Uozo, blabla na upendeleo wa wazi wazidi kuishushia hadhi Ballon d’Or

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Niliwahi kusema na kamwe sijawahi kufumba mdomo na kuacha kusema kuwa tuzo za Ballon d’Or ni tuzo za kipuuzi na kipumbavu kuwahi kutokea kwa miaka ya karibuni katika Ulimwengu wa Soka.

Tuzo hizi kwa miaka ya mwishoni mwa 2000 hadi sasa zimekuwa zikitawaliwa na skendo nyingi huku kwa nyakati tofauti zimekuwa zikionesha upendeleo wa waziwazi kwa mshindi.

Na kwa miaka ya karibuni pia tulishuhudia FIFA kuachana nazo, hivyo kutoka kuitwa FIFA Ballon d’Or zikabaki tu kuitwa Ballon d’Or na makocha na manahodha wakawa hawana haki tena ya kupiga kura badala yake Ballon d’Or wapiga kura ni waandishi wa habari ambao mifano yao tunayo hata hapa kwetu.

Waandaaji wa tuzo hizi wamekubali kushikiwa akili na makampuni makubwa mawili yanaodhamini Vilabu na hata wachezaji, wote mnayajuwa sina haja ya kuyataja.

Jarida la France Football linalotoa tuzo hizo nalo limejiweka uchi wa mnyama huku likishindwa kutolea majibu maswali magumu wanayo ulizwa kila mwaka wanapo mtangaza mshindi wa tuzo hizi.

Upande wa Pili kwenye tuzo za FIFA Men Player of the Year wenyewe wapo safi na salama. Tuzo zao ni safi na washindi wao ni wale wanaostahili na sio blabla za wenzao wa Ballon d’Or.

Blabla za Ballon zilianzia pale kwa kiungo wa Inter na timu ya Taifa ya Uholanzi Wesley Sneijder ambae aliisaidia timu yake kubeba mataji lukuki yakiwemo ya Champions League, Scudetto, Coppa Italia na FIFA Club World Cup, lakini mwisho wa yote tuzo akapewa Mtu mwingine kwa vigezo kuwa wamempa huyo Mtu wao kwa kigezo cha kufunga magoli mengi.

Watu tukahoji bila kupatiwa majibu ya kwamba kwanini tuzo zilizopita alipewa Mtu kwa kuwa alishinda mataji mengi na kuachwa yule mwenye magoli mengi?

Hapakuwa na majibu ya kueleweka zaidi ya blabla tu na baada ya hapo Watu wengi wa Soka walitoa kauli kali na za kuiponda tuzo hio inayozidi kupoteza wapenzi Siku hadi Siku. Baadhi ya wachezaji walishakataa mialiko ya kwenda kwenye tuzo hio baada ya ujambazi huo wa wazi wazi.

Miaka kadhaa iliofuata wale jamaa wawili tena wakawa hawana lolote kumzidi Frank Ribery lakini cha kushangaza mwisho wa Siku akateuliwa mmoja wapo na kupewa tuzo hio huku Ribery akiondoka mikono mitupu.

Baada ya maswali kuwa mengi ikabidi France Football waseme kuwa eti sadari hii waliwaachia wapiga kura waamue na hawakutaka kuangalia vile vigezo vyao.

Lakini hali ikazidi kuwawia vigumu baada ya Watu kuanza kufuatilia kura zilizopigwa na kugundulika kuwa kuna baadhi ya manahodha walipiga kura zao kwenda kwa Mtu fulani lakini zikadondokea kwenye sanduku la Mshindi. Miongoni mwa kura hizo ilikuwa ni ya Nahodha wa Juventus Gigi Buffon.

Hapa tena France Football wakazidi kujishushia hadhi na heshima waliokuwa nayo tangu awali.

Mikanganyiko na upendeleo wa wazi ukazidi kuziandama tuzo hizi. Wakati bado Watu wakiwa wanaendelea kuvunja uaminifu na kujitoa kufuatilia tuzo hizi, waandaaji wakaja na kituko na sarakasi mpya.

Baada ya wale jamaa zao wawili kukosa vigezo vyote yaani mataji na magoli eti wakaja na porojo mpya ya Mfungaji mwenye magoli mengi kwa kalenda ya mwaka.

Watu tukahoji Kalenda ya mwaka inaingiaje kwenye maswala ya Soka ukizingatia kalenda ya mwaka imebeba misimu miwili tofauti ya Soka?

Kwa maana Ligi huwa zinaanza mwezi wa 8 na kuisha mwezi wa 5?! Safari hii hawakuwa na jibu lolote wakaamua kunyamaza kimyaa.

Msimu uliopita wale jamaa zao wote wawili walikuwa chali, hakuna aliekuwa na makombe mengi wala magoli mengi. Kwa kifupi hakukuwa kati yao hata na mwenye takwimu za kuongoza kwa kupiga madochi mengi, hivyo France Football wakaamua kujibanza kwenye kivuli cha Covid-19 hivyo kwa Mwaka huo tuzo hazitokuwepo.

Duru za Soka hazikunyamaza zikawahoji je kwani Ligi si ziliendelea na mabingwa walipatikana sambamba na wafungaji bora?!
Sasa kwanini Tuzo zisiwepo? Safari hii tena hawakujibu kitu na wakaendelea kutoa misaada kwa waathirika wa Covid -19.

Wakati France Football wanajistua wenyewe na kukimbia kwenda kujificha chini ya Meza, upande wa pili FIFA waliitoa tuzo yao ya mchezaji bora wa Mwaka kama kawaida na kumpa aliestahili Bob Lewandowsky.

Msimu huu tumeshuhudia tena matapishi kwenye ugawaji tuzo yakiendelea kama ilivyo ada. Safari hii tumeshuhudia ikitangazwa tuzo mpya eti ya Mfungaji bora.

Baada ya kutangazwa tuzo hii na kupewa Bob Lewandowsky basi wajuzi wa mambo tukazima TV kwa maana tulishajuwa wazi kuwa ile ni danganya toto tu ya kumpoza Lewa ambae ndie ana Magoli mengi kumzidi mshindi na ni mmoja kati ya Watu waliostahili sambamba na Joji ambae yeye ana Mataji mengi makubwa msimu huu kumzidi mshindi.

Mpaka sasa hakuna maelezo toka kwa waandaji wa tuzo hizo, kwanini Mtu mwenye taji moja kubwa taji ambalo linaamuliwa kwa mechi 6 tu zikiwemo dhidi ya Peru, Bolivia na Colombia ambayo haijafunga goli kwenye mechi zake 5 za mwisho apewe tuzo hio ya Ballon d’Or?!

Sijui watajitokeza au wataamua kunyamaza kama kawaida yao kwa miaka ya hivi karibuni?!

Tusubiri, ila naweka msimamo wangu kuwa tuzo hizi ziliisha thamani tangu mwaka 2007. Kilichoendelea baadae hata shetani kasema hahusiki na dhambi hizo tusimshirikishe.
 
255718011579_status_7d8d4fa0086a4c26b27fbceee45ea868.jpg
 
Ribery
Robben
Iniesta
Wesley
Lewandowisk

Hawa jamaa walistahili pakubwa
Hapo kwa Ribbery, ndo ilikua wazi wazi kabisaa. Robben mzee wa para kutoka iv amestaafu au? Maan simsikii now. Au mie ndo nipo nyuma ya life la kabumbu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom