Tatizo la maji, Itungwe Sheria kila Mtu awe na mti aliopanda

... huwa mnakumbuka haya mambo ya kupanda miti pale mnapoona negative effects; mvua zikinyesha mnasahau tena! Miti namba moja ya kutunza sio mipapai na miembe mnayopanda kwenye maeneo yenu! Miti muhimu zaidi kwa tabia nchi ni misitu ya asili ambayo wafugaji wanaohamahama na wachoma mikaa wana ugomvi nayo wa kudumu. Nchi inageuka jangwa hii!

Huwa najiuliza, kama biogas inayotokana na vinyesi vya kuku inaweza kutumika kupikia hadi kuwasha taa majumbuni, hizi stori kwamba gesi asilia ya Mtwara haifai kwa matumizi ya majumbani inatoka wapi? Hata kama inatakiwa kuwa processed ili ifae, kwanini isiwe processed wananchi wakapata nishati kwa bei nafuu?

I tell you, mtungi wa gesi 30kg ukiuzwa not more than 15,000/= zaidi ya 80% ya wananchi wata-opt gas na kuachana na mkaa na kuni na hapo ndipo serikali itakuwa na nguvu ya kutunga na ku-enforce sheria ya ku-criminalize mkaa na kuni kuwa nyara za taifa! Vinginevyo, ni kuwaonea wananchi; at 60,000/- mtungi wa gas ni wangapi wanamudu? Serikali ina sehemu ya lawama kwenye hili!
 
Hapa ndipo nashindwa kukubaliana na wabongo, wao matatizo badala ya kuyapatia ufumbuzi yanageuzwa mchongo wa watu kupiga hela.

Tatizo letu kubwa na la msingi sio mabadiliko ya tabia nchi, sie tatizo letu kubwa na kubwa kuliko ni kile kidogo tulicho jaaliwa tunatumiaje. Kuna watu wao wakilalamika kuhusu tabia nchi na kukosa maji tunawaelewa. Hivi ni maji kiasi gani tunatumia na kiasi gani yanaenda baharini??? Hivi kweli tumeshindwa vuna maji ya mvua kwa kuweka tanks za kutosha au kuchimba mabwawa ya kutosha.

Mgao ni hulka ya watoa huduma, viongozi wa serikali, na wanasiasa. Mnatutengenezea matatizo na mnakuja na solution zenu za kiwaki. Kama hakuna maji na mnataka kupanda miti hiyo miti mtamwagilia na nini.

Tatizo ni la kwenu ila mnahamisha magoli na kuwapelekea msala watu wasiohusika kabisa. Sasa ni kweli mkipanda miti mingi ni maji mtayazuia yasiende baharini kweli??? Mvua kwetu ni ya msimu miaka yote sasa watumiaji wa maji wameongezeka manake tutunze maji yanyopatikana kwa msimu ili tuyatumie kwa kipindi chote. Hizi zingine ni siasa zile zile za kuendelea kutumia vibaya mali ya umma kama kuwajengea soko la mabilioni wajasiriamali wasio na mtaji hata wa laki moja.
Ukiwa na mawazo km haya wanakuona snich wanataka wanafiki
 
Mabadiliko ya tabia ya nchi ni tatizo la dunia, kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kumekuwa na athari nyingi ikiwa ni pamoja na ukame unaokumba nchi nyingi duniani. Baadhi ya nchi kwa sasa zinakosa mvua kwa kipindi cha mwaka mzima au zaidi.

Kwa namna shughuli za binadamu zinavyoongezeka, hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi inazidi kuwa mbaya saana, uwezekano mkubwa saana baada ya miaka 10-20 kiwango cha upatikanaji wa mvua kikawa kidogo saana kuweza kutosheleza mahitaji ya binadamu kama jitihada za makusudi na kweli hazitachukuliwa.

Miaka 40 nyuma, mito mingi inayopatikana Tanzania ilikuwa inatiririka mwaka mzima, lakini kwa sasa imebaki mabonde tu yasiyo na maji hata kipindi cha mvua, tatizo ni kubwa na kadri siku zinavyokwenda tatizo linaongezeka.

