TCRA, Tunaomba ufafanuzi

Dstv naona local channel moja tu yaani TBC, zingine sioni na wala sijawahi ona hata siku moja, please anayejua namna ya kufanya hata nione Star TV tu. Msaada please

Mkuu DSTV bana haipo kwenye michakato ya TCRA, utaishia kuiona TBC tu
 
me mbona nina cha startimes na local chaneli zote tano nazipata though bado nasubiri vingine nihame.elfu kumi na nane then chaneli zenyewe za kizushi tu.kwa anayetumia zuku anaweza tupa data zake?

Elfu kumi na nane za nini? tumeambiwa local channels zitakuwa za bure.....upuuzi mtupu! najiandaa kuandamana peke yangu, wanatangaza kuwa king'amuzi kinauzwa 39,000/= ukifika pale unaambiwa ni sh. 62,000/= nimeenda kufunga kimegoma wameniambia ninunue antena yao!!!????
 
Mkuu DSTV bana haipo kwenye michakato ya TCRA, utaishia kuiona TBC tu

Kwa sheria, walitakiwa waoneshe local channels zote - free. DSVT ni scandal mwanzo mwisho.

Na hii switch-over imeenda vibaya sana, na naona ni failure ya Wizara na TCRA kutofanya maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha local channels zinapatikana.
 
Kwa sheria, walitakiwa waoneshe local channels zote - free. DSVT ni scandal mwanzo mwisho.

Na hii switch-over imeenda vibaya sana, na naona ni failure ya Wizara na TCRA kutofanya maandalizi ya kutosha ili kuhakikisha local channels zinapatikana.

Ofkoz nakubaliana na wewe kuhusu DSTV walitakiwa kuingia kwenye mipango ya TCRA. lakini hili neno free nalo ni tata.
lakini pia unaposema hii ni failure ya wizara na TCRA inabidi utoe ufafanuzi kuntu mkuu FJM
 
Reactions: FJM
Awali tulielezwa kuwa tv zitakazoathirika kwa kutokuonyesha ni zile za analogy ambazo ndiyo zitahitaji visimbuzi! Sasa inaonekana kila mtu amekuwa affected na inafanywa bihashara. Hivi nchi zingine waliotutangulia nazo unahjitaji visimbuzi kuona channel ambazo si za kulipiwa? zaidi kwa nini mtu ununue visimbuzi vinavyoonyesha vituo vya ajabu usivyotaka kuangalia ilimradi tu upate TBC na Channel ten?
 
kwani ni lazima sana muangalie TV? Hamna shughuli zingine za kufanya?

umetoka baaa sio mda mrefu wewe,sio kosa lako,hata humu jamvini sio mahali panapokufaa.HABARI,MATANGAZO, NA BURUDANI UTAZIPATA WAPI?
 
Natumia Startimes; nipo mby city; naona local channel zote 5; ITV, STARTV, EATV, TBC & CHANNEL 10. Ila nitahama vikija ving'amuzi ambayo package zake zina ridhisha, coz ktk startimes kifurushi cha bei rahisi (9,000) channel za ziada nyingi hazina mvuto sana!
 
Siyo viwili ila tegemea sebule nzima, am tired!Hivi hawa jamaa TCRA si wao ndo wangeuza hivyo ving'amuzi na sisi tukawafuatehao jamaa wengine ili tulipie hizo chanel zingine za movie?Yaani ni usumufu kweli
Kwa mwendo huu wa hawa TCRA tutajikuta tuna ving'amuzi zaidi ya viwili kupata local Channels..... Gharama zaidi kwa mwananchi....
 

Itv na eatv zina sauti?
 
Siyo viwili ila tegemea sebule nzima, am tired!Hivi hawa jamaa TCRA si wao ndo wangeuza hivyo ving'amuzi na sisi tukawafuatehao jamaa wengine ili tulipie hizo chanel zingine za movie?Yaani ni usumufu kweli

acha uvivu. inaonyesha hukuwa unafuatilia matangazo ya tcra. changamoto zipo lakini baadhi yetu hatupendi mabadiliko.
 
