Elections 2010 TBC wamefanya kweli

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Wadau, nimetazama taarifa ya habari saa 2 usiku tbc, wameonesha dr slaa alivyoiteka mwanza Jana. Ule Imati unaashiria jambo, hasa ukizingatia punde tu walikuwa wamepigwa mabomu ya machozi. Unaashiria kwa Shari kabisa kwamba wananchi wako tayari, kwa amani.
 
Ukweli TBC wana afadhali sana kulingasha na Channel Ten, Channel Ten wanatia aibu. Wameamua kuwa chombo cha propaganda badala ya kuwa chombo cha habari. Ikianza tu taarifa ya habari ujue maneno ya kwanza yatakuwa "mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi" hayo ndio maneno yao ya kwanza siku zote. Basi atapambwa hapo dak hata 20, ukisikia chadema ujue ni mashitaka hakuna cuf wala chama kingine. Watuambie kama imekuwa m/c ya propaganda ya ccm na wamejitoa kuwa chombo cha habari. TBC pamoja ya kuwa ndiye mwajiri wao, wanajitahidi sana.
 
Nilikusudia kusema " kwa dhati" badala ya "Shari"

Kuna kisehemu hapo chini kimeandikwa ''edit'' ukikiponyeza unaweza kuedit post yako
.naam DR anafanya mambo ya kweli na wananchi hatutaki masikhara sasa hivi.
Tushachoka usanii,usanii kuanzia kwa JK mwenyewe hadi makada wote mpaka serikali nzima inatuletea usanii lakini mwaka huu wamelima mchicha huku dibwi la kumwagilia ni letu(kura zetu) na hili dibwi sasa tumeamua kulijengea uzio kulizunguka tr 31 tuone maji ya kumwagilia mchicha wao watayatoa wapi.wanatuona sisi machizi majuha hatujui kitu,sikia
eti wanatishia hata kufungia gazeti la mwananchi huku daily news wakiliangalia tu,
sio wao ndio dailynews wenyewe wamesahau kuwa sisi ndio tumeshika mmpini (kura zetu) na lazima watatutambua.
Hakika watajuta na watatafuta sehemu ya kuficha vichwa vyao na maovu yao mengi ambayo yamejificha yatafunuliwa baada ya alama ya V kuingia madarakani....

Abiziani................................
 
Ni kweli ila nahisi wamepokea malalamiko kwamba kwanini watuletee taarifa kwa njia ya simu wakati yupo mpiga picha na mwandishi wao mkutanoni? Japo nafuu kdg
 
safi sana watu wa mwanza,nashukuru mkutano uliisha vyema bila tatizo maana ule msongamano mimi ulinitisha ungeweza kuwa kama disco toto na madhara yake (misongamano ya watu wengi na hatimaye kukosa hewa)
 
Ukweli TBC wana afadhali sana kulingasha na Channel Ten, Channel Ten wanatia aibu. Wameamua kuwa chombo cha propaganda badala ya kuwa chombo cha habari. Ikianza tu taarifa ya habari ujue maneno ya kwanza yatakuwa "mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi" hayo ndio maneno yao ya kwanza siku zote. Basi atapambwa hapo dak hata 20, ukisikia chadema ujue ni mashitaka hakuna cuf wala chama kingine. Watuambie kama imekuwa m/c ya propaganda ya ccm na wamejitoa kuwa chombo cha habari. TBC pamoja ya kuwa ndiye mwajiri wao, wanajitahidi sana.

Hivi Channel ten ni television ya nani jamani? Mimi zamani nilikuwa nafikiria ni ya Jenerali Ulimwengu. Lakini nikiangalia mtizamo wa Ulimwengu na mwelekeo wa hiyo television, sioni kabisa uhusiano. Hebu nifumbueni macho wakuu ni TV ya nani hii?
 
hivi channel ten ni television ya nani jamani? Mimi zamani nilikuwa nafikiria ni ya jenerali ulimwengu. Lakini nikiangalia mtizamo wa ulimwengu na mwelekeo wa hiyo television, sioni kabisa uhusiano. Hebu nifumbueni macho wakuu ni tv ya nani hii?

Mbona jibu rahisi "ni ya Mafisadi"
 
Hivi Channel ten ni television ya nani jamani? Mimi zamani nilikuwa nafikiria ni ya Jenerali Ulimwengu. Lakini nikiangalia mtizamo wa Ulimwengu na mwelekeo wa hiyo television, sioni kabisa uhusiano. Hebu nifumbueni macho wakuu ni TV ya nani hii?
Nasikia imenunuliwa na Rostum.
 
