Tatizo la kula/kutafuna kucha

Kwenye hili la kucha nakubaliana nao kabisa. Nawajua watu kadhaa wa karibu walaji kucha waliobobea kitu kimoja kuhusu hawa jamaa huwa hawaumwi na kila kitu wao wanakula tu. Kama umesoma article inasema ulaji kucha kwa watoto ina maana watakula na uchafu na hatimaye mwili wao kujenga immunity ili kupambana na magojwa hivyo immunity zao kuwa strong zaidi. Nadhani ni very reasonable
Ni sawa lakini tuangalie madhara kuliko faida kwenye hili...hivi kweli tujenge immune kwa kuharibu kucha zetu? Hili ni tatizo kubwa kuliko hilo na kuwa na kinga ya magonjwa Bufa
Uzuri/ubaya wa kitu tunapima kwenye mizani...je itaegemea upande upi? Wa faida ama hasara?
 
View attachment 387667

Hiki kitu kina waathirika wengi sana wake kwa waume wakubwa kwa wadogo. Tunaweza kudhani tu kuwa ni tabia mbaya au mazoea! La hasha kutafuna kucha za vidole vya mikononi ni tatizo la kisaikolojia linalomla mtu ndani kwa ndani kwenye ufahamu wake ambapo hupelekea viashiria hivi:-

-woga
-mawazo/msongo wa mawazo
-kutojiamini
-fadhaa/sononi
-kukosa la kufanya
-taharuki
-mapepe/restless mind
-hulka ya kuiga

Hivyo ni viashiria vikuu vya mtafuna kucha na hili jambo hufanya bila kupenda ni involuntary action. Kuna baadhi hufanya wakiwa pekeyao kwenye upweke na wengine hufanya pindi anapokutana na mtu kwa mara ya kwanza ama hadhira.

View attachment 387681

Kwakuwa hili ni tatizo la kisaikolojia zaidi basi hata tiba yake ni ya kisaikolojia, hasa hasa

-councelling/ushauri nasaha
-kumjengea uwezo wa kujiamini mwathirika
-kutafiti kupitia yeye mwenyewe chanzo cha tatizo lake hilo na muda

Wengine hukutana na hii hali katika hatua fulani ya makuzi na ikipita tatizo hujitibu lenyewe!

Je una tatizo kama hili ama ndugu yako? Ama rafiki? Usikimbilie kwa mganga wa kienyeji utaambiwa una jini njaa..! Tiba unayo mwenye
hiyo picha ungeweka ya mtu mweusi ujumbe wako usingefika?
 
Jaribu hizo tiba mbalimbali nimeona na aloe Vera kumbe pia ni dawa
Sasa mkuu iyo dawa itanitibu kisaikolojia? Maana nikiwa na stress au mtu akiniudhii huwa sipendi kuongea nakata tu kucha zangu na si wakati wote
 
Sasa mkuu iyo dawa itanitibu kisaikolojia? Maana nikiwa na stress au mtu akiniudhii huwa sipendi kuongea nakata tu kucha zangu na si wakati wote
Hapana hizi ni kwa ajili ya Ladha ishu ya kisaikolojia ukipenda ni mpaka tuonane
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom