Tazama mtoto huyu mbele ya Mkuu wa mkoa

Tazama mtoto huyu mbele ya Mkuu wa mkoa

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,945
Mtazame huyo mtoto mwenye gauni la "orange"......rangi ya gauni na huruma ya uso wake..........sidhani hata kama anasoma chekechea...lakini ni tafsiri ya maisha ya watoto wa kijijini wa Tz.....
 

Attachments

  • mtoto.jpg
    mtoto.jpg
    74 KB · Views: 2,106
Ila siasa inahitaji kuwa na roho ngumu kweli. Situations kama hizi huwa zinanipa stress na nakuwa hyper for several days.
 
ukiangalia huyo mama anasema kuwa kinachofuata sasa ni kununua nguo za madogo kama huyu..
 
Maskini inatia imani kabisa, wao wameshiba sisi tuna njaa
 
Huyo Mkuu wa Mkoa gani?
Kweli ni huzuni sana ndg zangu.
 
mmmh! sijui naona vby amaa ndo hali halisi ilivyo??
 
Mkoa wa Rukwa!hapo wanapata msaada wa madawati toka taasisi binafsi!
 
Mkoa wa Rukwa!hapo wanapata msaada wa madawati toka taasisi binafsi!

Yeah naona madawati "donated by" kisha utasikia yameletwa na serikali.

Mtoto anatia huruma sana. King'asti tumfate?
 
Last edited by a moderator:
Wapo wengi sana wa hivyo tz hii

Huu ndio mfumo tulio uchagua

Zinduka mtz kashfa za udini hazitaleta ukombozi wa dhati

Dhulma hii kwa wananchi haibagui dini

Huu ndio mfumo wetu sisi wadanganyika
Wewe unaejisifia umesoma sanaa na dini yako ni bora. Unadhulumu masikini hutendi haki. Elimu na dini yako ni sifuri

Huu ndio mfumo wetu sisi watz

Mazao yao hayajulikani yatanunuliwa kwa bei gani na lini. Michango ya maendeleo kila mwaka wanatoa lakini hakuna maendelea.

Huu ndio. Mfumo ulee mfumoo..................
Gandamizi
 
Mtazame huyo mtoto mwenye gauni la "orange"......rangi ya gauni na huruma ya uso wake..........sidhani hata kama anasoma chekechea...lakini ni tafsiri ya maisha ya watoto wa kijijini wa Tz.....

Una matatizo ya kufikiri. Kwanini mtu azae kama hawezi kulea?

Mitanzania haiendelei kwa kuwa inataka yenyewe ilelewe na watoto wao walelewe. Wewe kama una huruma sana, umeshaokota wangapi wa mitaani ukawalea? au huwaoni?

Ni kipi kilichokufanya uropoke kwa kudhani kuhusu huyo mtoto?
 
Ila siasa inahitaji kuwa na roho ngumu kweli. Situations kama hizi huwa zinanipa stress na nakuwa hyper for several days.

Roho ngumu bado huwa inaruhusu sympathy. Kwa wanasiasa wakwetu ni KAUZU-anakutazama ila anazuia ubongo wake kukuona maana utamfanya akumbuke kwamba anadanganya!
 
Una matatizo ya kufikiri. Kwanini mtu azae kama hawezi kulea?

Mitanzania haiendelei kwa kuwa inataka yenyewe ilelewe na watoto wao walelewe. Wewe kama una huruma sana, umeshaokota wangapi wa mitaani ukawalea? au huwaoni?

Ni kipi kilichokufanya uropoke kwa kudhani kuhusu huyo mtoto?

Hivi huyo anayewapa buku saba kwa kila posti huwa hawapi miongozo juu ya nini cha kupinga na nini cha kusapoti? Kwa ulichoandika nadhani utakuwa unavuta msuba tena kwa kutumia makalio.

Binadamu gani wewe usiye hata na moyo wa kibinadamu? Dini gani hiyo inayokufundisha kuwa na roho ya kutu kiasi hicho?
 
Kaka tutawafuata wangapi unadhani? Huyo anatia huruma walau ana gauni. Kuna ambae yuko peku, mwingine kifua kinakoroma unajua kabisa anahitaji antibiotic na hospitali hamna. Na wazazi wao wanangojea baki ya mazao waliyokopwa na chama cha ushirika.

Nchi imelogwa na alieiloga keshakufa.
Yeah naona madawati "donated by" kisha utasikia yameletwa na serikali.

Mtoto anatia huruma sana. King'asti tumfate?
 
Kwa kweli nimeguswa sana na hali lakini nashangaa pia watz walivyo wanafki kujitia wanahuruma sana for some places only lakini ni dhahiri kwamba aina hii ya watoto na watu wazima wanaishi in our local areas lakini je ni hatua gani at least tumehukua kwa yale yaliyo ndani ya uwezo wetu kuwasaidia chakushangaza eti wengine wanajidai kushangaa as if ni diaspora hali ni unafki tu!!! Acheni izo sio mpango!!!
 
Una matatizo ya kufikiri. Kwanini mtu azae kama hawezi kulea?

Mitanzania haiendelei kwa kuwa inataka yenyewe ilelewe na watoto wao walelewe. Wewe kama una huruma sana, umeshaokota wangapi wa mitaani ukawalea? au huwaoni?

Ni kipi kilichokufanya uropoke kwa kudhani kuhusu huyo mtoto?

Mazombi ndo akili yenu
 
Back
Top Bottom