Historia ya Hermann von Wissmann Katika Vitabu Vyangu Viwili

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
HISTORIA YA HERMANN VON WISSMANN KATIKA VITABU VYANGU VIWILI
Tuanze na sanamu ya Hermann von Wissmann.

Picha na maelezo hayo hapo chini nimeyatoa mahali katika mtandao na nimefanya uhariri kidogo:

''Kabla ya sanamu ya askari iliyowekwa na Waingereza 1927, awali palikuwa na sanamu ya Gavana wa Deutsch-Ostafrika (DOA), Herman Wissmann iliyowekwa 1911.''

Napenda kuwaeleza wasomaji wangu nilivyomwandika Hermann von Wissmann katika kitabu cha Abdul Sykes historia hii ikiwa imetoka kwenye kinywa cha Affande Plantan akimweleza mwanae wa kulea Kleist Sykes kabla kifo chake tarehe 11 December, 1914.

Kisha In Shaa Allah nitamweleza Wissmann katika historia ya Muro Mboro wa Machame Nkuu aliyeishi wakati Wajerumani wanaingia Tanganyika mwishoni mwa miaka ya 1800.

Historia hii ipo katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama.

Affande Plantan amezikwa makaburi ya Ilala karibu na Uwanja wa Mpira wa Karume.
Muro Mboyo amezikwa Machame Nkuu katika ya ardhi yake mwenyewe.

''Efffendi Plantan, Sykes Mbuwane na mamluki wengine wa Kizulu walikuja Tanganyika katika meli ya kivita ya Wajerumani iliyotia nanga Pangani mwaka 1894.

Wazulu hawa walitokea Inhambane, Msumbiji iliyokuwa ikitawaliwa na Wareno.

Kijiji chao kilikuwa kinajulikana kama Kwa Likunyi. Mjerumani aliyewaleta toka huko alikuwa na sifa ya kuwa mwanajeshi na mvumbuzi, Harmine von Wissman. Wazulu wenyewe walikuwa wakiwaeleza watoto wao kuwa:

''Wajerumani waliweka mkataba na Mohosh, Chifu wa Inhambane nchini Msumbiji, kuwa watu wake watakwenda na Wajerumani hadi Tanganyika kupigana, wakakubaliana kuwa ardhi yoyote atakayoteka watagawana sawasawa kati ya Wazulu na Wajerumani.

Wajerumani waliwachukua Wazulu katika meli hadi Pangani chini ya uongozi wa Mohosh, shujaa wa vita ambaye baadae alikuja kujulikana kwa jina la Effendi Plantan.''

naandika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama nilimsoma tena Hermann von Wissmann katika mapambano na Wachagga.

Hivi ndivyo nilivyomweleza Wissman katika kitabu cha Rajabu Ibrahim Kirama:

''Mwaka wa 1890 Herman von Wissman baada ya kumaliza vita na Abushiri na kumnyonga alielekeza jeshi lake kaskazini na akamshambulia Mangi Sina katika vita vikali ambavyo jeshi la Sina lilionesha uhodari mkubwa wa mapambano.

Vita hivi vilinyanyua haiba ya Sina na Wajerumani wakanyoosha mkono wa urafiki na huo ndiyo ukawa mwisho wa uhasama baina ya Mangi Sina na Wajerumani.

Juu ya haya Rindi aliungana na Hermann von Wisssamann dhidi ya Sina na na hii ikapelekea kwa Sina kushindwa vita mwaka wa 1891.

Fitna na usaliti ukawa sasa ni moja ya silaha zilizowapa Wajerumani ushindi.

Sina alifariki mwaka wa 1899 akiwa kaacha sifa ya ushujaa wa vita mbele ya Wajerumani kwani peke yao hawakuweza kumshinda hadi ulipopitika usaliti dhidi yake.

Kunyongwa kwa Mangi Meli Old Moshi mwaka wa 1900 pengine yeye Muro Mboyo (baba yake Rajabu Ibrahim Kirama) akiwa shahidi wa mauaji yale ulikuwa ujumbe tosha kuwa nyakati zimebadika.

Meli kama ilivyokuwa kwa Abushiri na yeye alisalitiwa pia na wale aliokuwa akiwapigania."

1696050396323.png


1696050439083.png

1696050493355.png

1696050516647.png

 
Nimefarijika nimeelimika.

Je lengo la andiko lako ni kumuonesha Mjerumani kama shujaa ama.mhalifu aliyekuja kuambukiza dhambi ya usaliti kwenye jamii yetu iliyojijengea utu, ukarimu na upatanishi kabla ya watu weupe kuja?
 
Back
Top Bottom