Mzozo wa CHADEMA na TBC: Nitasema mimi kiazi, wewe muhogo una mzizi'!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
106,867
2,000
MZOZO WA CHADEMA NA TBC: 'NITASEMA MIMI KIAZI, WEWE MUHOGO UNA MZIZI'!

Wiki iliyopita nilihudhuria Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Tundu Lissu katika Viwanja vya Zakhiem, Mbagala jijini Dar es Salaam. Kama kawaida yangu, nilitoa nasaha au hotuba fupi kabla ya kuufungua Mkutano ule kwa Sala. Baada ya hapo viongozi kadhaa wa CHADEMA walihutubia akiwemo Mwenyekiti wake Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Kulikuwepo na vyombo kadhaa vya Habari likiwemo Shirika la Utangazaji la Tanzania, TBC. Yapo matendo yaliyoonyeshwa au kufanywa na TBC yaliyopelekea Mheshimiwa Mbowe kuwafukuza mkutanoni siku ile. Kama Askofu nilishtuka na kushangaa kwa kuwa tukio lile halikuwa la kawaida ingawa kwa tulio wengi lilikuwa na tafsiri yake katika 'ulimwengu wa roho'. Mwitikio (reactions) kutoka kwa Mbowe ulikuwa wa ghafla (instant) ambao hata hivyo ulionekana kujengwa katika misingi ya kihistoria ya mahusiano kati ya CHADEMA au Viongozi wake na TBC.

Askofu ni mtetezi wa haki na haki haina upendeleo! Lakini katika tukio lile, Askofu alijikuta akikutana na mwitikio (reactions) kutoka kwa watu wanaodhani kuwa hawakutendewa haki na TBC. Kwa kuwa Askofu alikuwa ameukabidhi Mkutano ule mikononi mwa Mungu na kusafisha anga lote la Mbagala, akiendelea kuwa mtulivu kwa kuwa aliamini kuwa mbingu zilikuwa kazini.

TBC ni taasisi ya Umma inayoendeshwa kwa kodi za wananchi wa Tanzania wakiwemo wafuasi wa CHADEMA na vyama vyote vya Upinzani. Huko nyuma niliwahi kuisema TBC hadharani kupitia ukurasa wangu kuwataka waache upendeleo. Ni dhahiri kuwa baadhi ya matokeo ya hisia za upendeleo ni yale tuliyoyaona kule Mbagala wakati TBC ilipofukuzwa Mkutanoni. Watangazaji, Wapiga Picha, na Waandishi wa Habari wa TBC ni watoto wa nchi hii. Wao hawahusiki sana kwa kuwa wako chini ya watu wanaotoa maelekezo. Kama kuna shida ye yote kuhusiana na utendaji wa TBC wasilaumiwe hao, bali walaumiwe waliokabidhiwa kuongoza TBC akiwemo Mkurugenzi wake Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi.

Mara kadhaa TBC imerusha hewani maudhui ya viongozi wa serikali inayotokana na CCM pasipo kukatisha matangazo hayo hata kama baadhi ya viongozi hao wametoa kauli ambazo kwa muono wetu kauli zile zinadharirisha watu wengine! TBC na Vyombo vingine vya Habari kwa pamoja vimevumilia maudhui kama hayo kurushwa mubashara pasipo kukatizwa. Hivi karibuni nimewasema Star TV kwa kuruhusu maudhui yaliyokuwa yanamfedhehesha Mgombea Urais wa CHADEMA, Mheshimiwa Tundu Lissu kupitia kipindi cha 'Agenda 2020' kinachoongozwa na Aloyce Nyanda 'Mtozi'! Star TV haikukatiza matangazo yale ingawa huko nyuma iliwahi kukatiza matangazo ghafla wakati mmoja wa viongozi wa CHADEMA akitoa hoja.

