JokaKuu
Platinum Member
- Jul 31, 2006
- 30,441
- 55,018
Mwandishi punguza chuki. Hio picha ya Jussa ni miongoni mwa mamia ya walijeruhiwa kabla na Luna wengi waliuawa. Hoja yako nini hapa?
Huijui siasa ya Zanzibar wala humjui adui was kweli was Zanzibar na pengine huwajui Wazanzibari wanataka nini.
Kama siasa iko hivyo unavyodhani basis kusingepatikana hata hiyo GNU 2009, maana watu walishakufa sana mwaka 2001.
Kufikia malengo kwenye siasa hakuna njia moja. Maalim na Wenzake wametumia njia zote kufikia malengo na hakufika asilimia 100.
Unataka kuchora picha ya uchonganishi kwenye msiba wa jemedari aliyekufa katikati ya mapambano kwa kumwita msaliti ilihali maelfu wanamlilia na kumuhitaji?
Akina Jussa wako wengi tokea 1995, 2000, 2005, 2010 ,2015 na 2020.
Kwa nini unaegemea 2020 pekee?
Wazanzibari wako kwenye mapambano na mwaka 2020 walichagua maridhiano kuendeleza mapambano yao. Jemedari Maalim alitangulizwa ndani ya GNU kwa maslahi ya Zanzibar.
Tangulia Maalim. Mwandishi usitoneshe watu vidonda.
Daima tutakukumbuka
..tatizo wanaoumizwa na kutiwa vilema ni wapinzani tu. ccm wao aaahh, wako na raha zao.
..binafsi simlaumu mtoa mada, na pia siwalaumu mnaounga mkono ACT kujiunga na GNU.
..ninachojiuliza ni hali hii ya wapinzani kufanyiwa unyama na ccm, na kutendewa kama raia wa daraja la tatu itaisha lini?