Tatizo la umeme halitakuja liishe

Tatizo la umeme halitakuja liishe

Pamoja na haya uliyosema ila tutakapofikia hatua ya kutenga siasa na taaluma tutafika mbali sana. Mathalan mtu akitaka kuwa mkurugenzi wa Tanesco sharti ateuliwe na Rais. Hii si sawa hata kidogo. Tukitaka kupata viongozi wenye sifa sharti waombe kazi, wafanyiwe usaili na wachujwe kwa sifa zao na sera zao juu ya kuendeleza shirika. Hili la kila kitu afanye Rais si sawa. Tutachelewa sana kwenye maendeleo

Ni kweli.

Na hii ya kila mtendaji mkuu wa taasisi iliyo chini ya Setikali kuteuliwa na Rais, imesababisha kuzaliwa kwa machawa wengi, na kuwa na watendaji ambao akili na uwezo hakuna kabisa. Kuna baadhi unaongea nao masuala ya kitaalam mpaka unakata tamaa kabisa! Maana unamwona ni mtupu wa ajabu, hata huelewi amekuwaje hapo mtu asiyejua chochote kwa kiwango hicho.
 
Umeongea uhalisia kabisa. Serikalini kuna watendaji ambao uwezo wao ni wa kawaida sana na wanajaribu kulificha hilo kwa mbwembwe za maneno, kufoka foka, na kusifia

Wenye uwezo hawadumu kwasababu wenzao wanawaona kama hawaendani nao. Wanapotoa mawazo yaliyokinyume na mipango na matarajio ya wengine

Hata hivyo hili kwa kiasi kikubwa linachangiwa na kuwa na viongozi wa aina hiyo hiyo kwenye top position

Kiongozi ndio dira ya taasisi. Yeye ndio mwenye maono na watu wote wanasubiri wafuate mwongo atakaotoa

Inapotokea kiongozi akawa hana dira wala mwelekeo, anapenda mapambio kuliko uhalisia. Akiambiwa kwa maneno anaamini pasipo kufanya ufuatiliaji wale wote waliochini yake wata underperform kwasababu always human being are lazy. Mfanyakazi yoyote anahitaji close supervision ili uone matokeo chanya

Nchi itapiga hatua na kuachana na hayo yote uliyosema endapo tutapata viongozi wenye maono na wasioamini katika kukwezwa kwa maneno na sifa zisizo na msingi
Umemaliza kila kitu.
Nchi yetu kwa sehemu kubwa inaongozwa na watu wasio na uwezo kwa sababu tu wao ndo vimbelembele, wanoko na machawa.


Watu wenye uwezo na maono ya kweli katika nchi hii wanapigwa sana vita na kamwe hawapewi nafasi na hata wakipewa nafasi wanapingwa sana na siku ya mwisho kutolewa kwenye nafasi zao kwa majungu, chuki na wivu.

Nchi hii itapona siku tukiwa na watu sahihi kwenye maeneo sahihi na hili litawezekana pale tu utaalam utakapopewa nguvu juu ya siasa kupitita Katiba
 
* Ili kupata maendeleo vinahitajika:
1. Ardhi ✅
2. Watu ✅
3. Sasa safi ✖️
4. Uongozi Bora ✖️
  • Namba 3 ndio huzaa namba 4, vitu ambavyo ukiwa sirikalini na ukavipigia kelele ndg zako wanaweza omboleza mazishi yako haraka au uishi kama mzururaji.
  • Kwa jirani ili mtu apewe CEO wa shirika inafanyika vetting ya nguvu na mijadala nchi nzima; kwingine inapaswa kwanza uwe 'chawa', n.k. Je 'chawa' amewahi kuleta tija kwenye kaya yako?
 
Huwezi kuona kwa sababu wewe ulishajipofusha akili na macho yako na hivyo kuona maruerue tu mbele yako. Siku ukiacha akili yako na macho yako yakatizama mambo katika uhalisia wake kwa hakika utaona maajabu makubwa sana yaliyofanywa na serikali ya Rais wetu mpendwa Na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan.