Ili kupambana na athari zinazotokana na madiliko ya tabia ya nchi na kupelekea kukosekana kwa mvua ni muhimu saana ikatungwa sheria inayolazimisha upandaji wa miti kwa hapa Tanzania.

Pamoja na juhudi nzuri zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita, chini ya Mh Samia Suluhu Hassan, yafuatayo yanaweza kufanyika-:
1. Kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 (Mwenye ajira ya kudumu) apande miti mitano kila mwaka, hili linawezekana.
2. Halmashauri zote ziweke mkakati wa kuwa na Shamba la miti, haijalishi ni ndani ya eneo lao au nje ya eneo lao kiutawala- Hii itakuwa pia chanzo cha Mapato kwa Halmashauri.
3. Shule zote (Msingi na Sekondari) ziwe na Shamba la mti, kila mwanafunzi awe na mti anaouhudumia (Zile za mjini ambazo hazina maeneo utaratibu uandaliwe kwa kupanda miti hapo shuleni tu)-Walimu Wakuu na MEK wapimwe kwa kuweza kusimamia hili.
4. Ofisi zote za Umma, kuanzia ofisi za Serikali za Mtaa, Kijiji, Kata e.t.c kila Mtumishi wa eneo hilo awe na mti anao uhudumia, kusiwepo na ofisi ya Umma isiyo na miti.
5. Serikali iwezeshe kitengo cha Mazingira katika Halmashauri, Maafisa Mazingira wa Halmashauri wapimwe kwa namna wanavyosimamia upandaji wa miti mipya.
6. Kila kibali cha ujenzi kinachotolewa kiwe na mkakati wa upandaji miti.

Tanzania ni yetu, tupande miti kwa kizazi cha leo na kesho

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan
Kabla hata ya kutungwa sheria wewe umepanda miti mingapi kama mfano?
 
... huwa mnakumbuka haya mambo ya kupanda miti pale mnapoona negative effects; mvua zikinyesha mnasahau tena! Miti namba moja ya kutunza sio mipapai na miembe mnayopanda kwenye maeneo yenu! Miti muhimu zaidi kwa tabia nchi ni misitu ya asili ambayo wafugaji wanaohamahama na wachoma mikaa wana ugomvi nayo wa kudumu. Nchi inageuka jangwa hii!

Huwa najiuliza, kama biogas inayotokana na vinyesi vya kuku inaweza kutumika kupikia hadi kuwasha taa majumbuni, hizi stori kwamba gesi asilia ya Mtwara haifai kwa matumizi ya majumbani inatoka wapi? Hata kama inatakiwa kuwa processed ili ifae, kwanini isiwe processed wananchi wakapata nishati kwa bei nafuu?

I tell you, mtungi wa gesi 30kg ukiuzwa not more than 15,000/= zaidi ya 80% ya wananchi wata-opt gas na kuachana na mkaa na kuni na hapo ndipo serikali itakuwa na nguvu ya kutunga na ku-enforce sheria ya ku-criminalize mkaa na kuni kuwa nyara za taifa! Vinginevyo, ni kuwaonea wananchi; at 60,000/- mtungi wa gas ni wangapi wanamudu? Serikali ina sehemu ya lawama kwenye hili!
Jukumu la utunzaji wa Mazingira ni la watu wote, maana athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ni kwa kila mtu, Serikali inaendelea kuchukua hatua ili kupambana na uhalibifu wa mazingira ikiwemo kutoa elimu kwa Wafugaji na Wakulima. Lakini ni muhimu pia kila Mtanzania akatimiza wajibu wake kupambana na uhalibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti inayoshauriwa na Watalaamu.
 
FAIDA YA KUPANDA MITI NA KUITUNZA

Kijiji Lufilyo, Busokelo
Wilaya ya Rungwe
Mkoani Mbeya, Tanzania

HAYA NDO MAENO YA KIJIJI CHA LUFILYO

Kwa wale ambao hamjafika Nyanda za Juu za Kusini, Tanzania na hakika picha hii itawapa nini maana ya kampeni ya kuhifadhi miti na mazingira inavyozingatiwa kijijini Lufilyo, Busokelo, Wilaya ya Rungwe na kampeni inavyoweza kupokewa ktk maeneo yote ya Tanzania.
 
Hiyo itakuwa sheria ya hovyo na kijinga kuwahi kutungwa duniani. Kinachohitajika ni kupiga marufuku biashara ya mkaa na kufanya control ya population ya watu.
 
Inasikitisha kuona miti ikikatwa kupisha uwekaji wa mabango ya matangazo

IPPMedia
https://www.ippmedia.com › habari
RIPOTI MAALUM Miti inapokatwa kupisha mabango

25 Jul 2022 — Ni sura nyingine ya uharibifu wa mazingira na hata taswira yenyewe ya Mkoa wa Dar es Salaam, unaosifika kwa kuwa kitovu cha ...
1666860025265.png

Picha: Miti iliyokatwa jijini Dar es Salaam ili kutoa nafasi ya kujenga mabango makubwa ya kutangaza biashara, huduma n.k

N.B
Je zama hizi za kidijitali wafanyabiashara hawawezi kutumia majukwaa ya kidijitali kujitangaza badala ya kuharibu mazingira na mandhari?
 
Hilo ndilo tatizo la msingi hasa, ukataji miti kwa mkaa, kuni na magogo inasababisha janga la kimazingira duniani kote.
Kipindi ya mzee wa msoga, miti ilikuwa inakatwa huko Meru balaaa, unapishana na malori ya magogo hapo Namanga yakienda Kenya kila kukicha....siku hizi hapo Meru hamna kitu, hata magogo biashara imeisha. mito iliyokuwa inapitisha maji safi kibao hapo Arusha mingi imekauka...
 
Mikoa ya Iringa Njombe na Mbeya kilimo cha miti ya kibiashara kv maparachichi na miti ya mbao angalau imesaidia uoto wa miti unaongezeka miaka ya hivi karibuni.

Kwa mikoa mingine hasa kanda ya kati na Pwani nadhani zoezi hili pendekezwa ni muhimu sana, sheria itasaidia kuongeza uwajibikaji wa wananchi ktk kutunza mazingira.
 
Hapa tatizo sio miti wala hali ya hewa
Tatizo ni serikali kutokuwa na nia ya dhati ya kusambaza maji ya uhakika kwa wananchi.
Israel ndio nchi inayoongoza kwa kilimo cha umwagiliaji duniani licha ya kuwa nchi hiyo ni jangwa.

Israel wamefanikiwa sana kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa kuchukua maji kwa mabomba kutoka mto Jordan na mto Nile na kuyasambaza nchi nzima. Wametumia vyema maji hayo kwenye kilimo na wameidhihirishia dunia kuwa hakuna kinachoshindikana. Ardhi ya Israel haina rutuba hivyo walikwenda kuchukua udongo kwenye nchi zingine na kuutumia kwenye kilimo na sasa wanaongoza duniani kwenye kilimo cha umwagiliaji.

Tujaribu kutafakari nchi ambayo ni jangwa, haina rutuba lakini wamefanikiwa si tu kuwa na maji ya matumizi ya nyumbani bali kuyatumia kwenye kilimo na kuuza mazao yao dunia nzima
Sisi ambao ndio tuna ziwa Victoria ambalo ndio chanzo cha mto Nile tunalia maji ya kunywa kweli?

Hivi inashindikanaje kuchukua maji ya ziwa victori ambayo ni maji ya uhakika mwaka mzima na kuyasambaza nchinzima nini kinashindikana?
Kama iliwezekana kujenga bomba la mafuta kutoka Tanzania mpaka Zambia (tena miaka hiyo kitambo) inashindikanaje leo kujenga bomba la maji kutoka Mwanza mpaka Dar na kwingineko?
Kama imewezekana kujenga reli ya kisasa kutoka Dar mpaka Mwanza nini kinazuia maji kutoka ziwa Victoria kusambazwa nchini?

Tanzania hatuna shida ya maji tuna shida ya viongozi wazalendo ambao wanajua wanananchi wanataka nini kabla ya kufikiria matumbo yao
Najiuliza fèdha walizonunulia ndege zisingeweza kutandika bomba la maji kutoka mwanza mpaka dar na baadae kusambaa nchi nzima?
Kipi kilipaswa kuanza kati ya ununuzi wa mandege yanayotupa hasara kila siku na ujenzi wa bomba kubwa la maji kutoka victoria kusambaza nchi nzima? hivi serikalini hakuna anayefikiria hili?

