[QUOTE/] Stella Manyanya kanitibua nyongo kwa kumuita Dr Ulimboka Hitler, mbele ya bunge! How cruel![/QUOTE]
Kama kasema hivyo kweli anachefua maana hao wapo wengi wanajipendekeza kwa Kikwete ili asiwaondoe madarakani lakini wanajichimbia shimo wenyewe.
Serikali inafanya ubabe kwasababu viongozi wake hawatibiwi hapa, kitu ambacho ni kibaya tena sana. Huwezi ukatetea sehemu ambayo wewe hufaidiki nayo. Hivi kweli inaingia akilini Nchi nzima hakuna CT Scan na viongozi wetu wakaona ni sawa, basi tuna safari ndefu sana. Shule haziwezi kuboreshwa, public transport pia kwasababu haziwahusu wao kabisa. Tutaendelea kuwasema madaktari lakini viongozi wetu ndio wanatuchimbia kaburi.
Dr. Stephen Ulimboka ni mmoja wa watu wachache duniani na wala sio Tanzania, mimi namfananisha na Steve Biko wa SA. Yeye ameamua kupigania maslahi ya mtanzania wa chini ambaye hawezi kwenda nje ya nchi au hospitali binafsi. Hata madaktari wakiongezwa kima cha chini hicho cha 3.5million yeye hakimhusu kwasababu hafanyi kazi serikalini. Kwanini watu hilo hawalioni? Inavyoonekana pia ni kiungo muhimu mno kwa madaktari kiasi cha kwamba kutokuwepo kwake madaktari wanaanza kuyumba. Mungu amsaidie apone na kurudi salama.
Hii ya Serikali kutaka kuingia mkataba na hospitali binafsi kwa ajili ya wananchi kutibiwa huko ni namna nyingine ya kutafuta ulaji. Ubabe hautasaidia, tunaoumia ni sisi wananchi wa kawaida
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI SEKTA YA AFYA.