Hao Chanel 10 umesahau kuwa pia ni chombo cha yule fisadi-papa anayemiliki pia Rai, Mtanzania nk? Embu chunguza!! JE, Wewe ukikata tawi la mpapai litatoa utomvu wa muwa? basi tuvumilie...utomvu wa mapapai kama yalivyo Uhuru, Mzalendo....!

Ndugu; Nadhani hata muda wa kutizama hizi channels za ajabu, ujaribu kuupunguza kama sio kuacha kabisa...ina-corrupt mwelekeo wako kwa muda huo..achana nayo!! At least hadi Uchaguzi upite, Mtu Makini awepo Ikulu, hizi station za TV za 'nguvu za giza' zitatamani zisiwepo, au zijibadili majina..!
 
Channel Ten ni ya mzungu koko mmoja mutaliano. Ndivyo nilivyokuwa najua. Sasa inawezekana mafisadi wameivamia na kuinunua, kama kawaida yao ili wajitanue kwenye anga la habari na kufanikisha propaganda zao na kuifisadi nchi. Mimi nawashangaa watangazaji. Hivi hawaoni kuwa wanaiangamiza nchi kwa matumbo yao kwa kufuata amri za waajiri wao mafisadi!? Ama kweli sasa nimeami 'njaa' inaondoa uwezo wa kufikiri. Lakini wakae wakijua kuwa wanaunga mkono upande ulioshindwa na wajiandae kutafuta mabwana wengine.
Watanzania wa leo mpaka vijijini hawadanganyiki na propaganda za kipuuzi. Wanachoataka ni maendeleo, basi.

Jamani kaeni mkijua TBC hawafanyi hivyo kwa mapenzi yao.
Lazima kuna nguvu ya kimungu inayowasukuma kutenda hivyo ili watoto wa Mungu (wananchi) kupitia kwa mteule wake Dr. Slaa wakombolewe. Hivyo ndivyo ninavyoamini. Suala hili ukilitafakari ni pana sana. Inafika wakati mimi naamini hata sisi m kufanya madudu ni msukumo wa kimungu kwa maana kwamba imefumbwa macho ifanye 'madudu' yake ili kukamilisha mazingira ya kuleta ukombozi wa nchi. Jamani acheni Mungu aitwe Mungu.
 
Kuna wakati nilisiki channel ten ilinunuliwa na R. Mengi. Yule mtaliano alishindwa akaiuza. Kwenye taarifa sahihi tafadhali atuweke sawa
 
Ukweli TBC wana afadhali sana kulingasha na Channel Ten, Channel Ten wanatia aibu. Wameamua kuwa chombo cha propaganda badala ya kuwa chombo cha habari. Ikianza tu taarifa ya habari ujue maneno ya kwanza yatakuwa "mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi" hayo ndio maneno yao ya kwanza siku zote. Basi atapambwa hapo dak hata 20, ukisikia chadema ujue ni mashitaka hakuna cuf wala chama kingine. Watuambie kama imekuwa m/c ya propaganda ya ccm na wamejitoa kuwa chombo cha habari. TBC pamoja ya kuwa ndiye mwajiri wao, wanajitahidi sana.

bora umeona. Hao jamaa ni kimeo. Bora hata tbc wanaendesha mchakato majimboni
 
Dalili ya mvua? ...............

hapana nadhani ni nyota njema..... maana ule umati wa Mwanza ulikuwa wa kufa mtu pamoja na kupigwa mabomu ya machozi na vitisho lakini hawakutetereka bali waliendea kumsikiliza mgombea kwa makini sana.
 
CH kumi mbona vimeo tuu!
TBC sometimes wanakuwa fair and sometimes wrong
 
Ukweli TBC wana afadhali sana kulingasha na Channel Ten, Channel Ten wanatia aibu. Wameamua kuwa chombo cha propaganda badala ya kuwa chombo cha habari. Ikianza tu taarifa ya habari ujue maneno ya kwanza yatakuwa "mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi" hayo ndio maneno yao ya kwanza siku zote. Basi atapambwa hapo dak hata 20, ukisikia chadema ujue ni mashitaka hakuna cuf wala chama kingine. Watuambie kama imekuwa m/c ya propaganda ya ccm na wamejitoa kuwa chombo cha habari. TBC pamoja ya kuwa ndiye mwajiri wao, wanajitahidi sana.

nawapa big up sana ITV kwenye kipindi hichi wameonesha wao sio waganga njaa kama wengine
 
Back
Top Bottom