Utaona mapinduzi katika Secta ya kilimo kulikowekezwa mabilioni ya pesa ambapo sasa bajeti ni Billion 970 ,utaona mapinduzi katika Afya ambako zaidi ya Trilioni sita zimetiririshwa huko,utaona mapinduzi katika Elimu,nishati, miundombinu,uchumi na maeneo karibu yote utakakopeleka jicho lako utaona mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kupatikana.
Hoja iliyopo mezani ni tatizo la umeme linaloendelea kila siku nchini, na huku chanzo chake kikiwa ni kukosekana na watu wenye sifa sahihi za kuweza kupewa dhamana katika uongozi na utendaji. Sasa wewe Lucas unadandia tu treni kwa mbele, na kisha kuingiza uchawa wako ili kuonyesha mahaba yako kwa rais na serikali hata kama inaboronga.

Ukiona "constructive critism" imeelekezwa kwa serikali, basi wakati mwingine pita hata kimya kimya pasipo kutia neno, ili upate madini kutoka kwa wachangiaji wengine. Maisha ya uchawa ni sawa kabisa na biashara ya udangaji. Tambua tu kuwa unajiuza kwa bei rahisi mno.
 
Huwezi kuona kwa sababu wewe ulishajipofusha akili na macho yako na hivyo kuona maruerue tu mbele yako. Siku ukiacha akili yako na macho yako yakatizama mambo katika uhalisia wake kwa hakika utaona maajabu makubwa sana yaliyofanywa na serikali ya Rais wetu mpendwa Na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan.

Utaona mapinduzi katika Secta ya kilimo kulikowekezwa mabilioni ya pesa ambapo sasa bajeti ni Billion 970 ,utaona mapinduzi katika Afya ambako zaidi ya Trilioni sita zimetiririshwa huko,utaona mapinduzi katika Elimu,nishati, miundombinu,uchumi na maeneo karibu yote utakakopeleka jicho lako utaona mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kupatikana.
Kilimo ambacho hakina tija?? Ambacho hakijawahi kumkomboa mkulima??

AFYA: Wingi wa majengo ambayo mnayaita vituo vya afya, visivyokua na wataalamu wa kutosha? Visivyokua na vifaa Tiba? Kila siku visivyokua na dawa, ikiwemo ujue Ni paracetamol, tofauti na hapo unashauriwa kanunue pharmacy.

ELIMU: Hapa nako Ni mitihani mitupu Mwenyezimungu awasamehe, mishahara kidogo kwa waalimu, Kila siku wanatuomba tuwakopeshe pesa, na kwa taarifa yako, waathirika wakubwa wa mikopo kausha damu Ni waalimu, tunawaona Kila siku wanavyodhalilika na madeni, hawana nyumba za kuishi, Bora wenzao polisi wanapewa pesa ya pango. Wao Kila siku Ni kilio, shida shida. Kwa mangi mwalimu Ana daftari la kukopea, kila mwisho wa Mwezi analipa Deni na kuanza Deni upya. Sizungumzui ubovu wa miundombinu, madarasa, meza na madawati, shule hazina ofisi za waalimu, Sera mbovu za ELIMU nk.

Kikubwa mlichobakiwa nacho Ni kusifiasifia tu na kusema anaupiga mwingi.

Nikukumbushe kuandika namba yako ya simu, Mana mikeka inatoka wewe huonekani
 
* Ili kupata maendeleo vinahitajika:
1. Ardhi ✅
2. Watu ✅
3. Sasa safi ✖️
4. Uongozi Bora ✖️
  • Namba 3 ndio huzaa namba 4, vitu ambavyo ukiwa sirikalini na ukavipigia kelele ndg zako wanaweza omboleza mazishi yako haraka au uishi kama mzururaji.
  • Kwa jirani ili mtu apewe CEO wa shirika inafanyika vetting ya nguvu na mijadala nchi nzima.
Nchi hii ina tatizo la Ujinga kwa wananchi wake katika kiwango cha kutisha sana.

Na bahati mbaya kupitia huo ujinga wa wananchi ndo tunapata Viongozi wajinga wasiojali kesho ya Taifa bali kesho ya mifuko yao na familia zao.

Amini maneno yangu. Ukiwachukua CEO's wote wa mashirika ya Umma, Mawaziri na Makatibu wakuu wote pamoja na Viongozi wote wakuu wa nchi hii ukiwauliza unaionaje Tanzania in the next 50 or 100 years unaweza pewa majibu ya ajabu hadi ukajuta kuzaliwa mwafrika na Mtanzania.

Kwa kifupi nchi hii u hovyo ndo umetawala kila mahali na tunaenda kwa kudra za MwenyeziMungu tu.

