TBC Mnakera sana!

TBCCM ni janga la Taifa, Mwakani CCM ikibwagwa wafanyakazi wote wafungashe virago tu. Ifungwe kwa muda wakati watawala wapya wanapanga safu zao. Halafu ndipo wakabidhi mitambo na ofisi na baadaye watafutwe wafanyakazi wapya wa kuendeleza gurudumu la maendeleo.
 
Mimi huwa najiuliza laini nashindwa kupata jibu: hivi watangazaji wote wa TBCCM ni makada wa CCM au wanajilazimisha tu kutekeleza matakwa ya CCM ili mradi mkono uende kinywani?
 
Inasikitisha sana !!!
Jana niliangalia habari na mwishoni wakasema nje ya bunge wabunge pia walipata nafasi ya kuelezea maoni yao lakini wakachukua maoni ya wajumbe wa ccm tu»»» jambo la ajabu
Wao ni kuegemea upande moja tu wala hawajui kubalance habari huku wanajiita "ukweli na uhakika"
 
Hata katika hii ripoti wakati mtangazaji akitoa introduction alisema kwamba baadhi ya wabunge waliochangia ni pamoja na Mh Duni Haji na Mh Injinia Habib Mnyaa. Lakini cha kushangaza kwenye main story michango ya Mnyaa na Haji haikurushwa hewani, na kipindi kiliisha saa 3:45 badala ya saa 4:00! Badala ya kurusha michango ya Mnyaa na Haji kwa dk 15 zilizosalia, mtangazaji kasema kipindi kimefika mwisho na hapo hapo akaanza kupiga taarab! Eee Mungu uwalaani wote wanaokandamiza maoni ya wananchi. Amen.
 
Ndio maana wao tu wanaruhusiwa kurusha matangazo liue.
 
Basi wafungue tv station mbona gazeti wameanzisha? Hata radio basi mbona ladyjaydee amefungua? Chadema watashindwa vipi? Japo gazeti lao news zao ni negative tu hakuna postive kama wenyekiti wamejihuzuru nk.
 
Mimi huwa najiuliza laini nashindwa kupata jibu: hivi watangazaji wote wa TBCCM ni makada wa CCM au wanajilazimisha tu kutekeleza matakwa ya CCM ili mradi mkono uende kinywani?

wanashida sana tuwaonee huruma tu. mzee masooood masooooooood wanamshindisha studio karibu masaa 24; na Marin hasan Marin nimegongana nae Mara mbili ubungo amepanda bodaboda. hata hela ya bajaji inazingua
 
Basi wafungue tv station mbona gazeti wameanzisha? Hata radio basi mbona ladyjaydee amefungua? Chadema watashindwa vipi? Japo gazeti lao news zao ni negative tu hakuna postive kama wenyekiti wamejihuzuru nk.

gazeti la Tanzania daima si laupande mmoja kama TBCCM ni juzi tu walilipoti "CCM wang'ara chalinze"
 
Mkuu, Laiti tu wangekusikiliza. Lakini wanasema; Sikio la kufa halisikii dawa. Hao wabunge wawili ni mwiba kwa ccm
mimimsiangaliagi ,imetokea wiki hii nipo safarini nikajikuta nilipo ni TBCMM pekee ndo ipo hewani ,aisee nimeogopa jamaa wamefungwa gavan ,sijui kama mtu mwenye akili kubwa kama anaweza kuvummila ujinga ule ....mh! siku ya ukombozi lazima watu wengine tuwan'oe hata nywele tu
 
Jaman hivi hakuna sheria au NGO au watetezi wahaki za raia ambao wanaweza kufungua kesi ya wananchi dhidi ya TBC kuwaomba. mahakama iwalazimishe TBC kubalance taarifa zao?
 
Jamani kitaifa tuna star tv, channel 10 na itv. Wasomi tunajua tusiangalie tbc maana huwezi kupata habari kamili, sahihi au mchanganyiko kama hizo channel zingine. If you want to be really current, drop tbc and watch the rest mentioned above.

Tbc ni janga la taifa tu!
 
Kama TBC walithubutu kuonyesha wanafunz wa UDSM wakimsomea dua Warioba ili afe ndani ya miaka mitano wanashindwa nini kufanya upuuzi wowote.
 
Mnajidai haimtazami TBC lakini utafiti unaonyesha nyie ndio watazamaji wakuu, kila mara mnakuja na malalamiko yasiyo na kichwa wa mguu humu!
 
Jaman hivi hakuna sheria au NGO au watetezi wahaki za raia ambao wanaweza kufungua kesi ya wananchi dhidi ya TBC kuwaomba. mahakama iwalazimishe TBC kubalance taarifa zao?

Hata mimi nimekuwa nikijiuliza sana swali kama hili. MCT je?
 
Mnajidai haimtazami TBC lakini utafiti unaonyesha nyie ndio watazamaji wakuu, kila mara mnakuja na malalamiko yasiyo na kichwa wa mguu humu!

Siku ukijifunza kujitegemea hutajitoa akili kiasi hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…