice za mtandao mmoja wa Simu hapa Tanzania unaoaminika kuwa na wateja wengi kuliko yote, na kupata consultations service, wao ndo wakanipa mbicho kavu kuwa Hao wanao ongea kwenye Vyombo vya habari si Wataalamu wa mambo ya Mitandao na Mawasiliano they are just Politicians) maanayake ni kitu ambacho kwa Tanzania Technolojia hii hatuna na huwezi pata kitu chochote kama umepotelewa na simu yako.

So TCRA kwanini munatumezesha sumu?

With windows phone kuna feature ya "find my phone", nilipoteza lumia 925 yangu na nikaipata kupitia huduma hii, lazima uienable hii huduma kwenye simu na uwe na data connection kwenye simu...

What it can do:
  • Ring your phone kukusaidia kujua ilipo kama ulidondosha
  • Itakuonyesha location ya simu
  • You can lock it
  • You can also erase kila kitu

Link to the service: https://www.windowsphone.com/en-us/my

Similar services are available for iOS and Android that many people forget to enable and use them
 
Mi niliibiwa simu yangu mbagara nikaipata tegeta hizi ant thief applications zina saidia sana.hadi polic walihisi mi mchawi kwani wao mambo haya hawajii kabisa.
 
Back
Top Bottom