Vitendo vya kuchagua maudhui ya kurusha kwa upande wa Upinzani na kutokuchagua maudhui ya kurusha kwa upande wa CCM na Serikali yake ndivyo vinavyopelekea baadhi ya Vyombo vya Habari ikiwemo TBC walaumike na kuhisiwa kuwa wana upendeleo. Haijawa mara moja baadhi ya Vyombo vya Habari kusitisha matangazo kwa muda endapo yanayoongelewa na Wapinzani yanaonekana kuwa tishio kwa CCM na Serikali yake. Lakini vyombo vya Habari havitakiwi kufika huko. Vyama vya Siasa vyote vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu ni vyama halali na chama chochote kati ya hivyo kinaweza kushika dola. Hakuna Chama cha Kigaidi katika hivyo, la sivyo visingelisajiliwa na kuruhusiwa kushiriki Uchaguzi Mkuu.

Vyombo vya Habari na hasa TBC watende haki na watimize wajibu wao pasipo upendeleo hasa ikizingatiwa kuwa wao wanaendeshwa kwa kodi za Watanzania wote.

Tunatoa wito kwa TBC na CHADEMA kuketi na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza. Tunahimiza uvumilivu kwa pande zote mbili wakati wa kushughulikia jambo hilo. Taasisi zote mbili yaani TBC na CHADEMA wajizuie kuendelea kutoa kauli endelezi hadharani kuhusiana na suala hilo zaidi ya kutafuta suluhu.

Wazaramo wana msemo usemao: "Sema wewe kiazi, nikisema mie muhogo nina mzizi'! Na mimi kama Askofu nimeamua kusema yale ambayo wengine wanaogopa kuyasema!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki
 

Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,746
2,000
CCM bado hawana uwezo wa kushindana kisiasa. Hii imethibitika baada ya kauli ya Mgombea wa ccm kuwaambia wapiga kura "Misichague viongozi wa upinzania hata kama wanafaa".

Kauli hii yenye ukakasi imezua tafakuri si kwa wapinzani peke yake, bali hata kwa wana ccm wa kawaida. Inafichua ni kiwango gani ccm imehujumu maendeleo ya taifa kwa matumizi mabaya ya raslimali za taifa wakiwemo watu ambao ni hazina ya taifa.

Tumeshuhudia kwa kipindi fulani sasa ni namna gani majimbo yanayoongozwa na upinzani yakihujumiwa maendeleo, kwa kubaguliwa eti walichagua upinzania bil kujali kwamba hawa wananchi ni walipa kodi tena wazuri pengine kuliko hata wana ccm ambao ni mafisadi wa vizazi na vizazi, ila wanabadili rangi na aina ya ufisadi tu kama vinyonga.

Kuna maeneo ambayo hata fursa za miradi mizuri ya maendeleo zilizuiliwa na wakurugenzi eti kwa kuwa tu halmashauri ziko upinzani (Hili mimi ni shahidi, nilishuhudia wakati nimetembeleo ofisi ya Manispaaa Arusha. Kuna mtu mmoja alikwenda kwa Mkurugenzi akiwa na mradi wa supply ya maji na salama kwa mji mzima wa Arusha uliokuwa na manufaa lukuki yakiwemo afya, umeme, mazingira, uzalishaji, etc, bila kuongeza gharama ya maji kwa mtumiaji. Ilikuwa wananchi wawe wanafungulia maji bombani kokote na kunywa bila kuchemsha. Kwa masikio yangu wakati huyo mwananchi anawasilisha, alijibiwa na Mkurugenzi "Umepitia halmashauri, halmashauri yenyewe ni ya CHADEMA, mradi hautekelezeki". Niliugua moyoni ni kumfuata huyo Mtanzania akiwa na mabahasha yake, ndipo nilipojua huduma.

Lakini hii ni kwa sababau ccm hawana uchungu na maendeleo wala ustawi wa taifa na ndiyo sababu wamefanya hujuma kama hizi ili kuwaaminisha wananchi wapiga kura wenye uelewa mdogo kwama "Wapinzania hawawezi kuwasaidia" Hii si haki Mbele za Mungu.

Mgombea wa ccm aliposema "Msiwachague wapinzani hata kama wanafaa" eti wachague ccm ili awabane. Hii ina maana

1. Nchi inaongozwa na utashi wa mtu na si mfumo wajibishi. Ikitokea kiongozi anayefanya juhudi za kuwabana watu akawa na udhuru wa kutokuwa ofisini, hakuna uwajibikaji, n ahata juhudi anazosimamia zinakomea pale, bila haki ya mtu kuhoji uendelevu wake.

