TBC Mnaibagua Chadema Mpaka lini?

TBC Mnaibagua Chadema Mpaka lini?

Ubaguzi kwa wana chadema, ni mkubwa utadhani ccm ndio walipa kodi peke yao. Ebu Angalien TBC1, hawawezi kutoa habari yeyote nzuri ihusiyo cdm, bali mbaya ndio wataitangaza weeeee. lkn ikiwa hata katibu wa ccm wa kata ameongea watairusha hewani kuliko kurusha ya m\kiti wa cdm. Mshana Naomba uelewe ya kuwa hata CDM nao wanahaki ya kusikiliza yanayofanya na viongozi wao kupitia vyombo vya habari vya Uma na sio ccm peke yako.
Na wewe mbaguzi! Kwa nini CDM tuu? Kuna vyama zaidi ya 15 mbona huvizungumzii?
Toeni huo uchafu unaoitwa CDM!
 
TBC wahangaike kuonyesha CDM wanavyo zomea watu kwenye mikutano! TBC acha neni kabisa na Chadema hadi wawambie wameacha tabia yao ya kuzomea zomea!

Mi sijaema kwenye mikutanao tu. Kwa mfano chadema walikuwa na mkutano wa halmashauri kuu last week, baada ya kikao hicho waliitisha press conference, Vyombo vingine vya habari kama Mlimani TV, ITV, Chanel Tena na Magazeti yalitoa ile habari lkn TBC hawakutoa hiyo habari bali walitoa habari ya Husen Bashe. Hiki ndicho nasema Kodi tunalipa sote.
 
Hii TV inaendeshwa na kodi zaq wananchi na wala si michango ya CCM, ipo siku tutaikomboa tuu hii nchi yetu
 
Chadema acheni ulalamishi, anzisheni tv yenu.
Kama mama Rwakatare kaweza, kwanini nyie mshindwe?
Kwani TBC1 ya ccm si nao waanzishe ya kwao! NDO MAANA CCM ITAKUFA TUU! HAYO WANANCHI TUNAYAONA NI MAGAMBA MENGINE TENA!
 
Hata CDM wakianzisha TV yao still watadai haki ya kuonyeshwa TBC kwani ni mali ya wananchi wote.
 
Imefikia hatua siangalii tena Habari kwao bora vituo vingine, wasipoangalia watarudi kipindi kile cha TVT...
 
Ndio maana huwa mimi nikitaka kuona au kusikia taarifa juu ya siasa na utawala wa nchi yangu, basi naizima TBC na kuwasha channel nyingine yeyote....! Mara nyingine bora niweke mkanda badala ya kuwaangalia wao TBC....!
 
Lakini wakumbuke mwisho wao unakuja na tena ni karibu sana, hawatakuwa upande wa ccm wara cdm au cuf.
Siku ambayo kila kilicho cha uma kitakuwa kwa ajili ya uma, SIKU HIYO TUNAINGOJA SANA

Mkuu hiyo siku ikifika ndipo na Bw. Yesu atakuwa amefika, ni lini vile?
 
Eti wana motto inasema Ukweli na uhakika si wabadilishe iwe uongo wa uhakika
 
Nimesoma mawazo ya watu tofauti kuhusu ubaguzi wa TBC anaouzungumzia Markach japo naye hakuweka wazi habari ipi haikutangazwa. Unajua siku zote ukikaa kulalamika kama mtoto yatima utaendelea hivyo kulalamika kuwa unaonewa hata kama hubaguliwi, tuzungumze kwa tawimu jamani, Wakati Chadema wanafanya maandamano nchi nzima kuzungumzia kupanda kwa gharama ya maisha kuna habari iliachwa? ilitangazwa kila siku na waandishi wengine wanatumwa kubalance kwa serika ijibu tuhuma zile kwasababu ilikuwa maslahi ya umma na watanzania wote tunaumia kwa bei ya vyakula kuwa juu, sasa habari ipi haikutangazwa hadi useme kuna ubaguzi? Sisi wa vijini tunasikiliza sana TBC Taifa na habari zote za Chadema tunapata kila siku, hatulalamiki, TBC1 hal kadhalika sasa wewe tuatkuelewaje?

Jana Mbowe akizungumzia bajeti ijayo nilisikia kwenye taarifa ya habari ubande wa TBC Taifa (redio) ambayo wote mliotoa mawao hapa hamsikilizi kwasababu mpo mjini mnajua TV tu nilisikia habari ya mbowe kwenye taarifa ya habari na pia kwenye kipindi cha Jungu kuu(matukio saa nzima saa 3 hadi saa 4 usiku) upande wa Tv yaani TBC1 mnayozungumzia nimeisikia asubuhi kwenye taarifa ya habari sasa with good coverage sasa mnalalamika nini jamani watanzania? najua wengine mmechangia tu hamjaangalia hiyo taarifa, msiwe na tabia ya kufuata mkumbo jamnai mjivunie shirika lenu la umma, tumeni maoni yenu na ushauri kwa TBC mkiwa nayo siyo malalamiko kwenye jamvi hapa bila takwimu. Sasa wengine wamesema wakati wa Tido mabo yalikuwa mazuri alitangaza vizuri chadema ndiyo maana kafukuzwa, jamani binadamu hawana wema na ni wanafiki kweli, si mlisema Jangwani kakata matangazo wakati wa kampeni kwasababu hapendi CDM? leo tena mnasema hivyo?
Haya mwingine umesema Mshana kepewa maagizo kufanya kazi ya CCM ana kadi ya chama, sasa imekuwaje jana habari ya mbowe imetangazwa vizuri japo hamkuona ndiyo maana mnalalamika hapa, fikirieni kitaifa na kwa maslahi ya umma wetu, msipandikize mawazo maovu kwa watu kuhusu shirika lenu la uuma.

Kwa jinsi nilivyosoma mawazo ya mliochangia hapa ni kwamba mnataka kutukuza vyombo binafsi ambayo hata ukiulizwa wanafanya nini kwa maslahi ya taifa utasema wanaaandika au kutangaza vizuri chama chako, sasa hapo ndo ugonjwa wako, chombo cha umma kinatangaza maswala ya uuma, kama CDM itasema jambo la kitaifa kama kupanda bei hiyo ikiachwa lalamika, lakini cDM wakimtukana Rais nayo iandikwe? hiyo ni habari? ukigombana na mkeo ukiwa kiongozi nayo ni habari? mfano wanasema Slaa na mbowe wanaweza timuliwa Chadema, TBC nayo iingie kwenye uchochezi huo? tafakarimara mbili vaa uzalendo tofautisha chombo cha umma na chombo binafsi.

Naomba kwasilisha mawazo yangu binafsi kama raia mwema huku kijijini.
 
Ubaguzi kwa wana chadema, ni mkubwa utadhani ccm ndio walipa kodi peke yao. Ebu Angalien TBC1, hawawezi kutoa habari yeyote nzuri ihusiyo cdm, bali mbaya ndio wataitangaza weeeee. lkn ikiwa hata katibu wa ccm wa kata ameongea watairusha hewani kuliko kurusha ya m\kiti wa cdm. Mshana Naomba uelewe ya kuwa hata CDM nao wanahaki ya kusikiliza yanayofanya na viongozi wao kupitia vyombo vya habari vya Uma na sio ccm peke yako.

Nanyi ni wabaguzi,kwa nini waoneshwe cdm na si vyama vingine.mbona itv hamuilaumu kwa ubaguzi au kwa sababu inawaonesha zaidi cdm? habari za cdm haziuzi,kila siku maandamo shughuli za maendeleo ziro.
 
"mimi najiuliza hawa wazee wanajifunza nini wanapoenda ziara nchi za nje yaani wanafanya mambo ya kijinga kweli.Siku hizi ukiangalia TBC taarifa ya habari kidogo tu inakata". Ndugu yangu viongozi wetu ni mbingwa wakuiga mambo mabaya,hv hujielizi Rais wetu akienda nje mfano marekani anaongea nini na Obama.Sijawahi kusikia labda ameomba vijana watanzania waende huko kusoma instead nafasi za masomo zikitolewa wanaenda watoto wao na wanaowapenda wao zikibaki wanatupia huko.
 
Mshana ni CCM, alikuwa mmojawapo wa watunza hazina wa Chama...
 
Chadema acheni ulalamishi, anzisheni tv yenu.
Kama mama Rwakatare kaweza, kwanini nyie mshindwe?
Kumbuka TBC ni chombo cha umma na siyo chama wala mtu binafsi mzeee.
Mchakato majimboni umemtokea puani Mhando TBC sasa kaletwa Mshana, amekula kiapo kwanza cha kutekeleza matakwa ya chama cha Magamba kabla ya kuingia ofisi za TBC, kazi ipo.
 
Tido ameondolewa pale kwa sababu alijaribu kuweka usawa sasa huyu Mshana nadhani ni moja ya maagizo ya yeye kuwepo TBC ni kuhakikisha habari za CDM ni zile -ve tu
 
Gabriel Zacharia na Malin h malin wanahusika sana katika hili.Hata habari ya cdm inaporushwa huwa ni vipande ambavyo havieleweki.Mfano kuna siku fulani kesi ya cdm arusha Lema alipotembea kwa miguu na badae kupigwa mabom,TBC walitangaza hivi'Hata hivyo wakati kesi hiyo ikiahirishwa ilibidi polisi watumie nguvu kusambaratisha raia waliokuwa wakiambatana na mmoja wa watuhumiwa pale alipoamua kutembea kwa miguu kutoka mahakamani'Hata picha waliyorusha ilikuwa si rahisi mtazamaji kujua kama yule mtuhumiwa ni Mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema.Nafikiri hii ilikuwa ni utekelezaji wa agizo la kutompa Lema umaarufu kwakuwa kipindi hiko lile sakata la Pinda kudanganya lilikuwa juu.Kuna maagizo yanayotekelezwatbc1 kutoka kwa viongozi wa ccm kuhakikisha wanafifisha nguvu ya cdm.Lakini pia nawashangaa hawa watangazaji kwa jinsi wanavyokubaliana na kuweka nyuma maadili ya kazi yao na kuendekeza ukanjanja.GABRIEL ZACHARIA NA MALIN H MALIN wanahusika sana,tusiishie kwa wakurugenzi tu,kwa nini watangazaji wakubali kutumika kulinda maslahi ya watu wachache?
 
Wewe subiri uone wala haitschukua muda mrefu! by the way hivi na wewe umeshavua gamba?
 
Back
Top Bottom