Itahitaji kuwa na watu based on merit wanaolindwa kikatiba inayoogopwa na kuheshimiwa na Wanasiasa na Wananchi wote ili nchi yetu iweze kupiga hatua sahihi za kimaendeleo na sio ngonjera tulizonazo sasa
 
Kuna mitambo fulani naona imeharibika inabidi inunuliwe mpya ifungwe 😄
Au kuna system imezingua kwa hiyo inahitajika bilion 10 kuboresha system mpya 😄

Kwa kwa kwa

Ova
Umeme umekatika Nchi Nzima au Sehemu kubwa ya Nchi !
Bilioni 10 ni pesa ndogo hiyo !
Wengine huwa wanaiita hela ya mboga tu !!
 
Kwa sasa umeme na hudumu ya umeme ni ya uhakika hapa nchini ,ambapo hakuna changamoto kama ilivyokuwa swali.ambapo ukiona umeme haupo basi ujuwe kunakuwa kumejitokeza hitilafu ndogondogo ambazo kushughulikiwa na kumalizwa kwa haraka. Na pia taarifa hutolewa haraka sana na mamlaka kuwapatia taarifa watanzania.
Changamoto zipo na hata hizo unazosema hazipo ni kwa sababu tu saivi mikoa mingi hasa ya kusini mvua zinanyesha hivyo mabwawa ya umeme kujaa.

Umeshawahi kujiuliza tukipata ukame wa mwaka au miaka 2 hali yetu ya umeme itakuwaje? Tuna vyanzo vya uhakika vya umeme vya kutupa umeme kipindi nchi imepata majanga kama ukame kwa muda mrefu?

Kama hujaelewa hii ndo hoja ya mtoa mada. Nchi hii inatakiwa kuwapa nafasi watu wanaowaza na kufikiria namna hii.

Wewe hujiulizi kwa nini Kenya hapo wameanza kujenga umeme wa Nyuklia?

Hizi ndo akili zinazotakiwa katika maeneo yote ya uongozi katika nchi yetu. Watu wanaowaza mbele sio watu wanaopewa nafasi za juu kwa sababu tu chawa, anajipendekeza, anajua kukaripia watu, mnoko au anasali sana au anaswali sana. Huu ni ujinga na ili tupate maendeleo ya kweli lazima tutoke huko na watu wapate nafasi based on merit.
 
Kwenye masuala ya management, tunasema mafanikio yoyote yanategemea aina watu ulio nao. People are the hub of the success wheel.

Aina ya watu ulio nao ndio wanaamua kampuni/taasisi/serikali, ifanikiwe au ishindwe kabisa. Haijalishi una pesa kiasi gani, haijalishi una vifaa kiasi gani, kama watu ulio nao hawana uwezo, utaanguka tu. Kama una watu wa hovyo, wanaweza kutumia pesa kununua mitambo na vifaa hovyo, wanaweza kuipa kandarasi kampuni ya hovyo. Hata uwe na vifaa vizuri na vya kisasa kiasi gani, ukiwa na operators wa hovyo, vyote vitakufa na hutaambulia chochote.

Wote tunajua jinsi huduma ya umeme ilivyo duni nchini mwetu. Siyo kwa sababu hakuna maji au gas, siyo kwa sababu hatuna nguzo au nyaya, wala siyo kwa sababu hatuna mitambo ya kuzalishia umeme. Tunaona barabara zinazojengwa kabla hazijamakizika zinaanza kuwekwa viraka, n.k; kila mahali ni hovyo. SABABU KUBWA NI KWAMBA HATUNA WATU SAHIHI WENYE UWEZO.

Kwa ujumla Serikali yetu haijawahi kufanya chochote kile kwa weledi na kwa mafanikio. Waliopo Serikalini hawanahata uwezo wa kumpata mkandarasi mzuri wa kuweza kujenga barabara kwa viwango bora.

Maadam umeme unaendelea kuzalishwa na shirika la TANESCO ambalo lipo chini ya Serikali, tusitarajie ufanisi wowote ule hata siku moja. Watanzania tukubali kuwa haya ndiyo ni maisha yetu ya kila siku. Aina ya watu waliopo huko Serikalini na namna wanavyopatikana, tusitarajie mafanikio yoyote zaidi ya hadithi za kila siku zisizoendana na uhalisia. Serikalini tuna watu mabingwa wa kuendesha mambo kwa ulaghai na uwongo. Na wao hiyo huiita ndiyo siasa ya Tanzania.

