Jicho la Tai
JF-Expert Member
- Oct 10, 2012
- 1,457
- 615
Wajameni Taarifa ya Uhakika
Msije mkapoteza simu mukadhani kuna kiinstitution kinaweza fanya Tracing Simu ikapatikana, Kwa Tanzania ni Propaganda tu na si kweli. hakuna TCRA wala Mtandao wa simu ambao unaweza kukupa support katika kufanikisha hili, limenitokea mimi na sasa nimepata majibu sahihi kabisa.
Kwa kifupi Jana nimepoteza simu yangu Nokia Lumia 520, niliinunua 1th December 2013, Saa nne asubuhi pale Mlimani city. Nimeitumia hata mwezi haujaisha Bahati mbaya Wezi na fani zao wakakwapua, nikawahi maramoja jana saa nne usiku kupiga kwenye mtandao ninao tumia Simu yangu ili kuliport juu ya kuibiwa na kuulizia Taratibu za kuitrace, jibu nililo pata (HUDUMA HIYO SISI HATUTOI LABDA UONGEE NA COMPANY ILIYO TENGENEZA SIMU WAFANYE HIYO)
Sikuchoka nikapiga simu moja kwa moja kwa NOKIA Dealer wa hapa Tanzania. nao wakaniambia hawana huduma ya kutrace. Nikasema ngoja nipige TCRA nipate haka kautaratibu Maana walisha tangaza sana kwenye Vyombo vya habari kuwa ukiwa na Cerial number ya simu ilio kuwa attached kwenye Receipt ama nyuma yaambako Batery ya simu inakaa basi mambo yamekaa sawa
Baada ya kupiga nikapewa jibu kuwa (Sidhani kama huduma hiyo inaweza kufunction Hapa Tanzania, sasa nikauliza inamaana kwenye TVs huwa munaongea uhongo "wanasema nilete ushahidi wa video ili waangalie kama wataweza nisaidia kutrace")
Nikaquit TCRA nikaamua kutembelea mwenyewe kwenye ofice za mtandao mmoja wa Simu hapa Tanzania unaoaminika kuwa na wateja wengi kuliko yote, na kupata consultations service, wao ndo wakanipa mbicho kavu kuwa Hao wanao ongea kwenye Vyombo vya habari si Wataalamu wa mambo ya Mitandao na Mawasiliano they are just Politicians) maanayake ni kitu ambacho kwa Tanzania Technolojia hii hatuna na huwezi pata kitu chochote kama umepotelewa na simu yako.
So TCRA kwanini munatumezesha sumu?
Ni uzembe ndio unaofanyika mkuu. Kwa sasa ukiweka simcard kwenye simu yeyote kule kwao itasoma sim card ile inatumia Handset yenye serial number fulani. Hivyo kujua kuwa handset yenye serial number fulani inatumika na line gani inakuwa ni rahisi lakini tatizo linakuja kwamba haiwezekani mtu wa voda kuitambua serial number ya mtu wa tigo au wa tigo kutambua wa voda (Yaani mitandao tofauti) Kuna kila sababu ya kuwa na institution ambayo itakuwa inashughulikia masuala haya. Kwani TCRA wamelala, na wenye mitandao wamelala.
Nimepata hili kama wazo jingine la kuongeza katika taasisi yangu ya Intelijensia.