Tatizo la umeme halitakuja liishe

Tatizo la umeme halitakuja liishe

Watanzania wenye uwezo wapo, na wengine wanafanya kazi hata nje ya Tanzania wakiwa na heshima kubwa kutokana na weledi wao
Mkuu naamini wewe sio mgeni wa hii nchi na huwa nakubali sana chambuzi zako humu JF. Mimi binafsi naamini watumishi waliopo serikalini wana utaalam na uwezo mzuri tu japo haiwezekani kukosa ambao hawana uwezo.
Nchi yetu inaharibiwa na mifumo iliyopo. Mwenye sauti ni mwanasiasa na sio mtu mwingine. Kimsingi rais ndiye mwenye final say hata kama atashauriwa vizuri. Na pia kumbuka washauri wakuu ni Mawaziri, unategemea ushauri wa maana kwa hawa machawa waliopo kwenye hizo nafasi!
Utakumbuka mzee JK akiwa rais aliwaleta wataalam wabobevu ambao ni watanzania wanaofanya kazi nje ya nchi. Wote ni mashahidi tunajua nini kilitokea wengine wakaangukia kwenye ufisadi. Kwa hiyo hata aje nani mfumo utammeza tu. Ambaye alishindwa kufanya kazi kwa sababu ya mfumo mbovu ni mzee Tido Muhando pale TBC. Wote tunajua mageuzi aliyofanya kwa muda mfupi alio hudumu.
Kama serikali imeshindwa kusimamia daladala hata 100 hazifiki unafikiri bila mifumo hata hao DP World watadumu?
Muda ni mwalimu, kuna mmoja ataomba kuvunja mkataba maana lazima huko mbeleni washindwane kwa sababu ya mifumo mibovu iliyopo.
 
Kwa sasa umeme na hudumu ya umeme ni ya uhakika hapa nchini ,ambapo hakuna changamoto kama ilivyokuwa swali.ambapo ukiona umeme haupo basi ujuwe kunakuwa kumejitokeza hitilafu ndogondogo ambazo kushughulikiwa na kumalizwa kwa haraka. Na pia taarifa hutolewa haraka sana na mamlaka kuwapatia taarifa watanzania.
Uhakika unamlaza mtu giza zaidi ya masaa 10

Ova
 
Mkuu Bams Hongera kwa andiko zuri lililojaa ukweli mchungu! Wenye uhalisia

Umeandika kwa hisia za mzalendo mwenye uchungu! Na anaegadhabishwa na huu uongo na ulaghai wa Serikali kwa mambo mengi sio umeme tu,

Binafsi naamini hili andiko litaishi humu miaka mingi, hata sisi tusipokuwepo

Kwangu Mimi pia NAAMINI! TATIZO LA MGAWO WA UMEME HALITAKUJAKAA LIISHE ABADANI! KAMA TUTAENDELEA KUWA NA KATIBA HII HII, NA SERIKALI HII!

Tusikae kudanganyana sijui bwawa la mwl. Nyerere, HAKUNA KITU HAPO! NI SANAA TU!... sijui wanatuonaje watanganyika!? Hili la umeme watu ndani ya Serikali Wana maslahi binafsi... NA NDIO MAANA MGAO WA UMEME HAUTAKUJA KUISHA!... NA HUO NDIO UKWELI MCHUNGU! TUNAPASWA KUISHI NAO... HATA KAMA HATUPENDI!
 
Umemaliza kila kitu.
Nchi yetu kwa sehemu kubwa inaongozwa na watu wasio na uwezo kwa sababu tu wao ndo vimbelembele, wanoko na machawa.


Watu wenye uwezo na maono ya kweli katika nchi hii wanapigwa sana vita na kamwe hawapewi nafasi na hata wakipewa nafasi wanapingwa sana na siku ya mwisho kutolewa kwenye nafasi zao kwa majungu, chuki na wivu.

