TCRA/Wabunge: Kampuni za simu zinatuibia. Hamlioni hili?

M_kara

JF-Expert Member
Jan 9, 2016
385
293
Kama wewe ni mteja wa Vodacom siyo siri kwamba ukinunua kifurushi cha 'Cheka' unapata dakika za maongezi, mb za internet na idadi ya sms, say for 7 days. Kwa sababu ya ufinyu wa mb za internet kwenye vifurushi vya cheka, mara nyingi mb za internet zinakwisha kabla dakika za maongezi kumalizika.

hiyo unalazimika kununua kifurushi kipya cha mb za internet pekee ili ku-access internet service, say for another 7 days. Baadaye utakapo lazimika kununua kifurushi kipya cha cheka, sema cha siku 7, unachajiwa tena mb tofauti za internet, wakati zile mb za kifurushi cha internet bado ziko kwenye mzunguko.

Kwa maneno mengine, unakuwa umelipia mb za kifurushi cha cheka na mb za kifurushi cha internet kwa muda huo huo (same time frame, but double tariffs) na zote zinatumika concurrently. Sijui mitandao mingine wanafanyaje, lakini kwa mfano huo wa hapo juu hawa watu wana waibia wateja mchana kweupe.

Suluhisho: TCRA iwaagize kuwe na bundles za muda wa maongezi pekee bila kuchanganya na mb za internet.
 
TCRA hawasikii.....malalamiko ya simu ni mengi lakini wamenyamaza kimya.......
 
Ukweli ni kwamba TCRA ni kama wameshindwa kabisaaaa kuyabana makampuni ya simu hasa kwenye huduma za vifurush na huduma bora za mawasiliano,me nnavyokwambia naish Dar natumia simu yenye uwezo mzur wa internet ila hyo 3G kuipata shida na E ni kawaida sana kwangu while H au H+ ndo 3G yangu,wizi upo pia tigo.Waziri wao alishawaambia TCRA sijajua wamefikia wapi,ila naona wapo busy na vituo vya redio na TV simu wameziacha kabisa
 
Wizi mkubwa kama huu hawaufatilii,ila ule mdogo mdogo usiyo na tija serikali inaenda mpaka na waandishi wa habari ili wapige picha
 
3g ni ndogo kwa h+ so usiwashutumu bila jujua kasi ya 3g ni ndogo sana kwa h+
 
Malalamiko yangu:

Mitandao ya simu wanatuuzia bidhaa ambazo hatuzitumii... Inapaswa kuwa na kifurushi cha muda wa maongezi pekee, MB pekee na SMS pekee..


Tupate Uhuru wa kuchagua, Nataka SMS pekee unanizia na MB, Nataka Muda wa Maongezi unaniuzia na MB+SMS.


Huu ni ubakaji wa demokarasia.
 
By the way, kwa uharamia ulivyo kithiri kwenye maeneo ya IT, najiuliza TRA wanadhibiti vipi kodi za haya malipo yanayo pitia mitandaoni moja kwa moja kwa ukusanyaji kodi!! Naamini hizo electronic receipt za makapuni ya simu hazina link na machine za TRA kama zile za wanazotumia madukani. Naashiria kuamini ni rahisi ku temper nazo na kupelekea ukwepaji mkubwa wa kodi. Just thinking.
 
Ukweli ni kwamba TCRA ni kama wameshindwa kabisaaaa kuyabana makampuni ya simu hasa kwenye huduma za vifurush na huduma bora za mawasiliano,me nnavyokwambia naish Dar natumia simu yenye uwezo mzur wa internet ila hyo 3G kuipata shida na E ni kawaida sana kwangu while H au H+ ndo 3G yangu,wizi upo pia tigo.Waziri wao alishawaambia TCRA sijajua wamefikia wapi,ila naona wapo busy na vituo vya redio na TV simu wameziacha kabisa
Mkuu km simu yako ina uwezo wa 3G na upo dar lkn hupati kasi ya internet ya 3G,tatizo lako litakuwa kwenye simu yako mkuu. Karibu kampuni zote za simu zimefunga 3G eneo lote la jiji la dar. Me nakushauri utembelee duka la kampuni ya simu unayotumia watakusaidia kukuwekea mpangilio wa kupata hiyo 3G bila shida.
 
Sio Vodacom tu makampuni yote ya simu wanaiba hadi airtime wanazotuuzia, bundles. Etc uhuni mtupu
 
MiniKabang ya Tigo miezi michache iliyopita sh. 4000 ulikuwa unapata dk 91 na MB sijui ngapi. Wiki chache zilizopita wakafanya the same amount of money unapata dk. 80. Juzi nimenunua, the same amount unapata dk. 70. Nahisi muda sio mrefu the same amount itakuwa dk. 10; yetu macho.
 