Maji sio tu afya bali ni ajira, tatizo la maji na umeme likipatiwa ufumbuzi wa kudumu litapunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kiasi kikubwa.
 
Hiyo itakuwa sheria ya hovyo na kijinga kuwahi kutungwa duniani. Kinachohitajika ni kupiga marufuku biashara ya mkaa na kufanya control ya population ya watu.
Bora iwe sheria mbovu lakini isaidie, Kupiga marufuku biashara ya mkaa kunahitaji sheria. hata hivyo si rahisi kupiga marufuku biashara ya mkaa bila kuandaa mazingira,
 
Mabadiliko ya tabia ya nchi ni tatizo la dunia, kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kumekuwa na athari nyingi ikiwa ni pamoja na ukame unaokumba nchi nyingi duniani. Baadhi ya nchi kwa sasa zinakosa mvua kwa kipindi cha mwaka mzima au zaidi.

Kwa namna shughuli za binadamu zinavyoongezeka, hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi inazidi kuwa mbaya saana, uwezekano mkubwa saana baada ya miaka 10-20 kiwango cha upatikanaji wa mvua kikawa kidogo saana kuweza kutosheleza mahitaji ya binadamu kama jitihada za makusudi na kweli hazitachukuliwa.

Miaka 40 nyuma, mito mingi inayopatikana Tanzania ilikuwa inatiririka mwaka mzima, lakini kwa sasa imebaki mabonde tu yasiyo na maji hata kipindi cha mvua, tatizo ni kubwa na kadri siku zinavyokwenda tatizo linaongezeka.

Ili kupambana na athari zinazotokana na madiliko ya tabia ya nchi na kupelekea kukosekana kwa mvua ni muhimu saana ikatungwa sheria inayolazimisha upandaji wa miti kwa hapa Tanzania.

Pamoja na juhudi nzuri zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita, chini ya Mh Samia Suluhu Hassan, yafuatayo yanaweza kufanyika-:
1. Kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 (Mwenye ajira ya kudumu) apande miti mitano kila mwaka, hili linawezekana.
2. Halmashauri zote ziweke mkakati wa kuwa na Shamba la miti, haijalishi ni ndani ya eneo lao au nje ya eneo lao kiutawala- Hii itakuwa pia chanzo cha Mapato kwa Halmashauri.
3. Shule zote (Msingi na Sekondari) ziwe na Shamba la mti, kila mwanafunzi awe na mti anaouhudumia (Zile za mjini ambazo hazina maeneo utaratibu uandaliwe kwa kupanda miti hapo shuleni tu)-Walimu Wakuu na MEK wapimwe kwa kuweza kusimamia hili.
4. Ofisi zote za Umma, kuanzia ofisi za Serikali za Mtaa, Kijiji, Kata e.t.c kila Mtumishi wa eneo hilo awe na mti anao uhudumia, kusiwepo na ofisi ya Umma isiyo na miti.
5. Serikali iwezeshe kitengo cha Mazingira katika Halmashauri, Maafisa Mazingira wa Halmashauri wapimwe kwa namna wanavyosimamia upandaji wa miti mipya.
6. Kila kibali cha ujenzi kinachotolewa kiwe na mkakati wa upandaji miti.

Tanzania ni yetu, tupande miti kwa kizazi cha leo na kesho

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan
Ni kweli ila nadhani sisi wabantu bado tuna kasumba ya kudhani miti inajiotea yenyewe,Kageme kafanikiwa katika hili.Utakuta mtu akipata kiwanja tu miti ni kufyekwa tu na wasomi wapo ajirani kwa sababu walisoma ili wapate mishahara na sio kuisaidia jamii ikabiliane na changamoto.
 
Mabadiliko ya tabia ya nchi ni tatizo la dunia, kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kumekuwa na athari nyingi ikiwa ni pamoja na ukame unaokumba nchi nyingi duniani. Baadhi ya nchi kwa sasa zinakosa mvua kwa kipindi cha mwaka mzima au zaidi.

Kwa namna shughuli za binadamu zinavyoongezeka, hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi inazidi kuwa mbaya saana, uwezekano mkubwa saana baada ya miaka 10-20 kiwango cha upatikanaji wa mvua kikawa kidogo saana kuweza kutosheleza mahitaji ya binadamu kama jitihada za makusudi na kweli hazitachukuliwa.

Miaka 40 nyuma, mito mingi inayopatikana Tanzania ilikuwa inatiririka mwaka mzima, lakini kwa sasa imebaki mabonde tu yasiyo na maji hata kipindi cha mvua, tatizo ni kubwa na kadri siku zinavyokwenda tatizo linaongezeka.

Ili kupambana na athari zinazotokana na madiliko ya tabia ya nchi na kupelekea kukosekana kwa mvua ni muhimu saana ikatungwa sheria inayolazimisha upandaji wa miti kwa hapa Tanzania.

Pamoja na juhudi nzuri zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita, chini ya Mh Samia Suluhu Hassan, yafuatayo yanaweza kufanyika-:
1. Kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 (Mwenye ajira ya kudumu) apande miti mitano kila mwaka, hili linawezekana.
2. Halmashauri zote ziweke mkakati wa kuwa na Shamba la miti, haijalishi ni ndani ya eneo lao au nje ya eneo lao kiutawala- Hii itakuwa pia chanzo cha Mapato kwa Halmashauri.
3. Shule zote (Msingi na Sekondari) ziwe na Shamba la mti, kila mwanafunzi awe na mti anaouhudumia (Zile za mjini ambazo hazina maeneo utaratibu uandaliwe kwa kupanda miti hapo shuleni tu)-Walimu Wakuu na MEK wapimwe kwa kuweza kusimamia hili.
4. Ofisi zote za Umma, kuanzia ofisi za Serikali za Mtaa, Kijiji, Kata e.t.c kila Mtumishi wa eneo hilo awe na mti anao uhudumia, kusiwepo na ofisi ya Umma isiyo na miti.
5. Serikali iwezeshe kitengo cha Mazingira katika Halmashauri, Maafisa Mazingira wa Halmashauri wapimwe kwa namna wanavyosimamia upandaji wa miti mipya.
6. Kila kibali cha ujenzi kinachotolewa kiwe na mkakati wa upandaji miti.

Tanzania ni yetu, tupande miti kwa kizazi cha leo na kesho

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan
Wizara ya mazngira jukumu lake nini ,wizara inapewa mgawo wa budget na hizo pesa kwanini zisipelekwe kuenda kutunza vianzo vya mto,na maeneo mengineo ambayo yanaweza kukontrol uwezo wa kuwepo maji?.sheria ya kutunza mazngira ipo.kazi ni serikali kushindwa kupeleka pesa kutunza vianzo, na miti ipandwa ya matunda ili matumizi yake yawe ya kimazingira na kiuchumi sio ipandwe mianzi kwa ajili ya Ulanzi tu.miti iwe stragic kwa chakula na biashara kw vizazi na vizazi. Serikali inashindwa nini?
 
Jukumu la utunzaji wa Mazingira ni la watu wote, maana athari za mabadiliko ya tabia ya nchi ni kwa kila mtu, Serikali inaendelea kuchukua hatua ili kupambana na uhalibifu wa mazingira ikiwemo kutoa elimu kwa Wafugaji na Wakulima. Lakini ni muhimu pia kila Mtanzania akatimiza wajibu wake kupambana na uhalibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kupanda miti inayoshauriwa na Watalaamu.
... nikipanda miti miwili mitatu ya kivuli hapa nje kwangu at the same time wachoma mikaa, warina asali, wafugaji, n.k wanateketeza maelfu ya ekari ya miti asilia kwa siku sidha kama itasaidia sana kupambana na hili janga.

Serikali iweke plan nzuri ya ardhi na maliasili hususan misitu ya asili. Atakayekamatwa anateketeza misitu iingie kwenye kosa la uhujumu uchumi! Ila hilo sio sahihi kufanyika wakati wananchi hawana option - mfano nishati. Shusha bei ya gas to affordable prices; I tell you wala huhitaji kutunga sheria ya ku-criminlze mkaa; wananchi wenyewe wataachana nao.
 
Back
Top Bottom