TBC sasa inaelekea iliko gazeti la Uhuru

HPAUL

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2011
Posts
410
Reaction score
567
Baada ya kuangalia tarifa ya habari Leo saa mbli ya TBC sasa ni dhahiri kabisa inaelekea kule lilipo gazeti la Uhuru, Nina maana ya kutokuwa na wateja kabisa. Najua wote mnaelewa Kuwa gazeti la Uhuru sasa hivi haliuziki kabisa labda chembe ya mauzo wanayopata ni taasisi za serikali. mawakala, wauzaji rejareja na wasafirishaji hawataki hata kuyaona. Reporting ya Leo ya TBC katika taarifa ya habari inayoendelea sasa hivi na hata wakati wanahitimisha live ufunguzi wa bunge maalum la katiba ni dhahiri inaelekea kule kule iliko fia gazeti la Uhuru kwa sababu zilezile za biased reporting. Waliohojiwa kwa comments ya Kikwete speech wote ni wabunge wa CCM. Sio Siri kwamba kwa kizazi cha sasa hivi zaidi ya 80% watazamaji, wasikilizaji na wasomaji ni Watu wanaopenda habari za mageuzi na sio mawazo mgando ya CCM. Kwaheri TBC na sasa mtegemee ruzuku tu.
 
umenikumbusha mbali hivi tbc ipo?? longtime sana lakn hata washabiki wa shshem huwa hawasikilizi extremly shamefully
 
Mimi huwa naingalia kwa nadra sana, na mara nyingi ni kwenye matangazo ya moja kwa moja ya Bunge, pale wengine wanapokuwa hawaonyeshi !

Baada ya kuangalia tarifa ya habari Leo saa mbli ya TBC sasa ni dhahiri kabisa inaelekea kule lilipo gazeti la Uhuru, Nina maana ya kutokuwa na wateja kabisa. Najua wote mnaelewa Kuwa gazeti la Uhuru sasa hivi haliuziki kabisa labda chembe ya mauzo wanayopata ni taasisi za serikali. mawakala, wauzaji rejareja na wasafirishaji hawataki hata kuyaona. Reporting ya Leo ya TBC katika taarifa ya habari inayoendelea sasa hivi na hata wakati wanahitimisha live ufunguzi wa bunge maalum la katiba ni dhahiri inaelekea kule kule iliko fia gazeti la Uhuru kwa sababu zilezile za biased reporting. Waliohojiwa kwa comments ya Kikwete speech wote ni wabunge wa CCM. Sio Siri kwamba kwa kizazi cha sasa hivi zaidi ya 80% watazamaji, wasikilizaji na wasomaji ni Watu wanaopenda habari za mageuzi na sio mawazo mgando ya CCM. Kwaheri TBC na sasa mtegemee ruzuku tu.
 
Eeh!

Wewe mkuu umechelewa kweli humu watu atulalamiki tena mambo ya tbc tunachukuwa hatua nina miaka kadhaa sasa sijaangalia tbccm
 
TBC1 ni television pekee inayoongoza Africa ya mashariki na kati

Nadhani ni kweli kua TBC1 inaongoza Afrika Mashariki na Kati kwa propaganda za kisiasa kama wakati ule wa ukomunisti. TBC1 ilikuwa chombo chenye heshima wakati wa Tido Mhando aliyejua ni nini maana ya kuwepo kwa chombo hicho cha Kitaifa. Ila sasa kimekuwa chombo cha siasa za kikomunisti tu.
 
Star tv wangekuwa wanatangaza bunge bila kukata kata nisingekaa niifungue tbc 1...
 
Wakati mwingine hata wahajatumwa ila ni tabia za watumishi wengi sasa hivi ni kujipendekeza kwa uongozi wa CCM!! Yaani ni wajinga kweli... Jitu utakuta linajipendekeza kwa CCM huku hali yake mbaya, kutwa kulialia shida na kukopa hovyo!!
 
Back
Top Bottom