Tatizo nini kufungwa Barca na A.C. Milan?

Tatizo nini kufungwa Barca na A.C. Milan?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,709
Reaction score
1,735
Katika UCL jana tarehe 20/2/2013 A.C. Milan wakiwa nyumbani walitutundika (Barca) mbao 2-0, leo magazeti takriban yote ya nchi hii yamepata soko wakati juzi tarehe 19/2/2013 huko London Arsenal walibamizwa 3-1 na Baryen Munich sikusikia mayowe.
Jamani tuwe wastaarabu kwani mpira una mambo matatu lazima ukubaliane nayo 1-kushinda, 2-kushindwa na 3-kutoka sare. Barca walikuwa ugenini na Arsenal walikuwa nyumbani sasa kwenye marudiano nani mwenye nafuu.
Cha ajabu wanaofurahia kufungwa Barca ni mashabiki wa Arsenal!
Nawakumbusha kuwa mechi ya jana haikuwa fainali bali tutarudiana huko Camp Nou.
 
Barca waliingia uwanjani wakiwa na lengo la kumiliki mpira na kupasiana kwa muda mrefu, wakati wenzao walikuwa na lengo moja tu: KUFUNGA MAGOLI.

Kila timu ilipata ilicholenga kupata. Barca walimiliki mpira karibu asilimia 80, lakini walipiga mashuti mawili tu golini, wakati wenzao wenye lengo la KUFUNGA MAGOLI walimiliki kwa asilimia hiyo 20 lakini walipiga mashuti 6 na kufunga mabao mawili
 
sasa unataka watu waandike utakavyo,kikawaida barca ni timu nzuri kuliko milan na ndio maana watu wote wameishupalia barca maana hawakutaraji matokeo yale.halafu walifikiri labda barca watapewa penati kama ya kipindi kile.acha hasira ulitaka wote tuishangilie barca.
 
Pasi 1000 za Barcelona si lolote pia ujue ndiyo kiwango na mbinu zinafifia wengi wanaamini Baca kesha tolewa.

Mapenzi kiasi lakini ukweli usemwe Baca safari km imewafikia vile.
Wajipange vema pia wengi waliibeza
Ac Milan .

Nou Camp ndipo ilipotolewa na Inter pia jua Milan wanapakuanzia wkt Baca wanasaka chochote kitu.

Ni vema ukubali kwa yaliyotokea tungoje watakaporudiana .
 
Back
Top Bottom