TBS kwenye kashfa nzito makampuni hewa nje ya nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TBS kwenye kashfa nzito makampuni hewa nje ya nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by YEYE, Jan 27, 2012.

 1. YEYE

  YEYE JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kamati ya BUNGE ya ukaguzi wa fedha za serikali ikiwa na kamati ya hesabu ya mashira ya uma ilienda
  kukagua kazi wanavyofanya TBS huko Hongkong na
  kugundua hawana ofisi, pesa wanaweka mifukoni.
  Source: TBC1
  "Hii ndo Tanzania uijuavyo"
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG] [​IMG]

  Deo Filikunjombe , Makamu Mwenyekiti (POAC) Mkurugenzi Mkuu (TBS), Charles Ekelege

  Madudu ndani ya mashirika ya umma yamezidi kuibuka ambapo jana Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (POC), ilibaini kuwa Shirika la Viwango nchini (TBS), limedanganya taifa kwa kutumia makampuni hewa ya kukagua magari nje nchi.Utapeli huo ulibainika baada ya timu ya wabunge kufanya ziara katika nchi za Singapore, China na Japan kwa ajili ya kutembelea makampuni yanayoelezwa na TBS kwamba yanahusika na ukaguzi wa magari kabla ya hayajaingia hapa nchini. Hata hivyo, wabunge hao walijionea vituko baada ya kufika huko nje ya nchi ambapo walibaini hapakuwa na kampuni wala ofisi yoyote inayofanya kazi hiyo ya ukaguzi wa magari.

  Mmoja wa wabunge hao, Deo Filikunjombe, alisema jana kuwa baada ya kufika walipata aibu mpaka wakafikia hatua ya kukimbilia ofisi za Ubalozi wa Tanzania zilizopo katika nchi hizo kwa ajili ya kujihifadhi. "Huko nje, hakuna ofisi, makampuni wala ofisi ambazo zimekuwa zikidaiwa na TBS zipo huko kwa ajili ya kukagua magari kabla hayajaingia nchini ili kujua ubora wake," alisema Filkunjombe.

  Kutokana na utapeli huo kuwa mkubwa, Kamati imemuandikia barua Spika wa Bunge, Anne Makinda, kutaka suala hilo litinge bungeni likajadiliwe na wabunge wote. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa POC, John Cheyo, alisema licha ya wabunge kukosa ofisi za makampuni hayo huko nje ya nchi, lakini pia hakuna mchanganuo wa fedha zilizopatikana kutokana na ukaguzi huo wa magari nje ya nchi.

  Alisema TBS kwa miaka 10 mfululizo imekuwa ikifanya vibaya katika mahesabu yake na kueleza kuwa hakuna shirika bovu la serikali kama hilo hapa nchini.

  Imedaiwa kuwa baadhi ya wabunge waliokwenda nje ya nchi kuangalia makampuni hayo walitaka kumpiga ngumi, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Charles Ekelege, ambaye aliwaongoza baada ya kubaini kwamba walikuwa wanatapeliwa. Kamati za Bunge za Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na ile ya Hesabu za Serikali (POC), jana zilisema ukaguzi wa magari unaingiza fedha nyingi lakini TBS imeshindwa kueleza mahali zilipo wala mchanganuo wake.

  "Huko nje ya nchi hatukukuta ofisi wala wakala wa ukaguzi wa magari baada ya kufanya ziara nje ya nchi," alisisitiza Makamu Mwenyekiti wa POAC, Filikunjombe. Wabunge hao ambao ni wajumbe wa Kamati hizo, walisema kutokana na utendaji mbovu wa TBS, kwa sasa haijulikani magari mangapi yanayokaguliwa ubora wake kabla ya kuingia nchini na ukaguzi huo unaingiza kiasi gani cha fedha. Kutokana na utata huo, kamati hizo zimeitaka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na TBS wiki ijayo kufika mjini Dodoma ili kutoa maelezo ya kina.
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hawa wabunge nao wamezidi sasa taarifa ya ugunduzi umetoka kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali wao wanasema wamegundua
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ahaaa, hao ndio wanaolipwa badala ya madactari.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ngoja nipate supu, halafu nitarudi hapa. TBS ni kero kero kerooooo.... kero.
   
 6. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Mwisho wa haya madudu kwa taifa letu ni lini?
  Mkombozi wa watanzania hajazaliwa?
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali huishia kwenye makaratasi na hajui hayo makampuni hewa ila anachojua kilichoandikwa vitabuni kwamba kuna makampuni yanayofanya kazi na hawa TBS. Wabunge ni wachokonoaji, hawaridhishwi na maneno ila hufanya utafiti na kufanya uhakiki hapo ndipo utokeapo mwanguko wa mende, ni kikwete na serikali yao ya kulindana atakayeshika kijiti kumpindua mende anayegaagaa miguu juu vinginevyo hainuki.
   
 8. Y

  Yetuwote Senior Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shirika la viwango!
   
 9. N

  Njele JF-Expert Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Yaani jitihada zote hizo zinazofanywa na waheshimiwa wabunge kuthibiti matumizi mabovu ya pesa za walipa kodi hawa watumishi wa umma ndio wanaspeed up? Inatisha@
   
 10. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Huyo mkurugenzi alipohojiwa na waandishi wa habari jana TBC1 alogoma kutoa majibu hadi jumatatu. Swali la msingi mpaka yote haya yanafanyika miaka kwa miaka watu wa TISS wako wapi jamani. Bila ya shaka hii ni dili ya mafisadi. Kweli watanzania ni watu wajinga sana duniani na kwa mtindo huu katu hatutapata heshima duniani zaidi ya ujinga.
   
 11. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Mh....jitihada kama zipo basi zinafanywa na wabunge wachache wa CCM na majority wa CHADEMA
   
 12. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  yawezekana hapo kwenye blue panajibiwa na hapo k wenye red!??
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  TAKUKURU kazi na wajibu wao tunaweza kuilinganisha na shirika maarufu la Marekani la FBI, shirika la uchunguzi, sasa hawa wanafanya nini hadi yote haya yanaendelea miaka nenda rudi kama kwamba hatuna chombo kinachofanya kazi hiyo? Tunaweza pia kupeleka lawama kwa shirika la usalama wa taifa, lakini tujue kwamba shirila la Usalama wa taifa haliwezi kufanya kazi kwa uwazi na hata kufungua mashtaka kwa vile hufanya kazi zake kwa usiri kadiri ya hulka ya mashari magumu ya kazi zao. Hawa TAKUKURU walitakiwa wafanye kazi zao na hawa wa usalama wa taifa hapo mambo mengi wanayoyajua usalama wa taifa yangetekelezeka na hawa TAKUKURU. Lakini wote wamebaki ni walaji tu na kujitanua kinamna kuwa na ubia wa makampuni hewa kuzidi kuumusha mifuko yao binafsi badala ya kulinda ile common pool tunayochota wote.
   
 14. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  TBC1 wanafanya nini kama si kujivika kilemba cha ukoka?
   
 15. muonamambo

  muonamambo JF-Expert Member

  #15
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  ngoja nikapate konyagi kwanza .... stahili hii inaweza kukulazimisha kusema vibaya na ukaishia gerezani.... kwa ufupi tu hao watu wa TBS BADO WANAISHI DUNIANI AMA WAMESHANYONGWA? Nadhani mbinu ya wachina inahitajika .... unalidanganya taifa unakatwa shingo.... akili itarudi.... naona nazidi kufunguka tu ngoja nirambe konyagi....
   
 16. B

  Biro JF-Expert Member

  #16
  Jan 28, 2012
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 331
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  kwani hao wakuu wa mashirika ya umma hawafanyiwa performance appraisal? kumbe ubebari una faida nyingi!
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  TBS sio kero, bali watendaji wake na serikali kwa ujumla kusindwa kusimamia kazi zake... hebu imagine inachukua 10 years kugundua kwamba tunapigwa changa

  halafu mbunge anasema wamegundua wao kumbe ni mfumo wa ukaguzi, wao walienda kuthibitisha tu:rant:
   
 18. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #18
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rostam na lowassa wanahusika
   
 19. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #19
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Hili shirika kama sikosei limewahi kupata certification ya ISO, hata kama hawajawahi kupata hiyo naamini kujitapa kwao kuwa "ndio wathibiti na wasimamizi wa ubora wa bidhaa" ni bure kabisa.

  Yaani kila gari liagizwalo toka nje "hulipiwa ada ya ukaguzi unaofanywa na tbs/wakala wake huko nje" HALAFU HAKUNA UKAGUZI. Hii ni skendali nyingine nzito.

  Ukitaka kujua "tbs ni legelege", angalia kuanzia magari yenyewe, matairi na bidhaa za mashine, mitambo na matumizi ya nyumbani zilivyo legelege.
  Haihitaji Phd ili ujue "hakuna udhibiti na usimamizi wa viwango Tz".

  Bidhaa zote bora zinazotengenezwa nchini na zile zinazoagizwa nje HUJA KWASABABU YA WAAGIZAJI WENYEWE NA SI TBS. Na hizo mbovu huja kwa sababu ya waagizaji na tbs.

  Tbs imezidiwa, inatakiwa ipanguliwe na iundwe upya.
   
 20. magessa78

  magessa78 JF-Expert Member

  #20
  Jan 28, 2012
  Joined: Sep 28, 2009
  Messages: 271
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Rostam na lowassa wanahusika
   
Loading...