Siyo kwamba nchi haina watu wenye uwezo. Watanzania wenye uwezo wapo, na wengine wanafanya kazi hata nje ya Tanzania wakiwa na heshima kubwa kutokana na weledi wao. Lakini hata ndani ya nchi wapo ambao wangeweza kuleta mabadiliko makubwa.

Lakini watu wenye akili na uwezo mkubwa katika weledi, hata siku moja hawakubali kuwa machawa, huwa ni watu walionyoka, ni watu ambao siyo wanafiki, wao spade ni spade. Watu wa namna hiyo huwezi kuwakuta Serikalini. Kwa sababu serikalini sifa kubwa ya mtu kuteuliwa kuongoza taasisi zilizo chini ya Serikali ni uchawa, unafiki na kujuana. Na wanaoweza kufanya hayo ni wale tu wenye akili ndogo na uwezo mdogo ambao huwa wanataka kuziba pengo la upungufu wao katika uwezo na akili kwa unafiki wa kusifia na kujikomba kwa watawala. Na kwa sababu Serikali inapenda sana kusifiwa, itaendelea kuwa na aina hiyo hiyo ya watu, na Watanzania wataendelea kuishi kwa kupewa huduma duni.

Kupunguza tatizo hilo la kuwa na watu wenye uwezo duni kwenye taasisi zilizo chini ya Serikali, ilikuwa ni ile katiba ya Jaji Warioba. Yaani watu wapewe nafasi mbalimbali kwa kuangalia weledi wao na kwa kufuata kanuni za ajira. Rais asijihusishe kabisa na uteuzi wa wakuu wa kuendesha hizo taasisi. Rais abakie na mamlaka ya kuwateua mawaziri basi. Wengine wote wapatikane kwa weledi wao na siyo kupewa nafasi hizo kwa hisani ya Rais.

Kuweka naibu waziri mkuu kutuongezea gharama bure. Hii post ifutwe!
 
Umemaliza kila kitu.
Nchi yetu kwa sehemu kubwa inaongozwa na watu wasio na uwezo kwa sababu tu wao ndo vimbelembele, wanoko na machawa.


Watu wenye uwezo na maono ya kweli katika nchi hii wanapigwa sana vita na kamwe hawapewi nafasi na hata wakipewa nafasi wanapingwa sana na siku ya mwisho kutolewa kwenye nafasi zao kwa majungu, chuki na wivu.

Nchi hii itapona siku tukiwa na watu sahihi kwenye maeneo sahihi na hili litawezekana pale tu utaalam utakapopewa nguvu juu ya siasa kupitita Katiba
Katiba mpya bora ni muhimu sana !
 
Kuweka naibu waziri mkuu kutuongezea gharama bure. Hii post ifutwe!
Juzi eti analalamika yupo kwenye ziara alafu mkuu wa Taasisi ametuma mwakilishi.

Tuna viongozi wanaofikiri kuwa kwenye ziara yake anatakiwa kuambatana na wakuu wa Taasisi alafu hao wakuu wa Taasisi kazi zao za msingi waziache ili wakatembee tu na Waziri.

Huyu ndo anapewa nafasi ya Naibu Waziri Mkuu alafu nchi mnawaza kabisa mtapata maendeleo ya uhakika.

Hii nchi ukiwa na akili piga zako kimya tu maana inatia hasira, huruma na kinyaa.
 
Katiba mpya bora ni muhimu sana !
Na hapa ndo mwanzo wa mabadiliko ya kweli . Ila mbaya zaidi Wanasiasa wameshaju hilo kuwa kabuli lao katika siasa zao za kujinufaisha na uzandiki ni Katiba Mpya inayoipa nguvu mifumo kuliko wao na matamko yao.

As long as nchi hii wanasiasa ndo kila kitu sahauni iyo Katiba mpya na kamwe msiitegemee kwa sababu mmewapa nguvu wenyewe wanasiasa kuliko wataalam kupitia mifumo imara inayowa control wanasiasa.
 
Hapa naandika reply simu yangu inachaji 12% na umeme hakuna tangu jana usiku
Huku kwetu na ratiba ya mgao huwa inatoka kabisa ya wiki wiki. Hata walipotangaza mgao kuisha, huku haujawaji kuisha.
 
Back
Top Bottom