2. Hao anaosema wachaguliwe atawabana, ameshindwa kuwabana hadi sasa ni diyo sababu ya tumeshuhudia aki recycle mawaziri hadi basi. Hii ni kutokana na kuwa na watu wasiofaa, wasiokuwa na uwezo wala sifa sahihi ambao wamekuwa mizigo si kwake tu bali kwa taifa. Kuongozwa na viongozi mizigo, kumeliletea taifa hasara kiasi gani cha kazi duni, upotevu wa muda na gharama za malipo yao?

3. Mheshimiwa angelikuwa na uwezo wa kuwabana, bila shaka angewarekebisha wakafanya kazi sahihi kwa kiwango sahihi. Lakini kuwabana kwa kuwafukuza kazi, ni dhahiri hawa watu si wa kurekebisha maana hawana uwezo wa kubadilika.

4. Kuwa na viongozi wanaotegemewa kubanwa ili wafanyekazi, ukaacha watu wenye sifa na uwezo ambao wamesomeshwa na taifa hili kwa gharama kubwa, wenye vipaji ambavyo Mungu amelitunuku taifa hili, ni kukosa uzalendo na ni hujuma kubwa kwa taifa.

5. CCM imedhihirisha kukosa uwezo wa kutumia raslimali za taifa ipasavyo na ndiyo sababu hawana uchungu kutamka wachaguliwe watu hata kama ni wa hovyo kwa gharama ya kodi za Watanzania, walipwe kwa kodi za wananchi, watumie muda mkubwa wa kukimbizana na kukwepana ambao ulitakiwa uwe muda wa kulizalishia taifa, watu ambao hawana uwezo wa kurithisha kitu chema kwa vizazi vijavyo kti ambacho ni cha huzuni sana.

6. Unaweza kuwabana watu katika utekelezaji wa maazimio. Lakini unawezaje kumbana mtu asiye na uwezo ili atunge sera na sheria za nchi? Hawa wanaopigiwa debe kwamba walpewe tu uongozi hata kama hawana sifa, watakwenda bungeni kuchanganua bills na kuzipitisha ama kushauri masuala ya levels gani katika dunia hii inayoathiriwa na masuala mbalimbali ya utandawazi? Hawa watu wanajua sera za nchi na sheria zinapashwa kuzingatia mambo gani? Wanapeleke wapi nchi yetu hawa?

7. Nimepata kwikwi sana katika hili nikaona, picha pana sana juu ya kukaatwa kikatili majina ya wagombea wa upinzania, kutokusilikizwa hata wakiwa na hoja za msingi kiasi gani, hila za kucheleweshwa mashauri ya uchaguzi, matumizi ya nguvu kama utekaji n.k bila kujali kwamba tunajenga taifa moja.

8. Kwa kuzingatia mambo mengi nyuma ya udhaifu huu, ninatoa wito kwa Watanzania wote, tuchague wawakilishi wenye sifa na wanaofaa bila kuajli vyama ili CCM wajifunze kutumia raslimali za taifa kwa maslahi ya taifa. Asiyetaka kufanya kazi na watanzania wenye sifa eti kwa sababhu hawezi kuwa thibiti, ni mtu asiyejue kwamba uongozi ni mifumo na bila mifumoa sahihi hakuna maendeleo endelevu hivyo, ajitathmini.
 

Kiongozi mkuu2020

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
1,412
2,000
Waandishi wa habari wana utamaduni wao wa kutoa taarifa inayoenda moja kwa moja kwenye jamii. Hivyo si kila tamko au mijadala inayozungumzwa huwa inapelekwa moja kwa moja . hivyo lazima ichujwe kwanzaaa.

Hivyo kinachowagarimu nyie hadi jamaa yenu mkuu akakasirika vile ni kwa sababu mlitaka kila mnalopayuka liende moja kwa moja kwenye umma wa watu.

TBC ni waandishi wa habari mahiri wanaozingatia miiko na taratibu za taaluma yao.
 

AGITATOR

JF-Expert Member
Apr 7, 2019
1,354
2,000
CCM bado hawana uwezo wa kushindana kisiasa. Hii imethibitika baada ya kauli ya Mgombea wa ccm kuwaambia wapiga kura "Misichague viongozi wa upinzania hata kama wanafaa".
Kauli ni sahihi maana wakiingia kule mjengoni ni kususa na kupinga kila kitu sasa tutapitishaje hoja zao waliopiga kura?. Safari hii wana saccos wa Ufipa, mtakula wa chuya.
 

