Tatizo la maji, Itungwe Sheria kila Mtu awe na mti aliopanda

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Jan 3, 2013
2,124
1,465
Mabadiliko ya tabia ya nchi ni tatizo la dunia, kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kumekuwa na athari nyingi ikiwa ni pamoja na ukame unaokumba nchi nyingi duniani. Baadhi ya nchi kwa sasa zinakosa mvua kwa kipindi cha mwaka mzima au zaidi.

Kwa namna shughuli za binadamu zinavyoongezeka, hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi inazidi kuwa mbaya saana, uwezekano mkubwa saana baada ya miaka 10-20 kiwango cha upatikanaji wa mvua kikawa kidogo saana kuweza kutosheleza mahitaji ya binadamu kama jitihada za makusudi na kweli hazitachukuliwa.

Miaka 40 nyuma, mito mingi inayopatikana Tanzania ilikuwa inatiririka mwaka mzima, lakini kwa sasa imebaki mabonde tu yasiyo na maji hata kipindi cha mvua, tatizo ni kubwa na kadri siku zinavyokwenda tatizo linaongezeka.

Ili kupambana na athari zinazotokana na madiliko ya tabia ya nchi na kupelekea kukosekana kwa mvua ni muhimu saana ikatungwa sheria inayolazimisha upandaji wa miti kwa hapa Tanzania.

Pamoja na juhudi nzuri zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita, chini ya Mh Samia Suluhu Hassan, yafuatayo yanaweza kufanyika-:

1. Kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 (Mwenye ajira ya kudumu) apande miti mitano kila mwaka, hili linawezekana.

2. Halmashauri zote ziweke mkakati wa kuwa na Shamba la miti, haijalishi ni ndani ya eneo lao au nje ya eneo lao kiutawala- Hii itakuwa pia chanzo cha Mapato kwa Halmashauri.

3. Shule zote (Msingi na Sekondari) ziwe na Shamba la mti, kila mwanafunzi awe na mti anaouhudumia (Zile za mjini ambazo hazina maeneo utaratibu uandaliwe kwa kupanda miti hapo shuleni tu)-Walimu Wakuu na MEK wapimwe kwa kuweza kusimamia hili.

4. Ofisi zote za Umma, kuanzia ofisi za Serikali za Mtaa, Kijiji, Kata e.t.c kila Mtumishi wa eneo hilo awe na mti anao uhudumia, kusiwepo na ofisi ya Umma isiyo na miti.

5. Serikali iwezeshe kitengo cha Mazingira katika Halmashauri, Maafisa Mazingira wa Halmashauri wapimwe kwa namna wanavyosimamia upandaji wa miti mipya.

6. Kila kibali cha ujenzi kinachotolewa kiwe na mkakati wa upandaji miti.

Tanzania ni yetu, tupande miti kwa kizazi cha leo na kesho

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan
 
Bwana Aggrey Mwanri alianzisha hyo project alivokua mkuu wa mkoa wa Tabora. His plan was to transform Tabora to look like Toronto.

Hajakaa sawa wakamtoa. U have a very good idea lakn serikali haiez kukubali au hata ikikubali kutakua hakuna ufatiliaji.

Nadhani the best approach ingekua ku raise awareness frm family level kuhusu upandaji moti badala ya kutegemea serikali
 
Kuitunza miti nako kunahitaji maji

Kwa mfano mti ukiupanda kuanzia november ambapo mvua huanza na kukatika april tayari utakua unaweza kujisimamia na kama ni umwagiliaji utafanya kidogo sana, tatizo hatuna sera thabiti na sheria wakuzitunga na kusimamia naona hawako serious, mazingira ni suala mtambuka lakini viongozi ni kama wanacheza nalo kisiasa bila kujali athari iliyo mbele yetu.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Nimepanda miti mingi. Tatizo ni kutegemea mvua. Mara ya mwisho nimeingia hasara ya laki tano pengine na zaidi sababu ya kupanda miti.
 
Bwana Aggrey Mwanri alianzisha hyo project alivokua mkuu wa mkoa wa tabora. His plan was to transform Tabora to look like Toronto.
Hajakaa sawa wakamtoa.
U have a very good idea lakn serikali haiez kukubali au hata ikikubali kutakua hakuna ufatiliaji.
Nadhani the best approach ingekua ku raise awareness frm family level kuhusu upandaji moti badala ya kutegemea serikali

Uko sahihi kutegemea sera au jambo lifanywe na serikali ni kama kupoteza muda tu
 
Kwa mfano mti ukiupanda kuanzia november ambapo mvua huanza na kukatika april tayari utakua unaweza kujisimamia na kama ni umwagiliaji utafanya kidogo sana, tatizo hatuna sera thabiti na sheria wakuzitunga na kusimamia naona hawako serious, mazingira ni suala mtambuka lakini viongozi ni kama wanacheza nalo kisiasa bila kujali athari iliyo mbele yetu.
Boss, mvua hazitabiriki pia.
 
Ilaumiwe ccm kwa upumbavu wote unaendelea nchini
 
FB_IMG_16658087755113046.jpg
Naunga mkono hoja
 
Bwana Aggrey Mwanri alianzisha hyo project alivokua mkuu wa mkoa wa tabora. His plan was to transform Tabora to look like Toronto.
Hajakaa sawa wakamtoa.
U have a very good idea lakn serikali haiez kukubali au hata ikikubali kutakua hakuna ufatiliaji.
Nadhani the best approach ingekua ku raise awareness frm family level kuhusu upandaji moti badala ya kutegemea serikali
Alikuwa na aproach nzuri saana, inatakiwa kuendeleza
 
Mabadiliko ya tabia ya nchi ni tatizo la dunia, kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kumekuwa na athari nyingi ikiwa ni pamoja na ukame unaokumba nchi nyingi duniani. Baadhi ya nchi kwa sasa zinakosa mvua kwa kipindi cha mwaka mzima au zaidi.
Hapa ndipo nashindwa kukubaliana na wabongo, wao matatizo badala ya kuyapatia ufumbuzi yanageuzwa mchongo wa watu kupiga hela.

Tatizo letu kubwa na la msingi sio mabadiliko ya tabia nchi, sie tatizo letu kubwa na kubwa kuliko ni kile kidogo tulicho jaaliwa tunatumiaje. Kuna watu wao wakilalamika kuhusu tabia nchi na kukosa maji tunawaelewa. Hivi ni maji kiasi gani tunatumia na kiasi gani yanaenda baharini??? Hivi kweli tumeshindwa vuna maji ya mvua kwa kuweka tanks za kutosha au kuchimba mabwawa ya kutosha.

Mgao ni hulka ya watoa huduma, viongozi wa serikali, na wanasiasa. Mnatutengenezea matatizo na mnakuja na solution zenu za kiwaki. Kama hakuna maji na mnataka kupanda miti hiyo miti mtamwagilia na nini.

Tatizo ni la kwenu ila mnahamisha magoli na kuwapelekea msala watu wasiohusika kabisa. Sasa ni kweli mkipanda miti mingi ni maji mtayazuia yasiende baharini kweli??? Mvua kwetu ni ya msimu miaka yote sasa watumiaji wa maji wameongezeka manake tutunze maji yanyopatikana kwa msimu ili tuyatumie kwa kipindi chote. Hizi zingine ni siasa zile zile za kuendelea kutumia vibaya mali ya umma kama kuwajengea soko la mabilioni wajasiriamali wasio na mtaji hata wa laki moja.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom