Tb Joshua alivyonipa utajiri

Tb Joshua alivyonipa utajiri

Sorry kwa kukuita akili mgando unayewaza kwa kutumia pua,ubongo huko tumboni,usipende kuchanganya mambo.ya mbowe ni full na vyombo vya kazi.ie speaker,generator nk.

Umeshalewa? maana ulichokiandika unakielewa mwenyewe, punguani wahed.
 
Jamani imani ni ugonjwa,kama ameamini kweli kafanikiwa tumpongeze.
 
acheni ujinga TB.J ni mtumishi wa MUNGU think big peoples but kwa habari ya anoiting water siyaamini kabisa coz kuna mtu alipewa hakupona but alienda NGURUMO YA UPAKO akapona saa ile ile na ilitokea infront of my own eyes

Imani yako ndio itakuponya,si vinginevyo.Unamkumbuka babu wa loliondo?kunawatu walipona.
 
biblia imeandika kwa jasho lako utakula. ila siku hizi hamtaki jasho mnataka miujiza. kuna miujiza Yesu alifanya ila sikumbuki ya kutajirishana. samahani lakini ni mtazamo tu
 
Kama utakumbuka, miezi miwili iliyopita nilikuja na post juu ya kutoa shukrani kwa Yesu kwa kumtumia mtumishi wa Mungu TB Joshua kuniponya tatizo langu la uvimbe sehemu za siri ambalo lilikuwa likinifanya kushindwa kusimamisha uume wangu kwa miaka zaidi ya 4. Uponyaji wa tatizo langu ulifanyika kupitia maji maarufu ya ANOINTING WATER yanayoandaliwa na kutolewa na TB JOSHUA MINISTRIES.

Leo nataka nikushirikishe juu ya jinsi maji hayo yalivyonipa FUSSO 2, COASTER 3, NYUMBA 2, na RESTAURANT 3.

Nilianza biashara yangu miezi 4 iliyopita. Kalikuwa ni kamgahawa kadogo tu lakini kwasababu niliamini kwenye nguvu iliyomo ndani ya Yesu, sikuwa na hofu yoyote kuwa mafanikio yanakuja.

Kabla ya hapo, nilisikia shuhuda za watu mbaimbali ambao walitajirika baada yakutumia ANOINTING WATER kwa imani. Nikaamua kuyatumia haya maji kwenye biashara yangu kwa imani kubwa. Nilichokifanya ni kupuliza haya maji kwenye milango na makabati ya chakula huku nikiamrisha wateja wafurike kwenye biashara yangu kwa jina la Yesu.

Huwezi kuamini, mauzo yalibadilika kutoka shs laki 2 kwa siku hadi milioni 2. Watu wanajaa kwenye restaurant hadi nikaamua kuweka viti na meza eneo la jikoni na bafuni. Wateja wako radhi hata kula huku wamesimama au wamechuchumaa. Inapofika muda wakufunga huwa inabidi niwafukuze wateja vinginevyo tunaweza kukesha.

Ndani ya miezi 3, nimejenga nyumba 2, nimenunua coaster 3, fusso 2 na niko mbioni kufungua restaurant nyingine 2.

ASANTE YESU. ASANTE TB JOSHUA

1. Wanafizikia tunajua kuwa ukirusha jiwe juu, speed lilioondokea ndio speed litakaloshuka nayo. Jiandae kurudi umaskinini kwa speed hi yo hi yo.

2. Hao wateja wanaojaa be careful, yawed a kuwa kiinimacho.

OMBI: acha kuweka Imani Yako kwa mtu. Ole wake amtegemeaye mwanadamu
 
Imani yako ndio itakuponya,si vinginevyo.Unamkumbuka babu wa loliondo?kunawatu walipona.

kati ya orijino na feki kipi kinadumu?
kama ni orijino, je kati ya babu na ngurumo nani ni orijino?
mimi nitajibu ngurumo coz ameanza zamani mwaka wa 2000 na sasa bado yupo.
babu alikua nifeki coz alivuma akanyamaza lakini ngurumo ni orijino coz alidumu mpaka sasa !
 
Ndugu we unapatikana wapi ? Ili tuweze kuthibitisha huo utajiri ulioupata kwani sikuhizi binadamu wamekuwa na mambo mengi sana
 
jambo moja ninajua mmepewa bure toeni bure. uponyaji ni karama toka kwa Mungu na alitoa bure kwa kazi yake ya msalabani. sasa iweje leo karama ya uponyaji iuzwee. nawewe mwenye ushuhuda wa kununua mafuso, coasta, kujenga nyumba mbili umekwisha tafuta kwanza ufalme wa mbinguni? chanzo cha mafanikio ya mwilini kwenye ulimwengu wa roho sio lazima ziwe ni nguvu za Mungu. hili linajulikana. Gamalieli mwalimu wa dini wa kiyahudi wakati Mafarisayo walipotaka kuwaua akina Petrol alisema hivi msiwaue waacheni maana ikiwa kazi hii ni ya Mungu itadumu na ikiwa siyo ya Mungu itakufa tuu. Kwa ufupi alisema time will tell. jambo la msingi kwa nyakati hizi wale walioamua kumfuata Kristo kwa dhati wawe makini maana wapo wavaao nguzi za kondoo kumbe ni umbwa mwitu wakali. tusifurahie miujuza na utajiri bali tufurahi kwakuwa majina yetu yameandikwa kwenye Ufalme wa Mungu. Just few word.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom