Tayari mabomu yanarindima hapa Njombe muda huu

Tayari mabomu yanarindima hapa Njombe muda huu

Rose Mayemba

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2012
Posts
721
Reaction score
1,017
Tuko hospitali ya mkoa wa Njombe muda huu.Mimi Niko kichochoroni nimejibanza baada ta kuanza kupigwa mabomu na polisi.

Wananchi walifunga njia ili kuishinikiza serikali itoe tamko juu ya mauaji ya RAIA aliyeuawa kwa risasi na polisi bila hatua.

Wananchi wametawanyika hovyo hivyo nitawajuza baadae kinachoendelea huko barabarani. Hapo jana iliripotiwa Polisi kuua Mwananchi kwa Risasi saa tatu usiku kwa kosa la uzurulaji=> Polisi waua raia kwa risasi Njombe kwa kisingizio cha uzurulaji

==== Updates =====

Wagonjwa walioko mawodini hali ni mbaya,moshi wa mabomu ya machozi umeleta athari kubwa sana.Manesi na madaktari wanahangaika kukimbia hakuna Huduma yoyote inayoendelea hapa hospitali.

attachment.php

Polisi wakiwa wametanda eneo la Hospitali

Tutaendelea kuleta habari jinsi zinapotufikia kwenye vyote vya habari.

View attachment 253147
 
Tuko hospital I ya mkoa wa njombe muda huu.Mimi Niko kichochoroni nimejibanza baada ta kuanza kupigwa mabomu na polisi.

Wananchi walifunga njia ili kuishinikiza serikali itoe tamko juu ya mauaji ya RAIA aliyeuwawa kwa risasi na polisi bila hatua....

Wananchi wametawanyika hovyo hivyo nitawajuza baadae kinachoendelea huko barabarani

Tutaendelea kuleta habari jinsi zinapotufikia kwenye vyote vya habari.

njombe.jpg
 
Polen sana wana njombe, Nadhani polisi wanawafikishia ujumbe kuwa seriali ya ccm imechoka na haiwajali tena.
 
Hawa Police wa CCM sijui wanatumia kiungo gani kufikiria na kutenda... Mabomu hospitalini?...
 
Poleni sana wana Njombe. Huyo Rose Mayemba ndiye mratibu wa vurugu hizo. Thanks jeshi la Polisi kwa kuwatawanya maana hali ingekuwa mbaya sana kwa wasafiri wanaotoka Songea. Ila hakikisheni mnamkamata huyu Rose Mayemba
 
Hawa Police wa CCM sijui wanatumia kiungo gani kufikiria na kutenda... Mabomu hospitalini?...
Ka bahati mbaya sana moshi hauchagui mahala pa kwenda. Mabomu ya machozi ni moja ya silaha zinazotumiwa na jeshi la polisi
 
Mimi nafikiri ifike mahari police watuheshimu wananchi,mkikamata police mfanyeni kama yule wa Burundi
 
Ka bahati mbaya sana moshi hauchagui mahala pa kwenda. Mabomu ya machozi ni moja ya silaha zinazotumiwa na jeshi la polisi

moshi hauchagui ila wao wangeweza kuchagua njia mbadala kwa kuzingatia uwepo wa hiyo hospital...wangeweza kuwamwagia maji kuwapiga ngumu au kuwakimbiza kwa mbwa!
 
Back
Top Bottom