TBC aibu tupu

TBC aibu tupu

inabidi tuunde kamati ya kufuatilia kiini cha tatizo kabla ya kuanza kuishambulia TBC kwani tbc imeleta naitaendelea kuleta mageuzi makubwa ndani ya taifa hili,imefanya mengi mazuri tusiyasahau .kosa moja halimfukuzi mke

Tutake radhi tafathali.:smash:
 
Huwezi amini lakini nfo ukweli mda huu taarifa ya habari inasomwa huku kuna nyimbo inapigwa kama vile muvi flani ndo staring anakuja kukomboa mateka walio tekwa.

TV ya taifa ni janga la kitaifa huwezi kujivunia kabisa kuwa nchi ina kituo bora cha tv

Pole sana ndugu, mimi niliacha kuingalia siku nyingi.

Bwana Tido aliondoka na mikakati yake, amewaachia wanasiasa ndio wanaiendesha, ubara wa vipindi si jambo la muhimu tena TBC.

Watu wanajivuna kuitwa wakubwa wamesahau kuwa ukubwa ni kutimiza wajibu.
 
Hivi magazeti yakiwagusa wakubwa hayasomwi. Yakitukana wengine sawa ila wakubwa hayasomwi kabisa. Mkiki kwa nguruwe.............
 
Kuna siku watarusha picha za ngono, najua hazikosi kwenye maktaba yao.

Ushauri, unapoangalia taarifa ya habari na watoto uwe na remote karibu, ili picha za ngono zikianza ubadili fasta.
 
Huwezi amini lakini nfo ukweli mda huu taarifa ya habari inasomwa huku kuna nyimbo inapigwa kama vile muvi flani ndo staring anakuja kukomboa mateka walio tekwa.

TV ya taifa ni janga la kitaifa huwezi kujivunia kabisa kuwa nchi ina kituo bora cha tv

What do you expect tv inapoongozwa na wakurugeni wallowekwa kiaiasA....kwa kuangalia vyeti bila kuwa na ubunifu stahili .......yaani TBC inashuka hadhi kila siku......

Sijui Kama directors waliokuwa kwenye timu ya Tido ..ie susane Mongi Kama nao wapo au waliondoka nae......watangazaji mahiri Kama shabaan kisu ...wamepelekwa kwenye vipindi tofauti na uzoefu wao ili wasisike
 
Huwa naangalia tbc kama channel nyingine hazipatikani, maana wanaficha uhalisia wa habari, wanachakachua mno bila aibu.
 
Huwezi amini lakini nfo ukweli mda huu taarifa ya habari inasomwa huku kuna nyimbo inapigwa kama vile muvi flani ndo staring anakuja kukomboa mateka walio tekwa.

TV ya taifa ni janga la kitaifa huwezi kujivunia kabisa kuwa nchi ina kituo bora cha tv

Watangazaji vihiyo kina Marine Hassan Marine....ni janga la Taifa..
 
Hakika, nami niliyaona madudu hayo TBC, yumkini ni ya kibinadamu, lakini nimesikitishwa kwa watangazaji wa TBC kushindwa kutuomba radhi watazamaji. Wana nafasi ya kufanya hivyo hata kesho, kama kweli wanatuheshimu.

Maggid Mjengwa,
Iringa.
unaijua kesho wewe??wasaidie leo leo kesho tusipokuona tumpe shemeji pole
 
Sisi tunaofuatilia na kujua nini kiini cha Tatizo hatuoni haja ya kuunda kamati Teule! Maana ni sawa na kuzuia Mvua kunyesha wakati huna Mamlaka yaho hata kidogo!.

Televisheni ya Taifa ( TVT) ilipokuwa inafanya kazi watanzania wengi walikuwa hawajaipa kibali kabisa maana ilikuwa ni Ujima zama za 1880 kwani hakukuwa na matokeo yaliyoleta mabadiliko!.

Wakati huo ilikuwa ni ndoto tena aghalab kumkuta kijana akiangalia vipindi vinavyohusu Taifa letu kwani hakukuwa na sababu ya msingi ya Kuvutia kwa Vipindi husika.

Rais Jakaya Kikwete alipoingia madarakani 2005 kwa haraka sana aliona ni vema kukafanyika Mabadiliko makubwa kwa TVT, mwanzo kabisa TIDO MHANDO akatolewa BBC SWAHILI akiwa Mkurugenzi na alipofika Tanzania kwa mara ya kwanza alitoa kauli ambayo kwetu tulio wengi tuliona ni Uongo sana namnukuu (wengi wataipenda na kuiangalia Televisheni ya Taifa) na Baada ya yeye kukabidhiwa Televisheni hii taratibu mabadiliko yakaanza na ghafla watazamaji wengi wakabadili mawazo na kuanza kuingalia.

Ni TIDO MHANDO ndiye aliyefanya yote haya na hakuna ubishi wala Siasa, ikumbukwe tayari TIDO alikuwa yuko katika viwango vya kimataifa hivyo mengi aliyafanya kwa kwa viwango hivyo sisi sote ni mashahidi kwani baada ya Mabadiliko kutoka TVT kwenda TBC kukatokea mabadiliko makubwa ambayo yalileta Hofu kwa Vituo vyote vya Luninga hapa Nchini, na hii yote ilikuwa kazi ya TIDO.

Toka hapo Tanzania ikawa na Kituo Bora cha Televisheni, ikumbuke Bungeni baadaye TIDO aliruhusu Kusulubiwa kwa Lowasa na Mawaziri wake TBC 1 huku kila Mtanzania akiangalia hali ilivyokuwa siku hiyo!.

Hapo watanzania wakaongeza imani kwa TBC 1 maana kila kitu kikawa Hadharani huku vipindi vyake vikiwa ni Bora na vya kuvutia.

Mahusiano ya TIDO na Serikali yalianza kulegalega baada ya Kuingia katika Makubaliano ya Kurusha Kipindi cha Mchakato Majimboni huku wagombea CCM 2010 wakionekana kupwaya kwa Majibu na Sera zao kwa wananchi kwani hapo ndipo CCM waliposurubiwa na TBC 1 maana hakuna asiyejua kama CCM yetu kwa wakati ule ilihiitaji Mtu wa kuwafariji na sio kuwapa Haki iliyostahili.

Aidha ikumbukwe ni Kipindi hiko ambacho aliyekuwa KATIBU MKUU CCM TAIFA - YUSUPH MAKAMBA alilalamika kwa Kipindi cha Mchakato Majimboni kuwa kilikuwa kinawakandamiza Wagombea wa CCM na hatimaye wakajitoa katika kipindi hicho.

TIDO aliendelea na Msimamo wake wa kutoa Haki kwa Wagombea wote na Hatimaye Kura za Urais zilipotangazwa Kikwete alionekana kutokubalika sana kama 2005 alivyoshinda ushindi wa Kimbunga, hapa ndio mwanzo wa Mahusiano ya TIDO na Kikwete yalipoanza.

Kiofisi TIDO alikuwa Hana tatizo na Mtu kwani alijuwa kuwa Kazi nzuri na malipo mazuri sasa Mtihani uliopo sasa je KIONDO MSHANA anaweza kuvaa Viatu alivyoacha TIDO na kutembelea!!! Maana Himaya ya Mfalme Kikwete imebomoka nayo iko wazi tena kweupe na kila Mtu na lake ndani yake!

Hivyo kwa yote yanayotokea ni Matokeo ya Ufalme wake kubomoka! Yatatokea mengi zaidi ya Haya maana Mfalme nguvu zake zimegawanywa na aliowapa utawala wake yeye angali akiwa kwenye Kiti.
 
Huwezi amini lakini nfo ukweli mda huu taarifa ya habari inasomwa huku kuna nyimbo inapigwa kama vile muvi flani ndo staring anakuja kukomboa mateka walio tekwa.

TV ya taifa ni janga la kitaifa huwezi kujivunia kabisa kuwa nchi ina kituo bora cha tv

NDO WANAJIAANDAA KUINGIA MFUMO WA DIGITALI ..mMMMMH
 
inabidi tuunde kamati ya kufuatilia kiini cha tatizo kabla ya kuanza kuishambulia TBC kwani tbc imeleta naitaendelea kuleta mageuzi makubwa ndani ya taifa hili,imefanya mengi mazuri tusiyasahau .kosa moja halimfukuzi mke

Tuongee kwa takwimu TBC imefanya yapi zaidi ya kuwa kibaraka wa CCM? Only wakati wa Tido tu afadhali kidogo
 
Huwezi amini lakini nfo ukweli mda huu taarifa ya habari inasomwa huku kuna nyimbo inapigwa kama vile muvi flani ndo staring anakuja kukomboa mateka walio tekwa.

TV ya taifa ni janga la kitaifa huwezi kujivunia kabisa kuwa nchi ina kituo bora cha tv

Kibaya zaidi:Watangazaji wala hawakujali kuwaomba radhi watazamaji pamoja na kasoro hiyo iliyojitokeza!
 
Nasikitishwa sana na mmabo yanayo tokea kwenye TV ya Taifa, hapa tanzania wajua niaibu sana mambo haya kutokea, but sipati shaka yote haya yanaletwa na tabia za kupeana kazi kijomba,kirafiki,uchumba,mke na mambo kama hayo, kwani na imani ingikuwa si hivyo tusinge weza kuona uzembe huu unaendelea kutokea kila mara mpaka imekuwa kawaida ni kama mazoea. Maoni yangu ni kwanini haya haya tokee kwenye tv za watu binafsi jibu ni moja tuu watu huwajibishwa kwa ujinga uliofanyika, i hope uongozi wa TV ya taifa ujifunze hili toka sekta binafsi.
 
nI KWA SABABU SIKU HIZI SIYO TELEVISHENI YA TAIFA ILA SASA IVI NI TBCCM,
 
Kumbe campeni za cdm wanazirusha kwa mafungu kuepusha rawama star tv wao wamezitoa wapi?
 
Back
Top Bottom