TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

TBC journalist Jerry Muro held over alleged graft

UMENENA THE PLAYER,Tatizo humu watu wakimpenda mtu huwa hawaamini kwamba anaweza kukosea,Bwana Muro anatuhumiwa kwa utapeli kwanza,polisi wanamchukua kwa ajili ya maelezo then katika hali ya kawaida wanaanzisha uchunguzi wa tuhuma hizo wanagundua Kumbe bwana MURO anamiliki pingu wanatuambia hivyo na kumtaka MURO alete stakabadhi ya ununuzi wa hizo pingu kosa la polisi liko wapi?wataendelea kutujulisha kila wanachogundua kumhusu MURO,Na inasemekana bwana MURO Aliwahi kudai na kupatiwa Tshs.4million kutoka kwa mke wa mmoja wa watuhumiwa wa EPA Akidai mbele ya mama huyo kwamba eti DPP Feleshi kamtuma yeye MURO akachukue fedha hizo kwake ili amsaidie mumewe.Huyo ndio Jerry Muro zaidi ya tunavyomjua.

Nadhani hapa zaidi si suala la kumpenda au kumchukia JM, mnajitahidi kuchambua lakini nimegundua humu ndani hakuna "fair play". Mwenye kucheza rafu rukhsa. Pia timu mchanganyiko golikipa mmoja. kila mtu anataka awe drogba. Humu ndani kuna mahakimu, hafande, maJM, na kila mmoja anataka afunge goli. Cha msingi tuvute subira tu. Unaweza kumtetea JM siku ya mwisho akawa mkosaji utaaibika, au ukamponda sana mwishoni akajaonekana shujaa ukaaibika.
 
Duh! jamaa wafufunguliwa mashtaka matatu 1 kuomba rushwa 2 kula njama 3 kudanganya wao ni maafisa wa takukuru, kila mmoja ametakiwa kutoa zamana ya Tsh milion tano.
 
Duh! jamaa wafufunguliwa mashtaka matatu 1 kuomba rushwa 2 kula njama 3 kudanganya wao ni maafisa wa takukuru, kila mmoja ametakiwa kutoa zamana ya Tsh milion tano.

Aksante tumsam kwa nyongeza wao wametakiwa kutoa shilingi milioni 5 kama dhamana na wadhamini wa 2 kila mmoja kwa kiasi hicho cha milioni 5, mmoja amefanikisha so ataachiwa muda wowote bado Jerry na mwingine (unfortunately majina sikushika)

Hivi kama sikosei Kova si alisema hawa wengine ni matapeli sugu na wana kesi nyingine za kujibu kwa hiyo hawataruhusiwa dhamana au nilisikiliza vibaya?
 
Mtangazaji wa TBC Jerry Muro na watu wengine wawili, Edmund Kapama na Deogratius Ngassa, wamepanda kizimbani mchana huu wakikabiliwa na mashataka kadhaa likiwemo la kula njama kutaka kupokea rushwa.

Mbele ya Hakimu Gabriel Mirumbe, Jerry Muro na washtakiwa hao wawili walishtakiwa kwa pamoja kwa kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 toka kwa mweka hazina wa wilaya ya Bagamoyo aliefukuzwa kazi hivi karibuni na Waziri Mkuu kwa ubadhirifu Bw. Michael Wage.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali Boniface Stancilaus akiwa na Mwendesha Mashtaka toka TAKUKURU Benny Lincolin wamedai mahakamani hapo kwamba mshtakiwa wa kwanza na wa pili pia wanakabiliwa na shtaka la kujipachika wadhifa ambao sio wao.

Inasemekana January 29, 2010 katika hospitali ya Sea Cliff washtakiwa walijitambulisha mbele ya Wage kuwa wao ni maafisa wa Takukuru wakati sio kweli.

Upande wa mashtaka uliiomba mahakama usitoe dhamana hasa kwa washtakiwa wa kwanza na wa pili kwa madai kwamba waliwahi kufungwa huko nyuma na kuwa kwao nje kutaharibu upelelezi ambao haujakamilika na bado unaendelea.

Hakimu alipowataka kutoa uthibitisho kwamba washtakiwa hao waliwahi kufungwa huko nyuma upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha hivyo dhamana ikawa wazi kwa masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wataosaini bondi ya milioni 5 kila mmoja, ama kwenda rumande hadi Februari 12, mwaka huu kesi itaposomwa tena.


Jerry Muro na Edmund Kapama
walitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa.
Ngassa atapelekwa rumande.


Source:
Michuzi​
 
Hakimu alipowataka kutoa uthibitisho kwamba washtakiwa hao waliwahi kufungwa huko nyuma upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha hivyo dhamana ikawa wazi kwa masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wataosaini bondi ya milioni 5 kila mmoja, ama kwenda rumande hadi Februari 12, mwaka huu kesi itaposomwa tena.

Ah polisi wetu jamaniah! Angekuwa ni mtoto unamkana hadharani kwa kweli!1
 
Inasemekana January 29, 2010 katika hospitali ya Sea Cliff washtakiwa walijitambulisha mbele ya Wage kuwa wao ni maafisa wa Takukuru wakati sio kweli.
Source: Michuzi

Kumbe ni Hospital ya Sea Cliff........
 
Kitu kikubwa cha kushangaza ni kwa nini Muro apewe special treatment ya kiasi hiki – kwani swali kubwa ni jee hawezi akawa naye ni tapeli tu kwa kutumia mwanya wa yeye kuonekana “mpiganaji mahiri” wa rushwa?

Wangapi tunao ktk serikali wanaotaka kujitambulisha kuwa ni wapinga ufisadi kumbe ni hypocrites tu – nao wamo? Ndugu zangu, haya yanawezekana sana tu.

Lakini tuangalie kwanza masuala ya msingi. Jee TBC ambako Muro aliko hivi sasa – yaani chombo cha serikali – ina dhamira ya dhati ya kuendesha kwa dhati vita dhidi ya rushwa – rushwa ya wakubwa? Ni kama vile uniambie kuwa Daily News inaweza ikawa mstari wa mbele katika vita ya kupinga ufisadi hasa ufisadi wa wakubwa.

Muro alikuwa ITV na alihama kwenda TBC kwa ushawishi wa wakubwa –akina manji, tanil Somaya na mafisadi papa wengine kwa misingi ya uhamisho wa wale wasanii wa Ze Comedi. Lengo ni kupunguza makali waliyokuwa nayo wakiwa ktk vyombo binafsi, hasa vya IPP ambavyo msimamo wao kuhusu ufisadi wa wakubwa unajulikana.

Ze komedi sasa hivi wamekwisha, wanaigiza rushwa za manesi na matrafiki -- siyo za wakati ule za akina Karamagi wanasaini mkataba wa Buzwagi ktk chumba cha hoteli moja ya London. Siku hizi hawawezi tena kuigiza vitu vya namna hiyo, wamekatwa makali na akina manji aliyewanunua na kuwapeleka TBC. Siku hizi wamebakia kuvaa sidiria na kuandama makarani etc.

Muro naye ni vivyo hivyo, alipelekwa TBC na hao hao mafisadi papa ili asiwe anawagusa, na badala yake awe anawaandama matrafiki na manesi tu.

Kwa hiyo ile dhana ya kusema Muro alikuwa anapambana na mafisadi papa ni dhihaka kubwa.

Na suala la kwa nini polisi, na siyo PCCB, wanalishughulikia suala hili linatokana na matashi ya mlalamikaji, Wage, na bila shaka alikuwa ana sababu zake za kutokwenda kulalamika kwa akina Hosea. Tunajua jinsi Hosea anavyoshughulikia rushwa hasa za wakubwa. Anawalinda sana – ni taasisi ya hovyo kabisa kuhusu grand corruption.

Suala la pingu ndilo linaweza kumponza Muro kama hatalitolea maelezo ya kuridhisha kwa nini alikutwa nazo. Kwa kumtaka atoe risit, polisi wamefanikiwa kum-tie kwamba ni zake – a very important step. Muro angeweza kushikilia siyo zake – aliwekezewa tu na polisi.

Kuna wachangiaji humu ndani, na baadhi ya magazeti wanaona kuwa kwa vile ameonyesha risiti, basi hana kosa! Nashangaa hata MMKJJ katumbukia ktk ushabiki wa wazi wazi wa kumtetea Muro pamoja na kwamba kesi haijaenda mahakamani kwenye maamuzi ya sheria.

Kiuchunguzi wa polisi, Muro anatakiwa atoe maelezo ya pingu hizo, za kazi gani kwake – anatembea nazo ktk gari. Kujilinda? Bastola sawa – kwa ajili ya kujilinda. Lakini pingu? Hivi peke yake Muro anaeweza kumtia pingu mtu kiurahisi? Polisi wamefundishwa namna ya kumtia mtu pingu.

Halafu yeye ni mwanahabari tu, na maadili ya taaluma hiyo yanasisitiza mwandishi kuwa wazi katika kutafuta habari, asijifiche (asiji-conceal) identity yake na wala asitumie silaha ya aina yoyote. Hata hiyo bastola yake, asiitumie kukamua habari, ni ya kujilinda tu anapotishiwa maisha.

Jamani tujaribu kuwa objective. Na kama Muro ni shushushu kama wengine wanavyohisi, basi serikali inayo uwezo wa kusimamisha upelelezi na kuifutilia mbali kesi ili kumlinda. Hawa mashushushu nao hawaaminiki, nasikia walihusika pia ktk ufisadi wa EPA.
======
Ze Malang

I cant thank you enough for being objective.
Inatisha sana na kukatisha tamaa ikiwa crusaders wa kupinga ufisadi wataonekana ni mafisadi. Nimesikia kisa cha Muro/Mke wa Lukaza/DPP Feleshi kikanitisha sana. Huyu anaweza kuwa mzoefu wa kuingia kila penye tundu na kujipatia fedha kirahisi.
 
Jerry Muro na Edmund Kapama
walitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa.
Ngassa atapelekwa rumande.


Mkuu naomba kujuzwa zaidi mshitakiwa wa kwanza na wapili ni Muro na Edmund au Ni Endmund na Ngassa?
 
Hivi kama sikosei Kova si alisema hawa wengine ni matapeli sugu na wanakesi nyingine za kujibu kwa hiyo hawataruhusiwa dhamana au nilisikiliza vibaya?

Kova alisema hatowapa dhamana maana hata wakipewa "dhamana wanaweza kuzitapeli"
 
Naona pingu imekuwa mtaji sasa. Bei bado imebaki ile ile?
 
Back
Top Bottom