Tatizo langu ni lugha ya Kiingereza

Tatizo langu ni lugha ya Kiingereza

totoo brst

Member
Joined
Jun 3, 2014
Posts
85
Reaction score
22
Habari ta muda na wakati huu wapendwa?

Mwenzenu napenda sana kujua Kiingereza lakini ina niwia vigumu kutumia viunganishi vyake, Kwamba vinatumika wapi na kwa muda gani? Hili ndilo tatizo langu, naombeni msaada kama mtu anajua naomba ani orodheshee vyote hapa hapa.

Ahsanteni sana.
 
Sina shida nacho,hapo nimechapia bahati mbaya,kama unavyo jua simu zetu hizi za smart phone
 
Sawa tyta,
naaomba msaada wako pia katika lugha ya kiingereza
 
Kwangu mimi kujua lugha ninaanza na vitabu vya awali, nunua vitabu vya Kiingereza wanavyojifunzia watoto, usome na kujibu mwaswali mwenyewe, ikiwezekana tafuta na mwongozo wa mwalimu ujisahihishe. Shida itakuja kwenye ku pronounce, lakini ukifika huko jitahidi kusilikiza idhaa zinazoongea Kiingereza redioni.
 
muone RAS SIMBA, achana hawa
au mcheki LLE MUTUZ akufundishe cha kuonga na mbebiz mkarez
 
le mutuz embu njooo okoa jahazi bana nduguyetu wale wale tusijeaibika
 
Kwangu mimi kujua lugha ninaanza na vitabu vya awali, nunua vitabu vya Kiingereza wanavyojifunzia watoto, usome na kujibu mwaswali mwenyewe, ikiwezekana tafuta na mwongozo wa mwalimu ujisahihishe. Shida itakuja kwenye ku pronounce, lakini ukifika huko jitahidi kusilikiza idhaa zinazoongea Kiingereza redioni.

aisee hii tatizo ni kubwa kitaifa lazima lipewe kipaumbele kwenye kampeni za urais.wewe tunakuamini kwa ushauri mwanana unaanza tena kusema mwaswali? kheee..yaani asikilize BBC world ili kujua kiingereza?
 
Tuwe waungwana kidogo.

Kujua kiingereza siyo mpaka ujue kiswahili au lugha nyingine yeyote ile,japo kuna mahusiano kidogo ktk (comperative education). Elimu linganishi.

Unapotaka kujua kiingereza ni lazima ukubali kuwa msomaji wa vitabu na magazeti ya kiingereza. kama hukijui kabisa itakubidi uingie darasani ili angalau upate msingi wa lugha.

Tatizo kubwa la kiingereza hasa kwa watu wengi wanaojifunza ni pale anapotaka kukiongea mbele za watu na akahisi atakiharibu na kuchekwa au kudharauliwa, hivyo huamua kunyamanza kabisa au kuongea kwa kutumia maneno makuu tu kama vile; tomorrow akimaanisha i will go/come tomorrow.

Kwa Tanzania watu huamini kuwa anayejua kiingereza ni msomi lakini ukweli ni kwamba kiingereza huko Ulaya kwa nchi kama England katka baadhi ya maeneo hutumika mtaani kama lugha ya mawasiliano tu kama tunavyotumia Kiswahili huku kitaa.

Watu wengi wana idadi kubwa ya maneno ya kiingereza lakn kuongea ni shida na wengine wanajua kukiongea lakn kukiandika ni shida. tatizo hili linaweza kuwa lilisababishwa na mazingira; mwanafunzi mwenyewe au mwalimu wake.

Miongoni mwa mambo yanayosumbua sana ktk kuongea lugha hii ni pamoja na kujua haya:- the righ use of preposition such as "in,on,at,by" eg. Stand by somebody to refer to a help or support. Also the use of prepositional phrase like "away from, in the centre, at the edge of trouble".

To have the knowledge of TENSES(PRESENT/PAST/FUTURE, WORD CLASS(Noun, adjective, pronoun, verb, adverb, prep. Interjection etc. Having a little bit of knowledge of what i have flashed above will automatically guide you to have an access of speaking English regardless what first language you are from or know.
THANK U ALL COMREDZ
 
Kwangu mimi kujua lugha ninaanza na vitabu vya awali, nunua vitabu vya Kiingereza wanavyojifunzia watoto, usome na kujibu mwaswali mwenyewe, ikiwezekana tafuta na mwongozo wa mwalimu ujisahihishe. Shida itakuja kwenye ku pronounce, lakini ukifika huko jitahidi kusilikiza idhaa zinazoongea Kiingereza redioni.

Tunakubaliana nawe. Hivyo ndivyo nilivyojifunza Kifaransa na Lingala nilivyokaa Kinshasa zamani.
 
Cheki hii. Today.

Do & does
Kwa I ,YOU, HE, SHE, IT, WE, THEY.

1.I/you do, i do not do
Eg i play tennis everyday, I do not play football everyday
2. He/she/it does, does not do.
Eg He plays football every day, he does not play football every day.

Matumizi ya Do > { i, you, we & they}. Does{he, she & it}
 
Pole sana mkuu , upo sehemu gani wewe hapa jamhuri ya muungano wa tanzania?
 
Tatizo lako sio lugha ya Kiingereza tu! Hata Kiswahili tu nacho pia ni shida kwako! U have a long way to go...
 
Back
Top Bottom