Mkuu uko nchi gani wewe?, yaani matangazo yote yale yaliyotolewa na TCRA wewe bado hujaelewa!.
King'amuzi ni kimoja tuu utaona TV zote tano za "free to air" bure!.

Mpaka sasa kuna makampuni matatu ya kurusha matangazo, Star Media, Agape Associets "ting" na kampuni ya Mengi na Dialo ambayo king'amuzi chao bado hakijaingia sokoni, ila kimeanza kutangazwa!.

Ukishanunua king'amuzi chochote, hizo TV tano za bure utaziona bila kulazimika kuzilipia na zitaonekana kwenye ving'amuzi vyote vitatu, hivyo uko huru kuchagua kununua kingamuzi chochote kati ya hivyo!.

Mfano kingamuzi cha Star media hawana chanel ya movie ya HBO, kama wewe ni mpenzi wa HBO, huna jinsi, lazima ununue king'amuzi cha Agape!. Huko pia utaziona bute zile tv tano za bure!.

By choice, kama unataka usipitwe kitu, na unapenda mambo mazuri yote, then utavinu nua ving'amuzi vyote vitatu?.

Mimi nilianza na kingamuzi cha Easy TV, nikaja cha DSTV, Sasa ninacho cha Star Media, my boys wanapenda movies za HBO hivyo soon nitanunua cha Agape!.

Wengi wa Wakazi wa Dar, tunapenda zaidi starehe kuliko kuzijali familia zetu!, mimi nakunywa Sinza, kuna bar 250 na zote zinajaa, kwa nini tushindwa kulipia king'amuzi elfu 10 kwa mwezi?!.
Heri ya Mwaka Mpya.
Pasco.
 

Kwa kuongezea tu,sio kwamba clouds wameshindwa kukubalina na star times bali star times walikuwa wanarusha matangazo ya clouds kwa mfumo wa analogia

Zuku wanalocal channesls 3 channel ten,tbc1 na clouds tv,bwana mengi kakataa kurusha matangazo yake kupitia zuku kwa sababu ambazo nasikia ni zaidi ya sababu za kibiashara japo kuna taarifa kwamba na yeye king'amuzi chake pamoja na bakresa viko kwenye pipeline kuingia sokoni.
 

Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi,vipi kuhusu Dstv wataonyesha hizi 5 local channels?
 
Mkuu nashukuru kwa ufafanuzi,vipi kuhusu Dstv wataonyesha hizi 5 local channels?
Mkuu Namungula Jr, DSTV ni foreign channel, iko Africa ya Kusini, hii itaonyesha TBC tuu, tena hiyo TBC iliingia enzi za Tido, sijui kama itadumu!. Hizo TV tano za bure zinaweza kujiunga na DSTV ila kiukweli, kama kujiunga Star media ni issue, DSTV itakuwa ndio kabisa hawawezi kuigusa!.

Kwa mujibu wa matangazo ya ITV, king'amuzi chao kitakuwa kama cha DSTV, ni cha Digital signal, na picha ni za HD, hiki kingamuzi cha Star Media, kinapokea matangazo ya analojia na kuyarisha yakiwa hivyo hivyo analojia ila katika mfumo wa digitali.

Heri ya Mwaka Mpya!
Pasco
 
bongo mna kazi kweri kweri kudadadadeki kwa hiyo jana wengi wenu bila bila tv bwahahahaaha
 
itv na star tv unazipata?

binafsi naipata star tv kupitia king'amuzi cha startimes. Itv sijaiona, pengine pia ipo! Kwa mtizamo wangu swala hili limekaa kibiashara zaidi kuliko kuboresha huduma kama ambavyo tcra wamekuwa wakihutubia. Walisema katika mfumo wa digitali huhitaji kuzungusha zungusha antenna ili uone picha nzuri lakini kwa upande wangu bado nahitaji kuzungusha-zungusha antenna ili kupata vizur baadhi ya channels. Moreover, quality ya picha bado iko kama ilivyokuwa zamani. Kwa kifupi so far bado sijaona tofauti ya hii change (analogy-digital) zaidi ya usumbufu!
 

Du misamiati imekuwa mingi, hizo red red nayo ndiyo mdudu gani? Mnatuchanginyi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…