TIMING
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 24,893
- 11,290
Hata hivyo nina kaswali kadogo tu kwa Mheshimiwa - kwa nini aliutafuta ubunge kwa tiketi ya CCM. Nauliza hivi kwa sababu hii post yake yaonyesha wazi kuwa kwa hili la umeme haridhiki na sera zinazotekelezwa na chama chake.
Matatizo ya umeme nchini ni zao la hizo sera na ilani ya uchaguzi za chama tawala na amepiga kura mara ngapi kupinga miswada inayowakilishwa bungeni na serikali. Katika uchaguzi ujao kama atasimama tena kugombea ubunge, je ana mkakati gani kuwa haya mapendekezo yake yatapewa kipaumbele kama chama chake kinashinda ? Je ni haki kulalamika kuwa miradi kama hii inahitaji hela nyingi wakati rasilimali za taifa zinatapanywa kama vile hazina mwenyewe.
Karibu Mh. Mohamed Dewji, Mbunge wa Singida.
Sidhani kama sera fulani ikikukwaza kwenye chama chako lazima ukimbilie chama kingine, na sidhani Mo amekuja kulalamika kwenye JF. Na at least ame-dare ku-talk openly sijui huko chamani watamuambiaje maana kuna watu hawataki kusikia chochote kuhusu mapungufu yao
Amefanya la maana kuleta hoja kama Mo kutokana na his faith kwamba JF kuna great thinker na sio sinkers
Sometime japo kwa sekunde tujaribu kuweka constructive idea halafu tuone kama ataleta impact yoyote...