Nchi hii itapona siku tukiwa na watu sahihi kwenye maeneo sahihi na hili litawezekana pale tu utaalam utakapopewa nguvu juu ya siasa kupitita Katiba

Umenena sahihi. Kwa hivi tunavyoenda, ni manung'uniko kila siku, na kwa jinsi tunavyozaliana kwa kasi, na aina ya viongozi tunaokuwa nao kupitia hii mifumo yetu ya hovyo, matatizo yatazidi kuonezeka badala ya kupungua.

Bila katiba mpya nzuri itakayovutia wenye uwezo kuingia na kufanya kazi serikalini na kwenye taasisi zake, hatuendi kokote.
 
Ukifika kariakoo ni kelele za jenereta tu.Hii nchi imeoza kabisa kipindi hiki cha bibi.mambo haya tuliyasahau miaka mitatu nyuma
 
Kwenye masuala ya management, tunasema mafanikio yoyote yanategemea aina watu ulio nao. People are the hub of the success wheel.

Aina ya watu ulio nao ndio wanaamua kampuni/taasisi/serikali, ifanikiwe au ishindwe kabisa. Haijalishi una pesa kiasi gani, haijalishi una vifaa kiasi gani, kama watu ulio nao hawana uwezo, utaanguka tu. Kama una watu wa hovyo, wanaweza kutumia pesa kununua mitambo na vifaa hovyo, wanaweza kuipa kandarasi kampuni ya hovyo. Hata uwe na vifaa vizuri na vya kisasa kiasi gani, ukiwa na operators wa hovyo, vyote vitakufa na hutaambulia chochote.

Wote tunajua jinsi huduma ya umeme ilivyo duni nchini mwetu. Siyo kwa sababu hakuna maji au gas, siyo kwa sababu hatuna nguzo au nyaya, wala siyo kwa sababu hatuna mitambo ya kuzalishia umeme. Tunaona barabara zinazojengwa kabla hazijamakizika zinaanza kuwekwa viraka, n.k; kila mahali ni hovyo. SABABU KUBWA NI KWAMBA HATUNA WATU SAHIHI WENYE UWEZO.

Kwa ujumla Serikali yetu haijawahi kufanya chochote kile kwa weledi na kwa mafanikio. Waliopo Serikalini hawanahata uwezo wa kumpata mkandarasi mzuri wa kuweza kujenga barabara kwa viwango bora.

Maadam umeme unaendelea kuzalishwa na shirika la TANESCO ambalo lipo chini ya Serikali, tusitarajie ufanisi wowote ule hata siku moja. Watanzania tukubali kuwa haya ndiyo ni maisha yetu ya kila siku. Aina ya watu waliopo huko Serikalini na namna wanavyopatikana, tusitarajie mafanikio yoyote zaidi ya hadithi za kila siku zisizoendana na uhalisia. Serikalini tuna watu mabingwa wa kuendesha mambo kwa ulaghai na uwongo. Na wao hiyo huiita ndiyo siasa ya Tanzania.

Siyo kwamba nchi haina watu wenye uwezo. Watanzania wenye uwezo wapo, na wengine wanafanya kazi hata nje ya Tanzania wakiwa na heshima kubwa kutokana na weledi wao. Lakini hata ndani ya nchi wapo ambao wangeweza kuleta mabadiliko makubwa.

Lakini watu wenye akili na uwezo mkubwa katika weledi, hata siku moja hawakubali kuwa machawa, huwa ni watu walionyoka, ni watu ambao siyo wanafiki, wao spade ni spade. Watu wa namna hiyo huwezi kuwakuta Serikalini. Kwa sababu serikalini sifa kubwa ya mtu kuteuliwa kuongoza taasisi zilizo chini ya Serikali ni uchawa, unafiki na kujuana. Na wanaoweza kufanya hayo ni wale tu wenye akili ndogo na uwezo mdogo ambao huwa wanataka kuziba pengo la upungufu wao katika uwezo na akili kwa unafiki wa kusifia na kujikomba kwa watawala. Na kwa sababu Serikali inapenda sana kusifiwa, itaendelea kuwa na aina hiyo hiyo ya watu, na Watanzania wataendelea kuishi kwa kupewa huduma duni.

Kupunguza tatizo hilo la kuwa na watu wenye uwezo duni kwenye taasisi zilizo chini ya Serikali, ilikuwa ni ile katiba ya Jaji Warioba. Yaani watu wapewe nafasi mbalimbali kwa kuangalia weledi wao na kwa kufuata kanuni za ajira. Rais asijihusishe kabisa na uteuzi wa wakuu wa kuendesha hizo taasisi. Rais abakie na mamlaka ya kuwateua mawaziri basi. Wengine wote wapatikane kwa weledi wao na siyo kupewa nafasi hizo kwa hisani ya Rais.
Sasa hivi hata majaji, mawaziri wapitie kamati au Bunge kuwapitisha nk
 
Haitakaa itokee kama wafanyakaz wa nchi hii hawana spirit ya kazi.Siku Serikali itakapobadilika na kutumia kulingana na hali yetu kama nchi wafanyakaz watapata morali.Usitegemee mfano Mwl afanye kaz miaka 60 anapewa kiinua mgongo cha m100 halaf mwingine anafanya kaz miaka 5 anapewa zaidi ya 400 halaf mwl huyu afanye kazi kwa juhudi.
Tatizo kubwa ni kuwa keki ya Taifa haigawanywi ipasavyo,hakuna haki na kuna nepotism ya hatari.Thats y anyone anayepata post yenye marupurupu uzalendo wake kwa nchi humomonyoka kidogokidogo kwakuwa anaona loophole kule juu,watu hawauishi udunia ya tatu wetu so anaona avune tu because tumeamua kiwa hivyo.
Natamani waliopo kwenye vyombo vya maamuzi na vyombo vya sheria wangepata uzalendo kidogo mambo yangebadilika
 
Mkuu Bams Hongera kwa andiko zuri lililojaa ukweli mchungu! Wenye uhalisia

Umeandika kwa hisia za mzalendo mwenye uchungu! Na anaegadhabishwa na huu uongo na ulaghai wa Serikali kwa mambo mengi sio umeme tu,

Binafsi naamini hili andiko litaishi humu miaka mingi, hata sisi tusipokuwepo

Kwangu Mimi pia NAAMINI! TATIZO LA MGAWO WA UMEME HALITAKUJAKAA LIISHE ABADANI! KAMA TUTAENDELEA KUWA NA KATIBA HII HII, NA SERIKALI HII!

Tusikae kudanganyana sijui bwawa la mwl. Nyerere, HAKUNA KITU HAPO! NI SANAA TU!... sijui wanatuonaje watanganyika!? Hili la umeme watu ndani ya Serikali Wana maslahi binafsi... NA NDIO MAANA MGAO WA UMEME HAUTAKUJA KUISHA!... NA HUO NDIO UKWELI MCHUNGU! TUNAPASWA KUISHI NAO... HATA KAMA HATUPENDI!
Nakubaliana nawe 100%. Kwa aina ya watu tulio nao kwenye ngazi za maamuzi, hata bwawa la Nyerere lifungiliwe milango yote, hakuna kikubwa kitakachobadilika kwenye ubora wa huduma ya umeme.
 
Hawa wataweza piga hata trilion basi

Ova

Kwa hawa watu tulio nao ndani ya Serikali na taasisi zake, kila kitu ni deal. Hakuna wakifanyacho bila kutanguliza maslahi yao binafsi. Wakishafanikisha wizi wao watatoka na sifa kibao za kinafiki kwa Rais ili kumpofusha asione uovu wao.
 
Mbona nasikia wananchi washamshukuru mama?
1711973287730.png

Au wanatupanga🤣🤣 maana naona kimya
 
Tanesco inaendeshwa kisiasa ,mainjinia wapo wapo tu hawajui wanafanya nini....Yaani grid haina hata backup .its utter nonsense.
 
Back
Top Bottom