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,289
2,000
Waandishi wahabari wanautamaduni wao wakutoa taarifa inayoenda mojakwa moja kwenye jamiiiii. Hivyo sikila tamko au mijadala inayozungunzwa huwa inapelekwa mojakwa moja . hivyo lazima ichujwe kwanzaaa.
Hivyo kinachowagarimu nyie hadi jamaa yenu mkuuu akakasirika vile nikwa sababu mlitaka kila mnalopayuka liende moja kwamoja kwenye uuma wawatuuu.
TBC ni waandishi wahabari mahili wanaozingatia miiko na taratibu za taaluma yao.
Mkuu, umesoma na kuelewa au umekimbilia ku komenti moja kwa moja!?
 

Tabby

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
10,746
2,000
Waandishi wahabari wanautamaduni wao wakutoa taarifa inayoenda mojakwa moja kwenye jamiiiii. Hivyo sikila tamko au mijadala inayozungunzwa huwa inapelekwa mojakwa moja . hivyo lazima ichujwe kwanzaaa.
Hivyo kinachowagarimu nyie hadi jamaa yenu mkuuu akakasirika vile nikwa sababu mlitaka kila mnalopayuka liende moja kwamoja kwenye uuma wawatuuu.
TBC ni waandishi wahabari mahili wanaozingatia miiko na taratibu za taaluma yao.

Hiyo censor ni kwa upinzani tu? Unatumia mzani gani kuchuja kwamba hili wananchi wasilisikie na hili walisikie?

CCM you are too shallow with no qualities to lead the country. Mnafanya ukanjanja tu na ndiyo maana hata mkiandika, ni maushoes tu!.
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,652
2,000
Hivi waandishi wa TBC WANGEVAMIWA NA ILE HALAIKI NA KUSHAMBULIWA TUNGEANDIKA HAYA?
 

Kiongozi mkuu2020

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
1,412
2,000
Hiyo censor ni kwa upinzani tu? Unatumia mzani gani kuchuja kwamba hili wananchi wasilisikie na hili walisikie? CCM you are too shallow with no qualities the country. Mnafanya ukanjanja tu na ndiyo maana hata mkiandika, ni maushoes tu!.
Unaelewa kwa nini jaaama yenu aliwatimua?
 

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
13,720
2,000
Wacheni kuwaonea tbc matangazo yanarushwa kupitia mtandao wa internet na pale mbagala mawasiliano Ni ya kusuasua tatizo Ni wao cdm kufanyia mkutano vichochoroni,
 

Kiongozi mkuu2020

JF-Expert Member
Aug 8, 2020
1,412
2,000
Choko kweli wewe, yaani ningejua unapatikana wapi ningekupasulia yai KIMA wewe!
Matusi ni ndo Sera ya ilani ya uchaguzi kwenye chama chenu, halafu mnataka waandishi wa habari wenye werediii maalumu kama TBC wawarushe hewaniii.
Ilipobumaa bwana yenu mkubwa kama kawaida yenu kaamua kuporomosha matusi na kuwafukuza waandishiii wetu.

Endeleakutukana maaana ndo ilani yenu ya uchaguzi kwa miaka 5.

Miminiko apa ubungo, njooo mamaaa
 

Danny Jully

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,284
2,000
Waandishi wahabari wanautamaduni wao wakutoa taarifa inayoenda mojakwa moja kwenye jamiiiii. Hivyo sikila tamko au mijadala inayozungunzwa huwa inapelekwa mojakwa moja . hivyo lazima ichujwe kwanzaaa.
Hivyo kinachowagarimu nyie hadi jamaa yenu mkuuu akakasirika vile nikwa sababu mlitaka kila mnalopayuka liende moja kwamoja kwenye uuma wawatuuu.
TBC ni waandishi wahabari mahili wanaozingatia miiko na taratibu za taaluma yao.
Duh...!
Umesoma uzi wote kweli wewe? Au umesoma kichwa cha habari tu!!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom