Alitega kitendawiliHakutajwa jina ndio maana cjajua ni nani huyo hamnazo ila sasa nshamjua 😂😂😂
Nadhani point ipo hapo kwenye kuchomwa mbigiri za makalioniMbona jibu rahisi Tu, kama Hamnazo alishindwa kudhibiti mbigiri kabla hazijaingia shambani na akaamini kuwa anaweza kuzikanyaga na Maisha yakaendelea, tofauti na matarajio zikamchoma yeye mwenyewe na kusababisha kifo chake, basi TBC wametusaidia kujua kwamba haikuwa umeme WA moyo.
Hv Mwendazake hawez kurudi kweli?Siangalii tbc miaka mingi sasa,ila Hamnazo kwa mujibu wa summary yako ni Mwendazake
Wanafiki sanaWanamkana jamaa yao
Unauliza Meli Bandarini Kurasini Mkuu au?😂😂😂 Kwahy kiburi kimekuja bila kubisha hodi.? Yan kimekuja automatically 😁😁
I reserve my comments !!!Kwa walioangalia taarifa ya habari leo TBC watanielewa.
Kwa kawaida jina au neno hamnazo linamaanisha mtu mjinga, mpumbavu pia asiye na akili timamu.
Leo baada ya taarifa ya habari ya TBC huwa kuna kipindi nadhani cha dakika zisizozidi tano kiitwacho Tafakuri ambacho kinatangazwa na Shaban Kisu na huelezea mambo mbalimbali, sasa leo kipindi kilimuelezea mtu aliyepewa jina la Hamnazo.
Ndugu Hamnazo alikuwa ndani akiwa amevaa msuli bila nguo yoyote ndani yake, akaamua kwenda shambani kwake huku akiwa bila viatu, aliingia ndani ya shamba lake huku akikimbia huku shamba lake limejaa mbigiri (miiba) hivyo mbigiri zile zilimchoma lakini ndugu Hamnazo aliendelea kukimbia kuingia katika shamba lake baada ya kuchomwa sana na zile mbigiri akaamua kukaa chini (tukumbuke alivaa msuli bila nguo yoyote ndani yake) hivyo zile mbigiri ziliendelea kumchoma hata huko makalioni, alilia kwa uchungu bila msaada wowote hivyo ndugu Hamnazo akafariki.
Baada ya sehemu hiyo ya ndugu Hamnazo ikafata sehemu inayoelezea kuwa mbigiri ni sawa na ugonjwa wa corona, shamba ni nchi na huyo ndugu Hamnazo ni kiongozi ambaye hakuchukua hatua kuzibiti mbigiri zilizoota shambani kwake hivyo kupelekea kifo chake.
Mwisho, mtangazaji wa kipindi hicho cha Tafakuri ndugu Shaban Kisu akawashauri watu wajilinde dhidi ya ugonjwa wa corona ili wasife kizembe kama ndugu Hamnazo.
TBC1 hapa walimlenga nani kwa kumuita Hamnazo.?
Ohooooo ! Viongozi wa dini watakutoa utumbo!!!Tumepata jina jingine la kumuita yule mtu.
Hamnazo
Wadau, si jina limekaa poa? Au nyie mwaonaje.
Ntaangalia kwa Millard Ayo mkuuVp boss hata hii semina ya vijana na rais huangalii.?
NANI ANAEPASWA KUSHTAKIWA KATI YA WANAOTUMIA NENO MWENDAZAKE, NA TBC WALIOTUMIA NENO HAMNAZO?Kwa walioangalia taarifa ya habari leo TBC watanielewa.
Kwa kawaida jina au neno hamnazo linamaanisha mtu mjinga, mpumbavu pia asiye na akili timamu.
Leo baada ya taarifa ya habari ya TBC huwa kuna kipindi nadhani cha dakika zisizozidi tano kiitwacho Tafakuri ambacho kinatangazwa na Shaban Kisu na huelezea mambo mbalimbali, sasa leo kipindi kilimuelezea mtu aliyepewa jina la Hamnazo.
Ndugu Hamnazo alikuwa ndani akiwa amevaa msuli bila nguo yoyote ndani yake, akaamua kwenda shambani kwake huku akiwa bila viatu, aliingia ndani ya shamba lake huku akikimbia huku shamba lake limejaa mbigiri (miiba) hivyo mbigiri zile zilimchoma lakini ndugu Hamnazo aliendelea kukimbia kuingia katika shamba lake baada ya kuchomwa sana na zile mbigiri akaamua kukaa chini (tukumbuke alivaa msuli bila nguo yoyote ndani yake) hivyo zile mbigiri ziliendelea kumchoma hata huko makalioni, alilia kwa uchungu bila msaada wowote hivyo ndugu Hamnazo akafariki.
Baada ya sehemu hiyo ya ndugu Hamnazo ikafata sehemu inayoelezea kuwa mbigiri ni sawa na ugonjwa wa corona, shamba ni nchi na huyo ndugu Hamnazo ni kiongozi ambaye hakuchukua hatua kuzibiti mbigiri zilizoota shambani kwake hivyo kupelekea kifo chake.
Mwisho, mtangazaji wa kipindi hicho cha Tafakuri ndugu Shaban Kisu akawashauri watu wajilinde dhidi ya ugonjwa wa corona ili wasife kizembe kama ndugu Hamnazo.
TBC1 hapa walimlenga nani kwa kumuita Hamnazo.?
Kwel mtu ukifa Huna thaman kweli tbc ndio ya kumnanga jitu mwitu msitu
Rest in peace diktekta
Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app