TBS hizi nguo za kichina mnaziona?

TBS hizi nguo za kichina mnaziona?

Masulupwete

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
2,366
Reaction score
2,435
Unanunua dukani nguo nzuri kwelikweli inang'aa machoni.

Lakini cha ajabu ukiifua mara moja au mbili tu haitazamiki tena ni kama ulikuwa unanyang'anyana na ngombe.

Wataalam wetu TBS Pale bandarii huwa mnakagua nini?

Haya manguo hamyaoni au hamhusiki na ukaguzi wake?

Mtusaidie tunaibiwa.
 
Aiseee umeleta mada nzuri sn. Mimi kusema ukweli sipendi kuvaa nguo za mtumba. Lakini kila nikijaribu kununua hizi nguo za dukani hasa mashati na baadhi ya majinzi cha moto huwa nakipata. Nikifua nguo kwishaa habari yake. Inatoa rangi za kufa mtu aaafu inakunjamana hata uinyoooshe vp hainyoosheki.Aafu zinauzwa bei kubwa sn ubora sifuri.TBS kazi yenu ni nini?
 
Kwanini ununue nguo mtaa wa congo?
 
Unanunua dukani nguo nzuri kwelikweli inang'aa machoni.
Lakini cha ajabu ukiifua mara moja au mbili tu haitazamiki tena ni kama ulikuwa unanyang'anyana na ngombe.
Wataalam wetu TBS Pale bandarii huwa mnakagua nini?
Haya manguo hamyaoni au hamhusiki na ukaguzi wake?
Mtusaidie tunaibiwa.
TBS hii haikagui ubora inakagua muonekano yaani kama ni shati liwe na sehemu ya kuingiza mikono na kichwa. Nakushauri ukinunua vaa tu bila kufua au fua kwa petroli itabaki na ubora wake.
 
Tbs ni shirika la hovyo sana vitu vingi sana vinavyouzwa hapa nchini havina ubora lakini tbs wapo na wanalipwa mishahara kila mwezi
Kuanzia nguo, redio, tv, viatu, mpaka dawa za meno tena hizi wanauza mpaka kwenye mabasi ya mkoani
 
Nguo au kiatu vya kichina unanunua kwa shilingi elfu Moja Mia tano unataka vidumu muda gani?
 
Kwanini ununue nguo mtaa wa congo?

Nimenunua nguo Msasani mall pale.Hakuna lolote,nguo zinapauka balaa.Ninashukuru sasa tatizo limekuwa kubwa, watu tulioathirika tunakuwa wengi huenda tukasisika.

Mimi nilishalalamika kwenye page ya Fb ya duka husika,lakini hawakujibu chochote.Nimeamua kukomaa na mitumba tu kwa sasa,nikipata grade one hayo matakataka ya kichina nayatazama tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom