Robert S Gulenga
JF-Expert Member
- Jan 3, 2013
- 2,183
- 1,502
- Thread starter
- #61
Uko sahihi dudus ,wewe ukipanda miti umetimiza wajibu wako, na mimi nikipanda miti nimetimiza wajibu wangu na yule naye akipanda miti atakuwa ametimiza wajibu wake wa kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. Serikali kwa nafasi yake inaendelea kuchukua hatua stahiki kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.... nikipanda miti miwili mitatu ya kivuli hapa nje kwangu at the same time wachoma mikaa, warina asali, wafugaji, n.k wanateketeza maelfu ya ekari ya miti asilia kwa siku sidha kama itasaidia sana kupambana na hili janga.
Serikali iweke plan nzuri ya ardhi na maliasili hususan misitu ya asili. Atakayekamatwa anateketeza misitu iingie kwenye kosa la uhujumu uchumi! Ila hilo sio sahihi kufanyika wakati wananchi hawana option - mfano nishati. Shusha bei ya gas to affordable prices; I tell you wala huhitaji kutunga sheria ya ku-criminlze mkaa; wananchi wenyewe wataachana nao.
Kuhusu kushusha bei ya gesi -bei huwa zinaamuliwa na soko (demand and supply), serikali kama itaamua kushusha maana yake itoe ruzuku katika gesi, jambo hili linahitaji fedha, mikakati na mazingira lazima yawekwe sio jambo la siku moja. Muhimu ni kila mtu kuona kuna umuhimu wa kupambana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi