Tb Joshua alivyonipa utajiri

Tb Joshua alivyonipa utajiri

Kama utakumbuka, miezi miwili iliyopita nilikuja na post juu ya kutoa shukrani kwa Yesu kwa kumtumia mtumishi wa Mungu TB Joshua kuniponya tatizo langu la uvimbe sehemu za siri ambalo lilikuwa likinifanya kushindwa kusimamisha uume wangu kwa miaka zaidi ya 4. Uponyaji wa tatizo langu ulifanyika kupitia maji maarufu ya ANOINTING WATER yanayoandaliwa na kutolewa na TB JOSHUA MINISTRIES.

Leo nataka nikushirikishe juu ya jinsi maji hayo yalivyonipa FUSSO 2, COASTER 3, NYUMBA 2, na RESTAURANT 3.

Nilianza biashara yangu miezi 4 iliyopita. Kalikuwa ni kamgahawa kadogo tu lakini kwasababu niliamini kwenye nguvu iliyomo ndani ya Yesu, sikuwa na hofu yoyote kuwa mafanikio yanakuja.

Kabla ya hapo, nilisikia shuhuda za watu mbaimbali ambao walitajirika baada yakutumia ANOINTING WATER kwa imani. Nikaamua kuyatumia haya maji kwenye biashara yangu kwa imani kubwa. Nilichokifanya ni kupuliza haya maji kwenye milango na makabati ya chakula huku nikiamrisha wateja wafurike kwenye biashara yangu kwa jina la Yesu.

Huwezi kuamini, mauzo yalibadilika kutoka shs laki 2 kwa siku hadi milioni 2. Watu wanajaa kwenye restaurant hadi nikaamua kuweka viti na meza eneo la jikoni na bafuni. Wateja wako radhi hata kula huku wamesimama au wamechuchumaa. Inapofika muda wakufunga huwa inabidi niwafukuze wateja vinginevyo tunaweza kukesha.

Ndani ya miezi 3, nimejenga nyumba 2, nimenunua coaster 3, fusso 2 na niko mbioni kufungua restaurant nyingine 2.

ASANTE YESU. ASANTE TB JOSHUA
Itabidi na mimi niende kwa Mchungaji TB JOSHUA anipe hayo maji ya (ANOINTING WATER) Nije niwatibu watu humu Jami forums ili wapone hahahah. Kumbuka Bwana YESU alivyosema ninanukuu. ( Luka 18:24-25 ) "Kwa maana ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu".
 
Innocent Chacha

Hayo ni ya kweli? Nawezaje kuthibitisha kuwa miezi minne iliyopita ulikuwa huna kitu na sasa una utajiri kiasi hicho?
 
1. Kuuza milioni 2 kwa siku kwa bei ya chakula cha mgahawani ina maana umeuza pieces 1000 kwa wastani. Mgahawa kuhudumia watu 1000 kwa siku ni "miujiza"

2. Kuuza milioni 2 kwa siku, kwa biashara ya chakula faida haitazidi milioni moja ukiondoa gharama zote. Kwa miezi mitatu ina maana ulipata faida ya milioni 90. Coaster 1 ni sh milioni 40, so coaster 3 ni milioni 120. Fuso moja ni milioni 40 so fuso 3 ni miloni 90. Jumla ni milioni 210. Nyumba moja ya wastani ni milioni 30, so nyumba 2 ni milioni 60. Jumla yote ni milioni 270.

Kapange uongo wako vizuri...

siku zote miujiza huonekana kama uongo fulani vile. Kwahiyo sikushangai hata kidogp
 
Innocent Chacha

Hayo ni ya kweli? Nawezaje kuthibitisha kuwa miezi minne iliyopita ulikuwa huna kitu na sasa una utajiri kiasi hicho?

Mambo ya Mungu huwa hayahitaji uthibitisho. Unachotakiwa kufanya ni kuamini tu
 
Ushahidi wako ujakamilika mr chacha.hebu tueleze hiyo restaurant ako inaitwaje??kwa faida hiyo hata serena hotel hawana hiyo faida..mimi ni tomaso nahitaji uthibiti....sho wa macho.

Atwambie hiyo restaurant iko wapi,na yeye yuko wapi tuthibitishe. Nimetafakari hiyo turnover yake kwa miezi 4 nimeshndwa kupata jibu.

Hii ni marketing strategy,huyu dogo aliingizwa cha kike akanunua hiyo mimaji sasa imekosa soko anaitangaza,anataka tumuulize yanapatikana wapi ili akatuuzie.

Mura INNOCENT CHACHA acha uongo mura!. Tafta njia nyingine ya kudanganya ila hayo maji yaiyooshewa maiti hunishawishi ninunue.
 
Last edited by a moderator:
Atwambie hiyo restaurant iko wapi,na yeye yuko wapi tuthibitishe. Nimetafakari hiyo turnover yake kwa miezi 4 nimeshndwa kupata jibu.

Hii ni marketing strategy,huyu dogo aliingizwa cha kike akanunua hiyo mimaji sasa imekosa soko anaitangaza,anataka tumuulize yanapatikana wapi ili akatuuzie.

Mura INNOCENT CHACHA acha uongo mura!. Tafta njia nyingine ya kudanganya ila hayo maji yaiyooshewa maiti hunishawishi ninunue.


Hata YESU wayahudi walimuona kuwa ni muongo
 
Last edited by a moderator:
milion 2 ndani ya miezi 3 ni milioni 180 (2 mara 90 = 180)! Inawezekana vipi kwa milion 180 uweze kununua fuso 2, coasta 3 pia ujenge nyumba 2, restraurant 3? Innocent chacha hebu fafanua vizuri.

Hapo ujaweka jumapili ambazo hafanyi kazi,pia ujaingiza gharama za uendeshaji ikiwa pamoja na kodi,mishahara kwa staff ununuzi wa vifaa na ukarabati wa sehemu za kulia KUBWA KULIKO YOTE ETI WATU WANALIA MPAKA CHOONI

DAH KWELI HII NI BIASHARA LIVE
 
Last edited by a moderator:
Alifufuka mkuu ndio maana tunaamini la sivyo ukristo usingekuwepo, na kuhusu kufa msalabani ilikuwa lazima afe ili alipe deni la dhambi zetu ndio maana hakujiokoa. Ila kuna wajanja wachache wanatumia vibaya neema tuliyopewa bure.

Matayo 24 45-46 eloi eloi lamasabakhtani mungu Wang mungu mbona unaniacha ????sasa km yeye alikuwa kafara ili same he we dhambi kwanini alalamike kuwa mungu kamuacha???mbona Hanna logic
 
hahahaa we jamaa kiboko kwa hiyo restaurant yako ina meza hadi bafuni?!

Basi sawa.
 
Mimi ninachoamini ni kwamba, mafanikio yanapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na malengo. Priority ya Yesu sio kuwatajirisha wafuasi wake duniani, ila hiyo inakuja kama bakhshishi tu, ndio maana alisema utafuteni kwanza ufalme wake na hayo yote mtazidishiwa.
La pili lunalonipa shaka ni matumizi ya Anointed water. Kwa jina la Yesu halitoshi hadi ununue maji kutoka Nigeria? Huku ni kumshusha hadhi Mungu ambaye sifa yake ni kuwa mahali popote kwa wakati wote.
Unless hiyo ni business strategy.

Kula LIKE mkuu
 
Samahani mkuu, naona sijakuelewa vizuri; ulipewa 'anointing water' au 'damu halisi ya Yesu'? Na hiyo kutoka laki mbili hadi milioni mbili na mali zote ulizotaja ndani ya miezi minne haina uhusiano na chuma ulete kweli mkuu?

Hapa hapa JF wapo wafuasi wazuri tu wa Yesu, na mambo yangekuwa kihivyo wangekuwa mbali. Hebu tusubiri hoja zaidi toka kwa wadau.

Mkuu, kwa tunaojua neno la Mungu kwa kiasi chake tunajua Mungu ni mwenye utaratibu. Ana taratibu zake na wakati wake wa kufanya mambo. Si kwa upuuzi wa huyu mleta mada.

Cha msingi angeamisha post yake na kupeleka jukwaa la matangazo kama anauza anointing water, angepata wa kuwapata.
 
tobaaaa,kama ni damu ya yesu ingeitwa blood of jesus,ushasema alikupa maji yaitwayo anointing water. acha kujiuma uma huo ni ushirikina.

yesu alikufa msalabani miaka takriban 2000 iliyopita,leo umegaiwa damu yake inform of water.

Haya nayo yapaswa kuwa kivutio cha utalii tz
mwenzako ndicho anachoamini na matokeo yake ndo kama alivyosema. wewe kama huamini uchape tu lapa maana unapingana na ukweli ambao umedhihirika kwake. nyie watu wa jf mna matatizo na mnapenda kufuata mkumbo unacoment kwa kuangalia kwanza mwenzako kasmamia wapi. Angetoa post ya kumponda TBJ mngemuunga mkono asilimia zote. ila hapa huwezi kujua alikuwa amewekeza kiasi gani na akaja kuongeza kiasi gani wewe unakataa tu as if unamfahamu.
 
Lisilowezekana kwa wanadamu linawezekana kwa mungu, kama yesu mwenyewe alibadilisha maji kuwa divai tamu, na akasema mtafanya mambo makubwa kuliko haya kwa kuwa mimi naenda kwa baba, je haistahili aliyeamini kufanya haya? Mfungule fahamu zenu kwa jina la yesu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom