Tawi la CHADEMA kufunguliwa USA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tawi la CHADEMA kufunguliwa USA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TITAN, May 26, 2011.

 1. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wapiganaji wenzangu tunapenda kuwatangazia kwamba siku si nyingi Wapambanaji wa Chadema watafungua tawi USA, kunamaswala ya Itifaki na Kiufundi yanamaliziwa alafu watawajuza.
  Wanaomba maoni yetu Tafadhali.

   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Good Idea.... kamilisheni hizo Itifaki fasta Am behind you guyz
  we need changes
   
 3. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #3
  May 26, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Bad idea kama ilivyo bad idea kwa ccm kufungua matawi nje ya nchi. Kuisupport chadema kama upo majuu sio lazima mfungue tawi.....
   
 4. Tanganyika1

  Tanganyika1 JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  unamaana maoni yetu yanaweza kubadilisha dhamira ya sasa ya kufungua tawi hlo? Afu hayo matawi ya nje nchi ni mbwembwe tu...mtu anaishi marekani ambako umeme haukatik, afya poa, elimu bomba, hakuna njaa. We unadhani atawakumbuka mlie afrika juani? Ni upuuz mtupu.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Kazeni buti, hata kama mko nje mna mchango mkubwa sana kwenye ukombozi wa nchi. Fuatilieni habari za humu, zambazeni humo mliko ili wabeba vibakuli wakipita waulizwe i.e inakuwaje polisi wanaua raia? etc. jengeni mawasaliano mazuri na wanaharakati wa haki za binadamu huko ili wasaidie kushikinikiza serikali zao wawashughulikie hawa wanyonyaji.
   
 6. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu nimekupata sana, lkn helewa kwamba kila Mtanzania aliyepo mahali popote anaaki ya kusaidia nchi yake, japo kua si kifedha ila ata kimamazo na mtazamo.
  Kufungua tawi nje ya nchi ni ishara tosha kwamba tunakubali mabadiliko alafu tunataka kuwa na umoja ambao utatukutanisha ili tuweze kuangalia jinsi ya ku support mabadiliko.
  Pia elewa kwamba mageuzi ayaletwi na watu walio sehemu moja bali kila mpenda mabadiliko aliye kila mahali anaweza kuchangaia mageuzi. watu wanamichango mingi sana ya mabadiliko lkn inashindwa kutekelezeka kwa kuwa akuna kiongozi wa juu anayechukulia serious. kuhusu Umeme iyo issue imekaa kisiasa sana kuliko kiufundi.
  B

   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  The Best thing is to try to convice the GVT to allow people to Vote Overseas and not kufungua Tawi;

  Kwasababu ina Maana watu wa huku watakuwa wanatafuta Ruzuku toka Makao Makuu ya Chadema kama CCM? itakuwa ni Wizi Mtupu angalia USA hawana Tawi la Republicans or Democrats nje ya nchi yao, kwanini sisi Masikini?
   
 8. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  cdm acheni kuiga kilakitu toka ccm mtaiga vsivyoigiza
   
 9. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,757
  Likes Received: 6,055
  Trophy Points: 280
  Exactly Bro. The best they can do to support CHADEMA ni kama ifuatavyo badala ya kufungua tu matawi:-

  (i) Kwa dini yako, kwanza iombee Tanzania na watu wake; halafu ombea CHADEMA na viongozi wake Mungu awalinde hasa katika kipindi hiki kizito ambacho maadui ni wengi.

  (ii) Isaidie CHADEMA kwa michango ya hali na mali; mambo yanayotakiwa kufanywa ni mengi mno but resources are so limited.

  (iii) Wakati wa kujiandikisha na kupiga kura kwa uchanguzi wowote tokeni huko Marekani na kwingine mliko; rudini nyumbani muipigie kura CHADEMA.

  (iv) Fundisha watoto na watoto wa watoto wako, ndugu, jamaa, na marafiki zako kuyashika yote yaliyoelekezwa katika (i), (ii), (iii) hapo juu.

  This is the best you can do for CHADEMA and Tanzania in general.
   
 10. R

  Radi Member

  #10
  May 26, 2011
  Joined: May 22, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  All the best guy's. Pia naomba watueleze ni jinsi gani au kwa njia zipi tunaweza kujiunga na CDM tukiwa huku mbali.Freedom is comming now.
   
 11. F

  FJM JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Titan, naomba nirudie hili maana nina uhakika nalo. Jengeni mahusiano mazuri na wanaharakati wa haki za binadamu ili matukio kama ya Tarime yanapotekea inakuwa rais kwa dunia nzima kujua ni kwa jinsi gani haki za binadamu zinakiukwa.

  Kukiwa na pressure ndani, na nyie huko mkaanika kila kitu inatakuwa vigumu kwa hawa wakubwa kuendeleza ubabe. Jaribuni kuwasiliana na asasi kama Amnest International.

  Msife moyo na mitazamo tofauti tunayotoa humu jamvini. Ni Idea nzuri but you need to work out the best methods za kusaidia mapambano. Network network network.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  May 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Mbona kama kuna watu wanawasiwasi na jambo hili. Kama tawi linafunguliwa liwe moja kwa US nzima.. ndio ushauri wangu..
   
 13. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #13
  May 26, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Correct. Kama CDM itaanza kuiga CCM, basi by extrapolation kuna hatari nayo ikaja fikia kuwa gamba. Waacheni CCM na matawi yao. Nyinyi wafuasi wa CDM mnaoishi nje ya nchi mna nafasi n yingine nyingi za kuisaidia CDM bila kufungua matawi huko. Kwanza sidhani kama katiba inayatambua matawi ya aina hiyo
   
 14. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwa Mabest walioko huko U.S.A,mi nafsi yangu ningeomba contact ya mawasiliano yenu ya mkono tujadili mawili matatu. UKOMBOZI NI LEO.
   
 15. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekupa mkuu tunashukuru sana.
  Nashukuru sana kwa mawazo yenu wanajamii. Sisi tumekua tukifuatilia kwa karibu matukio yote yanayoteka nchini kwetu kwa baati nzuri tumekuwa na mawasiliano mazuri na baadhi ya wapiganaji apo nyumbani,
  1. tulipata DVD ya Matukio ya Arusha wakati wa uchaguzi wa Meya. (Ili lina utata kwani DVD tuliyo wapa na ile iliyo tolewa na serekali ni tofauti soo wanafanya investigation kujua ipi ni ya kweli na ipi ya uongo)
  2. Tulipata DVD ya Tarime/ Mara wakati wa uchaguzi mkuu watu walivyo fanyiwa.
  3. Tumepata picha mbali mbali za matukio ya ukiukwaji wa aki za binadamu,

  Tulitafuta watu wa kutusaidia kufatilia ili swala na kulipeleka congress pamoja na makao makuu ya aki za binadamu wamefanikiwa sana na wamewasiliana na serekali ya tanzania (according to them) wanasubiri ripoti kutoka Bongo kuhusu maswala yote.

  Kuhusu Ruzuku, kaka Sisi atutegemei Pesa kutoka makao makuu Tumejitole kwa iki tunachopata uku, ninazotengeneza apa zinanitosha Mm na familia yangu, Kingine akuna garama kabisa kufatilia aya mambo kwani uku swala la technologia linasaidia kupunguza garama za uendeshaji kwa kila kitu, kinacho tu cost ni muda tuu, but is better to work on serious issue kuliko ku suf kwy facebook.

  Kunamaswala mengi tuu tunaweza kusaidia but some times unaulizwa unaleta hii report ukiwa kama nani? Tunakosa majibu. but majibu yetu ni sisi ni Watanzania tunao pinga vitendo vyo ukiukwaji wa aki za binadamu. but some times wanauliza nani anawatambua? apo pagumu!!!!!

  Kunamengi ya kuzungumza but utapa yote soon tukimalizia maswala yetu, kila kitu kitakua kwy website yetu mengi atuwezi kusema apa kwakua tunaweza kuonekana tunatengeneza issue.
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  May 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Titan, naelewa muda ni tatizo kubwa sana hasa kwa huko mliko maana waajiri wako very strict na suala la muda. Ila naomba muangalie pia namna ya kusaidia ku-improve website ya CHADEMA ili iweze kuwa chombo muhimu cha kutoa habari za matukio na mikakati/sera za chadema. Kwa sasa ina mapungufu lakini huko najua swala la technology liko sawa.

  Kila la kheri.
   
 17. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekupa Mkuu tunashukuru sana, Tutajitaidi tuwasiliane na kitengo cha habari cha CDM tuangalie tatizo lipo wapi na jinsi ya kuwasaidi kama inawezekana tukiwa uku.
   
 18. MAFILILI

  MAFILILI JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,916
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ushauri wa bure, chama chetu cha CDM tutumie ruzuku kuhakikisha tuna matawi ambayo yanafanya kazi kwa kuanzia majimbo ypte ya DSM, pia tuongeze nguvu mikoa ya pwani, kwa vile huko tunawatembelea wakati wa uchaguzi tu . Hili la kufungua USA ni wazo zuri ingawa KIPAUPEMBELE kiwe ni kujitanua nchini.
   
 19. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  acha unafiki wewe,ni lini ulikuwa cdm ww? Ebu rudia michango yako ya nyuma hapa jf kama ujielewi.
   
 20. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #20
  May 27, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CDM inahitaji watanzania wote kuisaidia nchi yao kufikia utawala bora na maendeleo ya kweli ya Mtanzania. Inahitaji wapiga kura na elimu ya kutosha ya uraia kwa watu wake. Inahitaji wanachama wengi kadri inavyowezekana. Inahitaji michango mingi ya mali, elimu, sayansi na technologia kwa ajili ya kusaidia kuifanya nchi iendelee.

  wajibu mkubwa wa walio nje ni kuwa chachu ya maendeleo ya kijamii, kielimu, sayansi, demokrasia nk kwa nchi yetu. Ni vizuri kuwa na matawi, ila kabla kuanzishwa kwake ni lazima kufanyike utafiti wa nini itakuwa faida, na mwelekeo wa matawi haya. Ikizingatiwa sheria haziruhusu kupiga kura nje ya nchi.

  Je kukiwa na matawi kutawafanya wote wenye nia njema kuwa huru kusaidia chama kimawazo, na kimaendeleo?

  USA walipokuwa wanahangaika na health care bill, walifanyautafiti mkubwa na waliangalia kwa kina nchi zenye mfumo kama ule waliokuwa wanautaka ili kuona kama ni vipi walifanikisha kuwa na health care kama waliokuwa wakiitaka, waliangalia nchi kama Canada, na nchi za scandinavia.

  Sio jambo geni kuwa na vyama vya siasa nje ya nchi, bangladesh walikuwa na mkusanyiko wa wabangadesh ukiongozwa na Dr Yunus wakaweza kuitengeneza Bangladesh kuwa nchi. Ghana walifanikiwa kuitoa serikali iliyokuwa madarakani kwa msukumo wa watu walioishi nje. Italy ilisaidiwa na walio ishi nje ya italy. Singapore vile vile ilisaidiwa sana na wananchi wake walioishi nje ya nchi.

  Matawi ya nje ni lazima yawe yana mission sio utitiri tu wa matawi usio na kichwa wala miguu. huwezi kuwa na Tawi nje ya nchi la kudumu. Kazi za siasa haswa zinahitajika kwenye uwanja husika. Wengi walioanzisha matawi ya nje ni kwasababu ya hali ya kisiasa haikuwaruhusu kufanya kwa ufanisi kazi za siasa kwenye nchi zao.

  Ili kuisaidia Tanzania ni vyema kuanzisha taasisi za kusaidia maendeleo, kutetea haki za binadamau, mazingira, uwekezaji na haki elimu kwa jamii. kupitia haya tutasidia sana CDM ambayo tayari imeonyesha nia ya wazi kuwakomboa watanzania. Vikundi kama hivi huwa vinasikilizwa sana kwani huwa havionekani vimeegemea upande mmoja wa shillingi.

  Naipenda sana CDM na ningefurahi sana ingekuwa na matawi nje ya nchi ila nafikiri kunahaja ya kuangalia mtandao mzuri utakoisadia zaidi kuliko matawi ambayo hayatakuwa na kazi kubwa. Wapo watanzania wengi nje wanaoitakia mema Tanzania hasa kutoka mikononi mwa CCM. Na wanapenda sana kuisaidia CDM kwa hali na mali bila kuwa wanachama.

  Wakati tunafikiri kuwa na matawi hasa sisi wanachama hai, tujadili ufanisi wa hayo matawi, yasije yakawa matawi jina.
   
Loading...