Nipe ushauri.....
Ili niweze kutengeza apk kama Whatsapp, facebook, au android app yoyote ile.... Nisome code language ipi/zipi.
Swali zuri,
Kama ndio kwanza unaanza na area ya programming uliyoipenda ni Mobile Apps Programming kulingana na swali lako
Nakushauri uanze na JavaScript
(Au kama una passion zaidi tujifunze Typescript)
Japo ni rahisi Ku shift from JavaScript to Typescript baadae
Faida ya kujifunza JavaScript ni kwamba utaitumie pande zote mbili
Frontend na Backed
Kama haupo familiar
Frontend ndio huo muonekano wa App yako,hicho mtumiaji anachokiona na kukishika....User Interface
Then Backend ni nyuma ya pazia ya app yako
Logics ya app ndipo ilipo...
Advantage nyingine ya JavaScript ni kwamba Cross platform Mobile App Framework ambayo ni popular kwa sawa inatumia JavaScript au Typescript kama lugha mama
Na App kama Facebook , Skype na Instagram zimetengenezwa entirely na hio Framework
Inaitwa React Native nitakuwekea links zake kama utahitaji
Baada ya kujifunza JavaScript, jifunze
Nodejs na React Native
Hio ndio njia ya kuwa Mobile App developers bora kwa sasa
Usisahau pia Basics za Web
Kama HTML na CSS
Haswa CSS
Hii inatumika Ku style web page lakini kwa kutumia React Native kuna similar concept ya kustyle app yako katika mtindo aina ya CSS