Tatizo la maji, Itungwe Sheria kila Mtu awe na mti aliopanda

Mabadiliko ya tabia ya nchi ni tatizo la dunia, kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kumekuwa na athari nyingi ikiwa ni pamoja na ukame unaokumba nchi nyingi duniani. Baadhi ya nchi kwa sasa zinakosa mvua kwa kipindi cha mwaka mzima au zaidi.

Kwa namna shughuli za binadamu zinavyoongezeka, hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi inazidi kuwa mbaya saana, uwezekano mkubwa saana baada ya miaka 10-20 kiwango cha upatikanaji wa mvua kikawa kidogo saana kuweza kutosheleza mahitaji ya binadamu kama jitihada za makusudi na kweli hazitachukuliwa.

Miaka 40 nyuma, mito mingi inayopatikana Tanzania ilikuwa inatiririka mwaka mzima, lakini kwa sasa imebaki mabonde tu yasiyo na maji hata kipindi cha mvua, tatizo ni kubwa na kadri siku zinavyokwenda tatizo linaongezeka.

Ili kupambana na athari zinazotokana na madiliko ya tabia ya nchi na kupelekea kukosekana kwa mvua ni muhimu saana ikatungwa sheria inayolazimisha upandaji wa miti kwa hapa Tanzania.

Pamoja na juhudi nzuri zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita, chini ya Mh Samia Suluhu Hassan, yafuatayo yanaweza kufanyika-:

1. Kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 (Mwenye ajira ya kudumu) apande miti mitano kila mwaka, hili linawezekana.

2. Halmashauri zote ziweke mkakati wa kuwa na Shamba la miti, haijalishi ni ndani ya eneo lao au nje ya eneo lao kiutawala- Hii itakuwa pia chanzo cha Mapato kwa Halmashauri.

3. Shule zote (Msingi na Sekondari) ziwe na Shamba la mti, kila mwanafunzi awe na mti anaouhudumia (Zile za mjini ambazo hazina maeneo utaratibu uandaliwe kwa kupanda miti hapo shuleni tu)-Walimu Wakuu na MEK wapimwe kwa kuweza kusimamia hili.

4. Ofisi zote za Umma, kuanzia ofisi za Serikali za Mtaa, Kijiji, Kata e.t.c kila Mtumishi wa eneo hilo awe na mti anao uhudumia, kusiwepo na ofisi ya Umma isiyo na miti.

5. Serikali iwezeshe kitengo cha Mazingira katika Halmashauri, Maafisa Mazingira wa Halmashauri wapimwe kwa namna wanavyosimamia upandaji wa miti mipya.

6. Kila kibali cha ujenzi kinachotolewa kiwe na mkakati wa upandaji miti.

Tanzania ni yetu, tupande miti kwa kizazi cha leo na kesho

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan
Naunga mkono hoja
 
Kutoa maji Ziwa Victoria kusambaza nchi nzima kunahitaji kupanda miti?
Ni kwanini kila tatizo likitokea ccm inatafuta vijana wa kupumbaza watu mitandaoni badala ya kuongea ukweli na kutafuta njia za kutatua tatizo

Leo hii mnawezaje kuwaaminisha watu wenye akili timamu kwamba Tanzania hakuna maji
How?

Ziwa Victoria hakuna maji???
 
Mabadiliko ya tabia ya nchi ni tatizo la dunia, kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi kumekuwa na athari nyingi ikiwa ni pamoja na ukame unaokumba nchi nyingi duniani. Baadhi ya nchi kwa sasa zinakosa mvua kwa kipindi cha mwaka mzima au zaidi.

Kwa namna shughuli za binadamu zinavyoongezeka, hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi inazidi kuwa mbaya saana, uwezekano mkubwa saana baada ya miaka 10-20 kiwango cha upatikanaji wa mvua kikawa kidogo saana kuweza kutosheleza mahitaji ya binadamu kama jitihada za makusudi na kweli hazitachukuliwa.

Miaka 40 nyuma, mito mingi inayopatikana Tanzania ilikuwa inatiririka mwaka mzima, lakini kwa sasa imebaki mabonde tu yasiyo na maji hata kipindi cha mvua, tatizo ni kubwa na kadri siku zinavyokwenda tatizo linaongezeka.

Ili kupambana na athari zinazotokana na madiliko ya tabia ya nchi na kupelekea kukosekana kwa mvua ni muhimu saana ikatungwa sheria inayolazimisha upandaji wa miti kwa hapa Tanzania.

Pamoja na juhudi nzuri zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya sita, chini ya Mh Samia Suluhu Hassan, yafuatayo yanaweza kufanyika-:

1. Kila Mtanzania mwenye umri wa miaka 18 (Mwenye ajira ya kudumu) apande miti mitano kila mwaka, hili linawezekana.

2. Halmashauri zote ziweke mkakati wa kuwa na Shamba la miti, haijalishi ni ndani ya eneo lao au nje ya eneo lao kiutawala- Hii itakuwa pia chanzo cha Mapato kwa Halmashauri.

3. Shule zote (Msingi na Sekondari) ziwe na Shamba la mti, kila mwanafunzi awe na mti anaouhudumia (Zile za mjini ambazo hazina maeneo utaratibu uandaliwe kwa kupanda miti hapo shuleni tu)-Walimu Wakuu na MEK wapimwe kwa kuweza kusimamia hili.

4. Ofisi zote za Umma, kuanzia ofisi za Serikali za Mtaa, Kijiji, Kata e.t.c kila Mtumishi wa eneo hilo awe na mti anao uhudumia, kusiwepo na ofisi ya Umma isiyo na miti.

5. Serikali iwezeshe kitengo cha Mazingira katika Halmashauri, Maafisa Mazingira wa Halmashauri wapimwe kwa namna wanavyosimamia upandaji wa miti mipya.

6. Kila kibali cha ujenzi kinachotolewa kiwe na mkakati wa upandaji miti.

Tanzania ni yetu, tupande miti kwa kizazi cha leo na kesho

Mungu ibariki Tanzania
Mungu mbariki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan
Hizo tozo zijenge mabwawa mengi ya kuhifadhi maji ya mvua, yatasaidia pia kilimo
 
Back
Top Bottom