Tb Joshua alivyonipa utajiri

Tb Joshua alivyonipa utajiri

Shauri zako,
Kutoka laki mbili kwenda milion mbili kwa siku ni maajabu; hata zingekuwa zile hotel za kimataifa siyo hivyo.

Hizo hela ndugu yangu jiangalie mara mbili mbili, kuna siku watakuambia tunataka sadaka, kaa vizuri na mkeo/mume na watoto wako.

Usifurahie pesa za mapepo, hayo maji yangekuwa na huo uwezo akina martha kaaya wanaoyauza si wangekuwa mbali sana kimaendeleo?
Mamndenyi, huyu matha kaaya unaenzungumzia ni yupi?
 
Last edited by a moderator:
tukiachana na mambo ya maji na damu na yesu
turudi kwenye financial accounting au financial management au investment analysis au hisabati rahisi tu,
kwanza nakunukuu "Ndani ya miezi 3, nimejenga nyumba 2, nimenunua coaster 3, fusso 2 na niko mbioni kufungua restaurant nyingine 2" jambo hilo haliwezekani.

tuchukulie hio milioni mbili unayopata yote ni faida tupu kwa miezi mitatu (90 x 2 = 180) milioni. hivyo vyote umefanya kwa mil 180? haiwezekani. tafuta uongo mwingine.

Amejenga nyumba mbili za makuti,kibajaji used,na anategemea kununua bajaji used ingine,labda hiyo bjet inaruhusu lakini si fuso
 
Ndugu yangu endelea kumwamini mungu kwa kuwa Yesu wetu yu hai naanatenda kazi kupitia watumishi wake kama TB Joshua na wengine waliotiwa mafuta
Humlazimishi kuami
 
sijasema haya yote nimeyafanya usiku wa kuamkia leo. Unapopigia mahesabu mapato ya restaurant peke yake sijui una maana gani. Hizo coaster na fusso zimefungiwa chumbani?

Toka na hayo maji yako. Kawaogeshe wenye akili na wasiomjua Mungu kama wewe.
 
milion 2 ndani ya miezi 3 ni milioni 180 (2 mara 90 = 180)! Inawezekana vipi kwa milion 180 uweze kununua fuso 2, coasta 3 pia ujenge nyumba 2, restraurant 3? Innocent chacha hebu fafanua vizuri.
Mkuu bange mbaya aisee muache huyo jamaa anaota!!Na kama alikua anaweza kuzalisha 200000 kwa siku Dar huyo ni tajiri
 
Last edited by a moderator:
Alifufuka mkuu ndio maana tunaamini la sivyo ukristo usingekuwepo, na kuhusu kufa msalabani ilikuwa lazima afe ili alipe deni la dhambi zetu ndio maana hakujiokoa. Ila kuna wajanja wachache wanatumia vibaya neema tuliyopewa bure.

Hahaha daah"!!

Never underestimate the power of Imaan:::

Mkuu, kabisaaa???
 
milion 2 ndani ya miezi 3 ni milioni 180 (2 mara 90 = 180)! Inawezekana vipi kwa milion 180 uweze kununua fuso 2, coasta 3 pia ujenge nyumba 2, restraurant 3? Innocent chacha hebu fafanua vizuri.
Ila kuna sehemu kaeleza baada ya mda restaurant yake ilikua na akafikia kuingiza million 2 kwa siku,piga million mbili kila siku mara miezi 3,hehhe
Dah kama faida kubwa mno sijui itawezekanaje.
 
Last edited by a moderator:
milion 2 ndani ya miezi 3 ni milioni 180 (2 mara 90 = 180)! Inawezekana vipi kwa milion 180 uweze kununua fuso 2, coasta 3 pia ujenge nyumba 2, restraurant 3? Innocent chacha hebu fafanua vizuri.

siongei kuhusu yeye,mi naongelea mahesabu tu! Vipi kama faida inakuza mtaji?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hizo restaurant zako hapa bongo zipo maeneo gani inawezekana tushafika hapo,hebu piga picha za hizo restaurants zako utuwekee hapa tuhakikishe muujiza huo ili tuondoe huu u-Tomaso wetu
 
Kama utakumbuka, miezi miwili iliyopita nilikuja na post juu ya kutoa shukrani kwa Yesu kwa kumtumia mtumishi wa Mungu TB Joshua kuniponya tatizo langu la uvimbe sehemu za siri ambalo lilikuwa likinifanya kushindwa kusimamisha uume wangu kwa miaka zaidi ya 4. Uponyaji wa tatizo langu ulifanyika kupitia maji maarufu ya ANOINTING WATER yanayoandaliwa na kutolewa na TB JOSHUA MINISTRIES.

Leo nataka nikushirikishe juu ya jinsi maji hayo yalivyonipa FUSSO 2, COASTER 3, NYUMBA 2, na RESTAURANT 3.

Nilianza biashara yangu miezi 4 iliyopita. Kalikuwa ni kamgahawa kadogo tu lakini kwasababu niliamini kwenye nguvu iliyomo ndani ya Yesu, sikuwa na hofu yoyote kuwa mafanikio yanakuja.

Kabla ya hapo, nilisikia shuhuda za watu mbaimbali ambao walitajirika baada yakutumia ANOINTING WATER kwa imani. Nikaamua kuyatumia haya maji kwenye biashara yangu kwa imani kubwa. Nilichokifanya ni kupuliza haya maji kwenye milango na makabati ya chakula huku nikiamrisha wateja wafurike kwenye biashara yangu kwa jina la Yesu.

Huwezi kuamini, mauzo yalibadilika kutoka shs laki 2 kwa siku hadi milioni 2. Watu wanajaa kwenye restaurant hadi nikaamua kuweka viti na meza eneo la jikoni na bafuni. Wateja wako radhi hata kula huku wamesimama au wamechuchumaa. Inapofika muda wakufunga huwa inabidi niwafukuze wateja vinginevyo tunaweza kukesha.

Ndani ya miezi 3, nimejenga nyumba 2, nimenunua coaster 3, fusso 2 na niko mbioni kufungua restaurant nyingine 2.

ASANTE YESU. ASANTE TB JOSHUA

Mimi ninachoamini ni kwamba, mafanikio yanapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na malengo. Priority ya Yesu sio kuwatajirisha wafuasi wake duniani, ila hiyo inakuja kama bakhshishi tu, ndio maana alisema utafuteni kwanza ufalme wake na hayo yote mtazidishiwa.
La pili lunalonipa shaka ni matumizi ya Anointed water. Kwa jina la Yesu halitoshi hadi ununue maji kutoka Nigeria? Huku ni kumshusha hadhi Mungu ambaye sifa yake ni kuwa mahali popote kwa wakati wote.
Unless hiyo ni business strategy.
 
TB JOSHUA ni mtumishi wa Mungu. Anointing water ni damu halisi ya YESU

Samahani mkuu, naona sijakuelewa vizuri; ulipewa 'anointing water' au 'damu halisi ya Yesu'? Na hiyo kutoka laki mbili hadi milioni mbili na mali zote ulizotaja ndani ya miezi minne haina uhusiano na chuma ulete kweli mkuu?

Hapa hapa JF wapo wafuasi wazuri tu wa Yesu, na mambo yangekuwa kihivyo wangekuwa mbali. Hebu tusubiri hoja zaidi toka kwa wadau.
 
kuwa mfuasi mzuri wa Yesu haimaanishi kuwa mambo yako yatakuwa mazuri
 
Mimi ninachoamini ni kwamba, mafanikio yanapatikana kwa kufanya kazi kwa bidii na malengo. Priority ya Yesu sio kuwatajirisha wafuasi wake duniani, ila hiyo inakuja kama bakhshishi tu, ndio maana alisema utafuteni kwanza ufalme wake na hayo yote mtazidishiwa.
La pili lunalonipa shaka ni matumizi ya Anointed water. Kwa jina la Yesu halitoshi hadi ununue maji kutoka Nigeria? Huku ni kumshusha hadhi Mungu ambaye sifa yake ni kuwa mahali popote kwa wakati wote.
Unless hiyo ni business strategy.

Nakuhakikishia kuwa Mungu anapenda sana tuwe matajiri kuliko vile tunavyodhania. Kuhusu kutumia anointing water, hata YESU mwenyewe altumia tope kuponya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom