Uchaguzi 2020 Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961


Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake katika mkutano wao wa kuzindua Kampeni za Mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Zakheim, Mbagala Jijini Dar es Salaam, jioni hii.

TBC1 na TBC Taifa kama chaneli za umma zilikuwa zinarusha matangazo ya moja kwa moja kwenye uzinduzi huo kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mwongozo wa Tume wa mwaka 2020, (kifungu e na j), kanuni za maadili ya tasnia ya habari; vyombo vya utangazaji vya umma pia vinao wajibu wa kuhakikisha maudhui yanayorushwa hewani yanazingatia maadili ya taaluma na ya jamii.

Kitendo cha uongozi wa CHADEMA kutangaza kuwafukuza watangazaji wa TBC si cha kiungwana na kinahatarisha usalama wa watendaji hao na vifaa vyao.

Pamoja na kwamba TBC inapanga kutoa taarifa rasmi Polisi na kwenye Tume ya Taifa ya Uchaguzi, kwa sasa inasitisha rasmi kurusha matangazo ya CHADEMA hadi hapo watendaji wake watakapohakikishiwa usalama.

TBC inapenda kutimiza wajibu wake wa kisheria na imekuwa tayari, siku zote, kufanya kazi na vyama vyote vya siasa bila ubaguzi.
News Alert: - Yaliyojiri kwenye Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu katika viwanja vya Zakheim Mbagala, TBC Wafukuzwa
 
Tundu Lissu kweli kawashika MATAGA kunako.

TBC wanalia!
Polisi huko Twitter wanalia!

wameshikwa haswaaa!


1598634756304.png
 
Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Limesikitishwa na kitendo uongozi wa CHADEMA kuwakemea na kuwafukuza watangazaji wake katika mkutano wao wa kuzindua Kampeni za Mgombea wao wa Urais katika viwanja vya Zakheim, Mbagala Jijini Dar es Salaam, jioni hii...
BAK Kuna sehemu ulini quote na clip fulani ya mkulu. Hebu ilete huku tuone kama TBC waliyaminya yale maudhui ya kupiga mashangazi.
 
Back
Top Bottom