Haya makampuni makubwa ya simu hufanya ka Collabo flan na mamlaka kama TCRA kuna tu benefits wakubwa wanapatiwa,favours,misaada ya kitaalam,wanasaidiwa wanapokwama kwenye IT n.k. Soni ngumu mbwa unayemlisha akung'ate labda uwe umelikoroga kwelikweli.
 
Siku zote nasema aliyotoa wazo la kupewa Mb 8 ukijiunga kifurushi cha kupiga akili yake ilikuwa na funza...maana ukishajiunga tu kisha ukawasha data Mb 8 zilishapotea yaani kitendo cha kuwasha tu data mb 8 zinaisha....ni vema wakaondoa kabisa na kutuwekea vifurushi kama cha kupiga ununue cha kupiga tu na kama cha Sms ununue cha Sms tu na kama Bundle ununue bandle tu...

Alafu pia hii la Vifurushi kuwa na limit huu pia ni wizi wangesubiri mtu atumie kifurushi hadi kiishe.

Asilimia 80 ya Vifurushi tunavyojiunga vinarudi kwao bila ya kutumika.
 
Kwani yule Waziri wa kufanya usafi kila mwisho wa mwezi siku ya jumamosi si dadake anafanya kazi huko?haya makampuni kuyadhibiti ni kazi sana kwasababu tayari wana lobbyists mpaka serikalini!
 
TCRA hawathubutu kuyabana haya mashirika makubwa ya simu, wizi muda wa maongezi wa wateja ni jambo ambalo umma umelilamikia kwa muda mrefu lakini TCRA hawachukui hatua zozote!
Mimi nadhani mabosi wa TCRA wachunguzwe ni lazima wanashirikiana na hawa watu kufanya ufisadi wa kutisha
 
Hata kwenye muda wa maongezi, badala ya dakika kuwa na sekunde 60 utakuta dakika zao zinaishia sekunde ya 38 tu.
 
Ukweli ni kwamba TCRA ni kama wameshindwa kabisaaaa kuyabana makampuni ya simu hasa kwenye huduma za vifurush na huduma bora za mawasiliano,me nnavyokwambia naish Dar natumia simu yenye uwezo mzur wa internet ila hyo 3G kuipata shida na E ni kawaida sana kwangu while H au H+ ndo 3G yangu,wizi upo pia tigo.Waziri wao alishawaambia TCRA sijajua wamefikia wapi,ila naona wapo busy na vituo vya redio na TV simu wameziacha kabisa
Asilimia kumi labda inafanyakazi TCRA
 
Kama wewe ni mteja wa Vodacom siyo siri kwamba ukinunua kifurushi cha 'Cheka' unapata dakika za maongezi, mb za internet na idadi ya sms, say for 7 days. Kwa sababu ya ufinyu wa mb za internet kwenye vifurushi vya cheka, mara nyingi mb za internet zinakwisha kabla dakika za maongezi kumalizika. Kwa hiyo unalazimika kununua kifurushi kipya cha mb za internet pekee ili ku-access internet service, say for another 7 days. Baadaye utakapo lazimika kununua kifurushi kipya cha cheka, sema cha siku 7, unachajiwa tena mb tofauti za internet, wakati zile mb za kifurushi cha internet bado ziko kwenye mzunguko. Kwa maneno mengine, unakuwa umelipia mb za kifurushi cha cheka na mb za kifurushi cha internet kwa muda huo huo (same time frame, but double tariffs) na zote zinatumika concurrently. Sijui mitandao mingine wanafanyaje, lakini kwa mfano huo wa hapo juu hawa watu wana waibia wateja mchana kweupe. Suluhisho: TCRA iwaagize kuwe na bundles za muda wa maongezi pekee bila kuchanganya na mb za internet.
VODACOM NI JANGA!!, Awali kampuni hii ili hudumu kwa uadilifu mkubwa tofauti na kampuni nyingine nyingine zilizo kubuhu kwa wizi,sasa hivi Vodacom ndio masterling ni kama wamezinduka wana kula bila kunawa, rogwa uweke kifurushi cha internet cha mwezi 25,000/-uone wanavyo toa huduma ya kasi yao ni kukufilisi wiki haiishi huna kitu,TCRA wana ya elewa sana haya ila sijui wanafaidikaje na hali hii kiasi cha kupuuza vilio vya wananchi.
 
Back
Top Bottom