TB Joshu atabiri tena

TBJ ni mjanja sana. Yaani tabiri zake zote huwa anahakikisha ameacha mahala pa kutokea endapo utabiri hautotimia! Katika hili utabiri usipotimia atasema hamkuomba saana!
 
Nami namtabiria TB Joshua kuwa hivi karibuni yatamkuta makubwa na ataumbuka vibaya. Siyo mara yangu ya kwanza kutabiri. Nilimtabiria shehe Yahaya Hussein kuwa atarudisha namba na akarudisha kweli. Hivyo mshaurini asome utabiri wangu na aache utapeli yana mwisho.
 

Kwa tafsiri yangu..anaposema Chelsea inahitaji maombi zaidi kuliko Bayern mana'ke Bayern ina nafasi kubwa zaidi ya kushinda ukilinganisha na Chelsea,na ni maombi ya nguvu ndo yanayoweza kuja kuwapa matokeo mazuli Chelsea,kwahiyo acheni kupotosha watu kuwa eti ametabiri direct kuwa Chelsea watashinda
 
Anatafuta matusi kwa wapenda kabumbu kama mimi ambaye katu sikubaliani na utabiri wa matokeo kabla gozi halijapigwa uwanjani!
 
www.facebook.com/TBJoshuaMinistries

jamani emu chekini hiyo link hapo,
hizo taarifa si za kweli, na wamekanusha kabisa kwamba ni rumous.
Anayetaka ukweli acheki hapo.
 

HUYU JAMAA MKALI!! YAANI KESHAONESHWA KIPINDI CHA KWANZA NDOTONI!! HAHAHAHA! AISEEEE!!! :wacko:
 
HUYU JAMAA MKALI!! YAANI KESHAONESHWA KIPINDI CHA KWANZA NDOTONI!! HAHAHAHA! AISEEEE!!! :wacko:

Ni utapeli tu mkuu. T.B hana lolote zaidi ya kucheza na akili za watu. We tangu lini mungu akatabiri mambo ya soka? Atabiri basi na netbal, cricket, rugby, mieleka, boxing n.k. Watu wanamtania mungu tu na joshua ni tapeli
 
Jamani mimi nilimskia kwa maskio yangu alichosema ni kwamba chelsea wanahitaji maombi basi si zaidi ya hapo,mengine yote yanayosemwa ni uongo mnamsingizia kabisa
 
Soccer is all about making better use of one's chances and taking advantage of opponent's mistakes to the full...TB Joshua's voodoo is of no relevance whatsoever.

*And that tall guy that he is referring to might be Jerome Boateng*
 
Joshua mwizi tu. Hana unabii wowote, utapeli mtupu.

sssssshhhhhhhhhhhhhhhhhhh, taratibu wafuasi wake wasikusikie, usijesukumwa ukitoka kuoga ukapata mtikisiko wa ubongo.
 
Nabii ni sauti au ujumbe wa Mungu kwa watu wake.

Je Mungu ameanza kujishughulisha masuala ya mpira????
 
Soccer is all about making better use of one's chances and taking advantage of opponent's mistakes to the full...TB Joshua's voodoo is of no relevance whatsoever.

*And that tall guy that he is referring to might be Jerome Boateng*

Yes, given that Gustavo and Alaba will miss the final, Boateng is the only dark-skinned player remaining. Lets wait and see.
 
Mimi natabiri chelsea ni mabingwa, halafu tuone kati ya Mungu wake na Wangu yupi mkweli..mark my words na tukutane jumapili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…