Serikali yapigwa na kashfa ya Ghost Workers ya Sh6 Billion kwenye Payroll

Serikali yapigwa na kashfa ya Ghost Workers ya Sh6 Billion kwenye Payroll

OwadeKuya

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2026
Posts
452
Reaction score
273
Mamilioni ya walipa kodi wa Kenya huenda wamekuwa wakigharamia mishahara ya wafanyakazi hewa baada ya audit report kufichua dosari kubwa katika mfumo wa serikali wa malipo, HRIS-K.

Ripoti hiyo ilibaini kuwa karibu Sh5.9 billion zililipwa kupitia irregular earnings, huku maelfu ya records zikiwa na makosa ya ajabu. Baadhi ya wafanyakazi walionekana kuwa wamepelekwa kazini kabla hata ya kuajiriwa, while others had birth years listed between 2046 and 2049, jambo lililoibua maswali makubwa kuhusu integrity ya data serikalini.

Audit pia iligundua kuwa zaidi ya 5,700 employees walikuwa na taarifa zisizoeleweka, huku baadhi ya records zikionyesha KRA PINs batili, IDs zinazofanana, na bank accounts zinazoshirikiwa na watu tofauti.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba zaidi ya 4.7 million payroll records zilihaririwa bila timestamps, na wafanyakazi 77 walionekana kubadilisha taarifa zao wenyewe kwenye mfumo. Experts wanasema hali hii imeacha payroll ya serikali ikiwa vulnerable kwa fraud, misuse of public funds na cyber security threats.

Public Service PS Jane Imbunya amesema serikali imeanza hatua za kurekebisha mfumo huo kupitia forensic review, system upgrades na ushirikiano na National Intelligence Service (NIS) ili kufunga mianya iliyobainika.

Hata hivyo, changamoto mpya imejitokeza baada ya Bunge kuondoa fedha za Sh138 million zilizokuwa zimetengwa kuboresha HRIS-K, hatua ambayo inaweza kuchelewesha mageuzi yanayolenga kuondoa ghost workers na kurejesha uwazi katika matumizi ya fedha za umma.

Sasa Wakenya wanasubiri kuona ikiwa uchunguzi huu utawajibisha waliohusika au kama ripoti hii itaongezwa kwenye orodha ya scandals ambazo huishia bila hatua madhubuti.

Source: Nairobi Wire
 
Back
Top Bottom