Tazama video ya Jussa, jiulize ilikuwaje ACT Wazalendo ikaunda Serikali ya mseto

Mkuu PhD alianza nadhani 2015 kma sikosei..... Pengine anafanya by Dissertation tu so hapo inahitajika papers za kutosha kabla hujagraduate. Minimum ni miaka 5 so ni suala la muda tu but content wise ni PhD candidate yule.
Sawa lkn sio Dr bado unawaweza kusoma phd hata miaka 10
 
Sasa ni wakati muafaka kwa wazanzibari kujitoa kwenye hiyo sirikali fake ya mseto, na hii itakuwa njia muafaka ya kumu enzi maalim
 
Nyie acheni uchochezi! Mwenyezi Mungu hupanga kila jambo, uchaguzi huu ndio ulikuwa uchaguzi wenye matokeo mabaya kabisa kwa Maalim Seif Sharif Hamad lakini akakubali kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa!

Angalia ameenda Chato kumwaaga Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa JMT Dr.Magufuli na aka pledge commitments zake kwake , na amewaacha Wazanzibar wamoja kabisa.

Angalia mazishi yake jinsi yanavyofanyika kwa heshima kubwa, fikiria tofauti kama angekufa akiwa mtu wa vurugu na kuzira kama CHADEMA walivyokuwa wakitaka!

Hivyo tukubali tu kuwa sisi ni binadamu na mwisho wetu aujuaye ni Mwenyezi Mungu!
Maalima Seif Sharif Hamad amepigana vita vitakatifu na amemaliza kwa heshima kubwa ( Life well lived).
Rest In Peace Maalim, Amen!
umechanjwa au unategemea gamboshi?
 
Sawa lkn sio Dr bado unawaweza kusoma phd hata miaka 10
Wapi nimesema Zitto ni Doctor? Issue ni kugraduate tu lakini content si unakua umeipata. Hapo wanachelewa kwenye publications tu sababu lazima zipitiwe sana na machapisho walau yafike 5.
 
Kosa lingine walilo fanya wazanzibai ni kumwachia maalim augulie mikononi mwa ma CCM pamoja na akina zitto, kama unadhan sirikali hizi za ma-CCM zingeweza kumwangalia na kuya pigania maisha ya maalim basi wewe hujui siasa za TZ!!!!!!
 
Nyie acheni uchochezi! Mwenyezi Mungu hupanga kila jambo, uchaguzi huu ndio ulikuwa uchaguzi wenye matokeo mabaya kabisa kwa Maalim Seif Sharif Hamad lakini akakubali kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa!

Angalia ameenda Chato kumwaaga Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa JMT Dr.Magufuli na aka pledge commitments zake kwake , na amewaacha Wazanzibar wamoja kabisa.

Angalia mazishi yake jinsi yanavyofanyika kwa heshima kubwa, fikiria tofauti kama angekufa akiwa mtu wa vurugu na kuzira kama CHADEMA walivyokuwa wakitaka!

Hivyo tukubali tu kuwa sisi ni binadamu na mwisho wetu aujuaye ni Mwenyezi Mungu!
Maalima Seif Sharif Hamad amepigana vita vitakatifu na amemaliza kwa heshima kubwa ( Life well lived).
Rest In Peace Maalim, Amen!
Hoja hujibiwa kwa hoja, nami nitakujibu hapa hapa JF.

Kwanza kabisa, elewa tu, hakuna uchaguzi wa rais uliowahi kufanyika Zanzibar na Maalim Seif akashindwa kwa haki. Hakuna. Chaguzi zote zimekuwa zikichezewa na watawala.

Huu uchaguzi wa 2020 huenda ndio uchaguzi ambao Maalim amevuna kura nyingi zaidi kuliko uchaguzi wowote wa Zanzibar ikiwa haki ingetendeka. Kwanini? Ulikuwa ni uchaguzi wenye wagombea wawili muhimu, mmoja ni mtanganyika (Mwinyi) na mwingine ni mzanzibar (Maalim Seif). Kwa wazanzibar, huwezi kuwatenganisha na maalim Seif. Ni alama ya ukombozi wa wazanzibar wanaoteseka toka mapinduzi ya mwaka 1961.

Kuhusu Maalim Seif kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar kwa kipindi hiki, hilo lilikuwa ni kosa kubwa sana la kiufundi. Maalim Seif alikosea, tena alikosea sana. Sababu kuu ni hizi.

1. Aliibiwa kura na akakubali kuingia kwenye serikali bila maridhiano. Alikuwa anatafuta nini?

2. Alikubali kushirikiana moja kwa moja na adui yake bila tahadhari yoyote. Adui yako ni adui yako. Toka lini shetani akawa mwema kwako wewe unaempinga?

CCM ya Magufuli haijawahi kuwa na nia yoyote ya kudumisha demokrasia na haki za watu. Maalim Seif aliamini ipo siku watawala wa CCM wa zama hizi wangeingiwa na huruma au busara ili kumpa favour za kisiasa. Hilo lilikuwa ni kosa kubwa, na vizazi na vizazi vitabakia kujifunza hilo kosa alilolifanya maalim Seif.

Tukubali tu, Maalim Seif alikuwa ni mwamba wa kisiasa kwa wazanzibar, na kwa sasa ni mwamba uliolala milele. Ni ndege mjanja aliyenaswa na tundu bovu.

Poor Maalim Seif!!
 
Hili ndio kosa kubwa zaidi la kiufundi kwa Maalim Seif, alikosea sana. Kuwaamini watawala wa sasa wanaweza kusimamia afya yake. Wanasiasa wengine wajifunze. Adui yako ni adui yako tu. Daima ishi naye kwa tahadhari kubwa mnoo.
Kosa lingine walilo fanya wazanzibai ni kumwachia maalim augulie mikononi mwa ma CCM pamoja na akina zitto, kama unadhan sirikali hizi za ma-CCM zingeweza kumwangalia na kuya pigania maisha ya maalim basi wewe hujui siasa za TZ!!!!!!i
 
Nampenda Sana Jussa,yupo kati ya wanasiasa 10 ninaowahusudu duniani na kuwaheshimu sana. Yupo kwenye fungu moja kwangu na kina Mbowe, Obama, Peter Serukamba, Kikwete, Ghadafi, Javad Zarif nk
 
Back
Top Bottom