TBC Mnaibagua Chadema Mpaka lini?

markach

Senior Member
Oct 18, 2010
121
12
Ubaguzi kwa wana chadema, ni mkubwa utadhani ccm ndio walipa kodi peke yao. Ebu Angalien TBC1, hawawezi kutoa habari yeyote nzuri ihusiyo cdm, bali mbaya ndio wataitangaza weeeee. lkn ikiwa hata katibu wa ccm wa kata ameongea watairusha hewani kuliko kurusha ya m\kiti wa cdm. Mshana Naomba uelewe ya kuwa hata CDM nao wanahaki ya kusikiliza yanayofanya na viongozi wao kupitia vyombo vya habari vya Uma na sio ccm peke yako.
 
Ila kweli hawa jamaa mazuzu kweli utadhani wanalipwa na ccm ndio maana watu wengi mtaani wameacha kuangalia vipindi vyao,TIDO alitaka kuwa huru serikali ya ccm imemuondoa mimi najiuliza hawa wazee wanajifunza nini wanapoenda ziara nchi za nje yaani wanafanya mambo ya kijinga kweli.Siku hizi ukiangalia TBC taarifa ya habari kidogo tu inakata.
 
Ubaguzi kwa wana chadema, ni mkubwa utadhani ccm ndio walipa kodi peke yao. Ebu Angalien TBC1, hawawezi kutoa habari yeyote nzuri ihusiyo cdm, bali mbaya ndio wataitangaza weeeee. lkn ikiwa hata katibu wa ccm wa kata ameongea watairusha hewani kuliko kurusha ya m\kiti wa cdm. Mshana Naomba uelewe ya kuwa hata CDM nao wanahaki ya kusikiliza yanayofanya na viongozi wao kupitia vyombo vya habari vya Uma na sio ccm peke yako.

Kwani mshana ana kadi ya chama gani. Kama hana anaweza kukusikiliza. Watumishi wa umma wanruhusiwa kuwa wanachama wa CCM tu. Kama asingekuwa na kadi asingepewa hiyo nafasi. Dawa CDM anzisheni TV.:israel:
 
Chadema acheni ulalamishi, anzisheni tv yenu.
Kama mama Rwakatare kaweza, kwanini nyie mshindwe?
 
TBC ni chombo cha umma,kinaendeshwa kwa kodi za wananchi wote,bila kujali ni wanachama wa chama gani,hivo wana wajibu wa ku cover taarifa zote zinazohusu watanzania,wala sio kuegemea upande fulani.au wanapewa ruzuku na ccm? hawa wameanzisha redio,magazeti,si waanzishe na tv stesheni yao?hii ya umma watuachie sisi watanzania.wengine tukiona tu hiyo rangi ya kijani hata appetite ya dinner inapotea!!
 
Sumbalawinyo kwani Rwakatare ni yake si ya pesa zetu wanazochukua kwa kutumia kadi ya ccm,moja ya kosa kubwa la ccm ni kuruhusu matajiri kuitawala nchi Mama Rwakatare ana uwezo gani kuwa mbunge lakini mimi naifahamu ccm vizuri vijana wao njaa imewashika baba zao ndio wanaokula nchi,lakini vijana wao hata hawashituki bongo zao zina kansa
 
Lakini wakumbuke mwisho wao unakuja na tena ni karibu sana, hawatakuwa upande wa ccm wara cdm au cuf.
Siku ambayo kila kilicho cha uma kitakuwa kwa ajili ya uma, :israel:
 
Lakini wakumbuke mwisho wao unakuja na tena ni karibu sana, hawatakuwa upande wa ccm wara cdm au cuf.
Siku ambayo kila kilicho cha uma kitakuwa kwa ajili ya uma, SIKU HIYO TUNAINGOJA SANA
 
Lakini tukiangalia upande wa pili wa shilingi kuna maadili ya uanahabari na ethics za taaluma ya habari...hivi vyote hivi wameviacha TSJ na sasa ni kulinda tu kitumbua?...well! Kwa kukubali kutumika kwa namna wanavyotumika sasa siku bwana aliyekuweka hapo akipata mridhi uso wako utauweka wapi!....nionavyo taaluma ya habari inatakiwa watu wenye moyo wa udhubutu ambao wana msimamo kwa yale wanayoamini na si kukubali tu kutumiwa kwa ahadi za fulana na chandarua!
 
TBC wahangaike kuonyesha CDM wanavyo zomea watu kwenye mikutano! TBC acha neni kabisa na Chadema hadi wawambie wameacha tabia yao ya kuzomea zomea!
 
Najua Kabisa Mshana ana special package ya Mshahara wa Tsh 15,000,000 kwa mwezi ili kufanya anayofanya ila ajue kuna mwisho wake. Hii package ni kubwa sana hata mwenyewe sijui ni nini inasababisha alipwe pesa zote hizo za walipakodi akiwa hawatendei Haki!!!!
 
TBC1 wakumbuke kwamba kuficha ukweli kuna siku kutawaumbua,wameamua kutotoa habari zozote zinazohusu Chadema labda ziwe zile za Wasira,Mrema,Cheyo,UVCCM Nape au CCM wakiponda Chadema kwa kufanya hivyo wamejishushia hadhi sana kwa sababu hata wakionyesha kitu chochote cha ukweli kuhusu Chadema wananchi wanajua ni propaganda za TV hiyo,katika nchi zote TV ya taifa huwa ndio kimbilio la wananchi kwa kupata habari za uhakika,lakini hapa wananchi tunaidharau TBC1 kwa kuendesha propaganda za enzi za utawala wa kikomunisti zamani,zile za kughilibu akili za wananchi,wakati wananchi sasa hivi wanapata habari za uhakika kutoka magazeti,interneti na station zingine za TV
TBC1 toka TIDO aondoke imeshuka hadhi tu Zero,kunakipindi ITV,STar TV,Channel Ten walikuwa hawaoni ndani kwa TBC1 ,lakini sasa watu wanaaimini hizo station zingine ,pole TBC1 munaelekea kuzikwa
 
Hiyo ndiyo priority yake ya kwanza aliyopewa wakati anateuliwa.
Hata hivyo nguvu ya umma ina njia nyingi za kusikika. Wakiona hizo propaganda zao zinashindikana ndo wanaleta unafki wa kutoa viji-coverage vidogovidogo.
Na kitaeleweka tu.
 
Chadema acheni ulalamishi, anzisheni tv yenu.
Kama mama Rwakatare kaweza, kwanini nyie mshindwe?

Lakini tbc si mali ya ccm inaendeshwa kwa kodi zetu na inapaswa itumike kwa vyama vyote na watanzania wa kada zote bila kujali dini au itikadi za kisiasa
 
Kupata haki siku zote ni gharama sn,TBC walimuondoa Tido ili waweze kupambana Kama sio kusalia madarakani kwa gharama yyt ile.
 
Kumuondoa mhando TBC ni kosa kubwa ambalo ccm wamelifanya kwa maslahi ya kisiasa lakini watambue kuwa wananchi wa leo sio wale wa zamani. hata wakipiga propaganda zao watu wanaelewa
 
Back
Top Bottom